Tundu Lissu yuko sahihi: Majaji wengi hawajahitimu vyuo na elimu zao ni za mitandaoni

Lissu ameamua kupambana na jinai ambayo wengi waliiogopa. Ni ukweli kuwa mahakama zetu hazina hadhi wala maana kama zamani. Lissu ametoa ushahidi wa majaji vihiyo hata watoa rushwa waliopewa ujaji na Jakaya. Aliwataja Zainab Mruke na Nyangalika ambao kusema ukweli hata elimu yao ni ya mashaka. Muruke hata final paper yake alifanyiwa. Alipata masters kiajabu sijui kwa kuvua chu.. Kwa wanaojua hawa majaji wanashangaa jinsi vituko kama hivi vinaweza kuitwa majaji. Ukichanganya na ile ya wahalifu kama Mwanaidi Majaar kupewa ubalozi unabaki kushangaa. Mungu inusuru Tanzania na hili balaa linaloitawala kwa sasa.
 
kabla hata Tundu Lisu hajaongelea uteuzi wa majai wengi wetu tulikuwa tunafahamu teuzi zilikuwa na walakini kama teuzi mbalimbali zilizofanywa na awamu ya nne zikiwamo za wakuu wa wilaya ambao wana tuhuma mbalimbali kwa hili la mahakama inaonekana mkuu wa nchi ashauriwi vibaya bali ni mtu asiye makini kwenye maamuzi yake.Amekuwa mzito si kutoa maamuzi bali hata kutoa matamko kwa kifupi maamuzi yake mengi yamejaa dosari kiasi kwamba hata ndani ya chama chake wanamlaumu wengine kwa wazi na wengine kwa kificho hata aliyekuwa mshirika wake wa karibu Edward Lowasa naye ameanza kutoa kauli zinazoashiria hawako pamoja kama elimu kwanza,tusiwe na haraka ya kuchimba gesi ingawa hatujui kama kauli hizo ni za dhati au za kujipalilia njia mwaka 2015.Watu wa utumishi ambao wanahusika na teuzi mbalimbali wamekuwa wakiwekwa kando kwa makusudi ingawa baadae wanatupiwa lawama.Tulianza kulalamikia teuzi za mabalozi.wakuu wa mikoa na wilaya na kama umepata habari juzijuzi Mengi ametakiwa kuweka Deposit kubwa katika kesi aliyofungua Uingereza na moja ya kigezo ni rushwa iliyokithiri kwenye vyombo vya sheria Tanzania.Ni kweli tuna uhaba wa majaji lakini tunahitaji watu wenye Quality na sio Quantity
 
Ripoti yake hiyo ambayo inachukua sura ya kutaka kulifanya Bunge ni chombo cha kuisimamia mahakama, na hivyo kupoteza tafsir na mantiki ya mihimili mitatu ya serikali ya Tanzania. Kwa mujibu wa ibara ya 107 A, mamlaka ya kufasir sheria na kutoa haki yako mikononi mwa mahakama. Hakuna hata sehemu moja katika Katiba ambapo Bunge limepewa mamlaka yoyote ya kuisimamia na kuishauri mahakama.

Nafasi ya Bunge kuirekebisha mahakama katika mfumo wa "checks and balance" ni kwa njia ya kutunga sheria TU. Kwa kitendo cha kuisoma ripoti hiyo katika hadhara ya Bunge na kulitumia Bunge kuidhalilisha mahakama na majaji wake ni wazi Mhe. TUNDU analenga kulichonganisha Bunge na Mahakama.
Kiukweli hapa Tanzania, hatuna kabisa "The doctrine of Separation of powers" kilichopo ni kiini macho, na alichokifanya Tundu Lissu ni kuuthibitisha tuu udhaifu huu!.

Kazi ya bunge zaidi ya kutunga sheria, pia ni kuisimamia serikali, na kuithibiti mahakama!. Kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria, kuithibiti serikali na kulidhibiti bunge, na kazi ya serikali ni to provide kwa bunge na mahakama na kuendesha nchi kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na bunge, na kusimamiwa na mahakama!. Hivyo kila chombo ni big brother aki watch over and above mhimili mwingine ili kujenga hizo checks and balance, lakini kwa Tanzania ni shaghala bagala, Serikali ndio kila kitu, ikifuatiwa na bunge na mwisho ni mahakama!.

Rais wetu ni sehemu ya bunge, anaweza kulivunjilia mbali bunge as he pleases!, bunge likishatunga sheria, sheria hiyo haiwi sheria mpaka rais aikubali, na akiikataa bunge halina uwezo wa kufanya lolote, kwa sababu rais anaweza kulivunjilia mbali anytime!. Hivyo mbele ya rais, bunge si lolote sii chochote!.

Rais ndiye anayemteua Jaji Mkuu, bila any imput toka bunge, mahakama ikitoa capital punishment, adhabu hiyo haitekelezwi mpaka rais airidhie, rais anaweza kuamua kutotekeleza adhabu yoyote, kuwasamehe wafunga wowote, na kwa Tanzania hata kuzuia wahalifu kama ile mijizi ya EPA kupewa msamaha bila kufikishwa mahakamani ambapo ni uvunjaji wa katiba ya JMT, lakini hakuna mwenye uwezo wa kumfanya chochote rais, hivyo mbele ya rais, mahakama sii lolote, sii chochote!.

Kwa mtaji huo, Lissu is very right, bunge linapaswa kuidhibiti mahakama na ilipaswa jaji mkuu aridhiwe na bunge kama anavyoridhiwa waziri mkuu!. Bunge pia ndilo lilipaswa liwe supreme kwa sababu ndilo lililochaguliwa na watu, na sio serikali!. Hapa kwetu serikali ndio kila kitu, rais wetu ni Alfa na Omega!.

Pasco.
 
nisimgependa kukukwaza mkuu ASENGA WA PAKAYA, hasa ukizingatia sikukuu ya eid ndo hiyoo, lakini naomba kukutaarifu kuwa wanadamu tunapishana uwezo, vipaji na karama tofauti. Kimsingi kila mmoja anapaswa kutambua kipi hana na kipi kajaliwa, lakini ukishindwa kujitambua basi hatuna budi kukutaarifu.

Kwakweli wewe kitu kinachoitwa "ANALYTICAL SKILLS" huna kabisaaaaaaaaaaaaaa. so nakushauli kujifua kidogo katika hili eneo ili eweze kufit vizuri humu jukwaani,la sivyo utakuwa upset sana mkuuu

ashakum si matusi
 
Asenga good try kwa upande wako maana mi huwa napenda sana side comments nategemea na wengine wataleta uchambuzi mbadala wa ripoti.
 
Mleta Hoja unatupotezea mudA kusoma uetetezi wa mtu aliyekalia kiting cha jaji na tena jaji kiongozi kinyume cha katiba
 
Kusema kweli kwa ile taarifa ya Lissu chombo cua mahakama kimeonekana ni cha ajabu ajabu na watu walioisoma wamekosa imani kabisa na chombo hiki ambacho kinatakiwa kiwe ni chombo cha haki kischo na mawaa kama aliyoyaainisha Lissu.
Mkuu, Lisu kaja ongezea ushahidi wa lile walijualo wananchi. Haiaminiki.majaji, mahakimu, waendesha mashtaka, na makarani wote hawaaminiki ama kwa rushwa au uwezo mdogo. Ukiwa na kesi au ya nduguyo mahakama ya kinondoni, kwa mfano, nenda na pesa ya kutosha. Hakuna sehemu yenye transaction kubwa kama mahakamani.
 
Sidhani kama ni makosa kwa Tundu Lissu ku expose udhaifu wa mahakama,maana upo na siku zote mficha maradhi kifo humuumbua!
 
Mleta thread yaelekea huna huruma na Taifa letu, hivi hawa majaji walioteuliwa na hukumu zinazosomwa katika mahakama zetu we unaona ni sawa tu. Hata hivyo watawala wetu wanaongoza kuteua watu wasio na maadili kwenye nafasi nyeti za uongozi ila tu awe ni swahiba wa mtawala fulani. Mifano iko mingi hii ni aibu kwa Taifa.
 
Huu utamaduni wa kufumbia maovu yanayofanywa na majaji wasionauwezo wa kuibeba hiyo dhamana sasa umefika mwisho. Mi si mtaalam wa sheria ila nilikuwa napata mashaka na maamuzi yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya majaji, lissu nampongeza kwa kufichua madudu yanayofanywa na hawa watu ambao wengi wao wameteuliwa na jk labda inawezekana anafanya hivyo kwaajili kutaka kukontro maamuzi kwa kutoa maamuzi kadri ya maelekezo yake
 
KIBALAGHASHIA? Kwani huyo bwana aliyekuwa amevaa kibalaghashia alikuwa msikitini au mahakamani? Ni kweli KIBALAGHASHIA ni vazi maalumu la dini fulani lakini mahakama haina dini na kwahiyo haikuwa sahihi kwa mtu awaye yote kuvaa KIBALAGHASHIA mahakamani.
Hata hivo mkuu ASENGA WA PAKAYA ripoti ya TL imetokana na ripoti mbalimbali ambazo zipo katika taasisi ya mahakama, hakuna hata kitu kimoja ambacho TL amekitaja hakijatokana na kumbukumbu za mahakama. Mimi ningezani ungempongeza TL kwa ripoti yake ya kitaaluma ambayo itawasaidia watu wengi kuona udhaifu uliopo katika taasisi nyeti kama ya mahakama.
 
Tatizo mtoa mada unamchukulia kirahisi sana Mh. TL...kwa taarifa yako mkuu wa nchi anamuogopa huyu afadhali ya ukoma

jk mwenyewe alishasema ni bora slaa akachukua nchi lakini sio lisu. Huyu mleta mada kachemka, anataka kumtetea hata yule jaji ambaye hana bachelor ya law?
 
Ni muda sasa umepita bila ya mimi kuchangia hoja humu,ila jambo la muhimu kulitia kichwani ni kuwa.maisha na siasa za Tanzania hazipo static,na tunapolizungumza hili tunakuwa na uhalali wa kulijadili kwa kuunganisha hoja hii na ushaidi mwingine wa kihistoria.

Lissu alijenga hoja bungeni,wanafiki wakampinga, akaambiwa afute kauli,akakataa, akaagizwa kuleta ushaidi na akafanya hivyo.

Mpaka mda huu hakuna hata msemaji yoyote wa serikali aliyepingana na mh lisu,ushaidi wa ndugu Lissu si wakufikirika,ni hoja yenye mashiko,kutokea mtu kama huyu aliyetoa mada hii na kuchomoa moja ya hoja ya lissu na kuipa picha ya udini ni uhuni.pia kumwita mtu tundu la ndege ni uhuni. Na wewe mtoa mada tunakujua kwa kutaka kupata umaarufu kwa kupitia huyu bwana.

Tumekujua rangi yako huwez tusumbua.
 
Kusema kweli kwa ile taarifa ya Lissu chombo cua mahakama kimeonekana ni cha ajabu ajabu na watu walioisoma wamekosa imani kabisa na chombo hiki ambacho kinatakiwa kiwe ni chombo cha haki kischo na mawaa kama aliyoyaainisha Lissu.

kimbunga wewe ni mgeni au hauishi tz jaribu kupitia kessi mbali mbali au kusikia tu mwenye kesi mahakamani ndio utajuwa hii nchi hakuna mahakama .....ni ya wenye pesa tu ...unaweza kupanga hukumu na hakimu ndie atakufundisha .

assenga anasahau kwamba bunge linatunga sheria na kusimamiwa na mahakama je ni kosa gani alietunga hio sheria akiona haifuatwi si ni lazima ahoji?
 
..nilipoisoma makala ya Tundu Lissu akiitaja kesi ya "kibaragashia" I knew this was coming.

..Tundu Lissu alitakiwa awe makini zaidi na zaidi na kuielewa hadhira anayo-deal nayo.

..ukiachilia suala la "kibaragashia," naamini hoja ya Tundu Lissu imejaa madai mazito na serikali inapaswa kuyafanyia kazi.

..Tundu Lissu hajaidhalilisha mahakama. Raisi ndiye ameidhalilisha mahakama yetu kwa kuteua majaji wenye maadili na rekodi zenye mawaa.
Jokakuu,
Huenda kuna mengine pia mheshimiwa Tundu Lissu kachemka.

Mimi nalijua moja la huyo jaji Sekela ambaye Tundu anasema hakupendekezwa na tume ya uajiri. Ukweli ni kwamba Tanzania hakuna jaji anayeitwa Sekela Mushi, huyo mama anaitwa Sekela Cyril Moshi.

Sasa kwa mtu ambaye analalamikia ubabaishaji wa majaji, ningetegemea awe makini sana na kuhakikisha utetezi wake hauna makosa kama haya. Kwa Tanzania Mushi na Moshi ni surnames tofauti kabisa.

Huyu mama ni mzoefu na wa zamani sana kwenye mahakama na wanaomfahamu walitegemea hata awe jaji miaka mingi iliyopita. Kwa shuleni (UDSM) alikuwa na uwezo mzuri sana na pia aliteuliwa kuwa magistrate mapema sana kuliko hata wenzake aliosoma nao. Kuwa jaji ndio amechelewa sana kuupata mpaka miaka miwili iliyopita. Ndio maana hata mimi nashangaa, unelss huyu mama ana makosa ambayo sisi hatuyajui na Tundu angesaidia kuyaweka wazi kama anayajua, ni ngumu sana kuamini huyu mama hakupendekezwa na tume ya uajiri. Kumwita mama kama huyo katolewa vichochoroni ni dai zito sana ambalo lazima liambatane na maelezo zaidi, vinginevyo anakuwa amemchafua mno.

I hope hapa hatuongelei misteken identity. Maana unaweza kwenda tume ya uajiri kutafuta jina la Mushi wakati kumbe unayemtafuta anaitwa Moshi. Hapo ni wazi huwezi kulikuta hilo jina.

Madai ya mheshimiwa Lissu ni mazito mno, I hope ameyafanyia vizuri uchunguzi wake maana ukimtupia lawama nzito hivyo jaji, hapo umeua credibility yake yote na kila maamuzi atakayokuwa anatoa, yatakuwa yanaangaliwa tofauti na watu mbalimbali.
 
Majaji hawajahukumiwa bila kusikilizwa kwa sababu Lisu aliambiwa atoe ushahidi sasa kama unataka kuthibitisha ushahidi ule ni batili au la ndo unatakiwa uwape hao waliotajwa fursa ya kusikilizwa.Hakimu kukosea ni jambo la kawaida sana na mahakama ni independent organ hakuna hakimmu anayepewa adhabu kwa kukosea mahamuzi labda ithibitishwe alifanya makusudi.Kuvaa kofia mahakamani hairuhusiwi kimaadili na yule hakimu alikuwa mgeni kwa hiyo lile lilikuwa ni kosa la kawaida kabisa la kisheria watu kuzungumza haialalishi jambo.Umeshasema hakimu alikosea ndo mana alihamishwa hapohapo unasema kuhamisha hakimu ni utaratibu wa kawaida tukuelewe lipi?Watanzania tunapenda tu kushabikia bila kujua ukweli ni kama hii kesi ya mtoto ya juzi juzi ITV watakuwa wamejifunza no research no rigt to speak.Kudhalilisha mahakama kivipi tena washukuru hao law assisstant
 
Kusema kweli kwa ile taarifa ya Lissu chombo cua mahakama kimeonekana ni cha ajabu ajabu na watu walioisoma wamekosa imani kabisa na chombo hiki ambacho kinatakiwa kiwe ni chombo cha haki kischo na mawaa kama aliyoyaainisha Lissu.

Je kwa watu kukosa imani na chombo hicho kuna uhalali wowote wa chombo hicho kuendelea kuwepo?
 
Mkuu, Lisu kaja ongezea ushahidi wa lile walijualo wananchi. Haiaminiki.majaji, mahakimu, waendesha mashtaka, na makarani wote hawaaminiki ama kwa rushwa au uwezo mdogo. Ukiwa na kesi au ya nduguyo mahakama ya kinondoni, kwa mfano, nenda na pesa ya kutosha. Hakuna sehemu yenye transaction kubwa kama mahakamani.

Mawakili je ( binafsi na wa serikali), wao wanaaminika?
 
Back
Top Bottom