Tunduma: Mkutano wa CHADEMA mbunge Mhe. Mwakajoka akiongea na wananchi

Mhhhh watu kumbe bado wana imani na chadema. Ukisikiliza maneno ya akina pole pole unaweza dhani chadema imekufa. Nimeamini kumbe kuwa upinzani ni kama imani ambayo ipo mioyoni
Ni kweli upinzani ni itikadi.
Tatizo lipo ndani ya vyama ndio maana watu wanahama baada ya kuona figisu ndani ya Chama.
Mfano Wenyeviti kukaa madarakani kwa muda mrefu huku wakijiona kama vile maamiri jeshi wakuu ndani ya vyama na kuanza kufukuza viongozi na wanachama ndio tatizo.

Kuna watu wameondoka CDM baada ya kuona kuwa chama kimeingia hali Fulani ya udikteta wakati chama kilianza vizuri kujenga misingi ya Demokrasia.

Huwezi kujenga na kupigania demikrasia bila kuanzia chini.
Mtu aking"ang"ania madaraka madogo hata akipewa nchi atang"ang"ania .

Ni Mpango wa Mungu serikali ya CCM kuwa kama ilivyo lakini pia ni mpango wa Mungu Mbowe kuwekwa gerezani.
Mbowe angekua bado uraiani akiongoza chama hakika viongozi na wabunge na madiwani wengi wangekimbia japo mioyoni mwao wanaipenda Chadema lakini wanakwazwa na Mwenyekiti na kundi lake wanaoendekeza majungu badala ya kujenga chama.

Chadema kina wanachama na mashabiki wengi.
Busara iliyotumika kwa Kubenea na Komu ingetumiwa kwa Zito na Mkumbo leo chama kingekua kwa kasi zaidi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
By Mwakajoka
FB_IMG_1550726663674.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom