TUKUTUKU
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 11,763
- 4,041
Hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA imeelezwa kwamba ni shwari na hakuna matafaruku utakaotokea.Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni,Tindu Lissu,pamoja na Naibu katibu mkuu wa chadema Zitto kabwe walisema hayo kwa nyakati tofauti walipohojiwa kufuatia hatua ya wabunge wa 10,akiwemo naibu katibu mkuu wake,Zitto Kabwe kutokana na kupingana na msimamo wa chama hicho wa kutoka nje ya bunge wakati Rais Kikwete alipokuwa akihutubia bunge.
Hakuna mgogoro wowote baina ya viongozi wa chama bali kilichopo ni taratibu za kinidhamu na sio mgogoro wala mgongano wowotealisema.Akizungumza jana,Lissu alisema hakuna mpasuko,mgogoro wala mgongano wowote ndani ya chama hicho na kwamba kilichopo ni masuala ya kawaida yanayojadiliwa na vikao vya chama na kwamba hayawezi kuvuruga mshikamano uliyopo ndani ya chama hicho.
Kwa upande wake zitto kabwe alisema,hakuna mgogoro wowote ndani ya chama hicho na kwamba taratibu za kinidhamu haziwezi kuitwa mgogoro hata siku moja.Zitto alisema watu wengi wanakesha wakikiombea mabaya chama hicho na wengine kufikia hatua ya kusema uongo kwa nia ya kuleta chokochoko ,na akasisitiza haoni mgogoro wowote na kutaka wanaozusha maneno hayo watofautishe tofauti ya mgogoro na taratibu za kinidhamu.Zitto alisema wakati umefika kwa watanzania kujenga tabia ya kuimarisha vyama na sio kubomoa kama ulivyo sasa ambapo jambo dogo linakuzwa.[Mwananchi,6 Desemba 2010,pp 5]
My take
Mnaokodolea macho na kuombea chadema iingie kwenye mgogorona hatimaye kufa kabisa,hamta fanikiwa kamwe!CHADEMA ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo na kushamiri kwa kasi zaidi,hari zaidi na nguvu zaidi.Mungu ibariki CHADEMA,mungu ibariki Tanganyika.