Tundu Lissu yale yale uliyoyasema....

Tundu Lissu yale yale uliyoyasema....

Nimeliona na mimi ( Kididimo) ni mwanasayansi,na ethically ni mtafiti. Nimecomment kuwa 100% ya aliyosema huyu mteuliwa yanafanana na aliyosema TL. Alitakiwa a acknowledge TLs' work! That could be more ethical, cause, it was his original work!
[emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818]
 
Andiko la Dr Adelardus Kilangi,mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Arusha,mwanasheria kitaaluma aliyebobea kwenye sheria za madini,na mwenyekiti wa bodi ya Petrol Tanzania!
............................................
Nimeliweka hapa ili tu-flow vizuri na kujionea jinsi watawala walivyojawa chuki na unafiki juu ya Mh. [HASHTAG]#TunduLissu[/HASHTAG]...............

Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.
MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.
SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.
 
Yale yale uliyoyasema na labda yakapelekea ukapigwa risasi, leo mtu "aliyekopi" yale yale, nasema yale yale utadhani ulimtumia kopi ya andiko lako na kuyaweka JF na kwingine, ameteuliwa kuwa AG.
Ugua pole shujaa wa nchi hii! Utapona, Mungu yuko nawe!

mkuu weka bandiko la lissu hapa na la huyo kilangi, word by word compare and contrast

Kilangi kamuacha Lissu mbali sana sana sana , kuleeeee....kigoma na juu ya kilimanjaro

unapokosoa kitu, rudi kwenye basic, jenga hoja, kubaliana na alichofanya huyo mtu , shauri for improvement na acha mhusika aamue.....kavukavu na ukakasi siyo lugha za kisomi, na ndio unaona Kilangi yuko smart, Lissu mpeni kichwa tu

Lissu anajua kukosoa, hata kama anaongea point ataweka personal attacks, atataka kujikuza, kujifanya mjuaji, atamdhalilihs mhusika ili kuwa kusanya wapuuzi kama wewe!!

that is what he knows, that is how he is

Lissu angekuwa anakosoa kwa staha, ana appreciate wengine na anatoa solution angekuwa one of great and most influential person in this country, sasa yeye kila wakati ni rigid, uanaharakati na ndio inamfanya anakosa kibali cha kulisaidia taifa, attitude is verything mkuu, hata uwe genius vipi, una attitude mbaya you LOST!! its natural

there is no way you can think others are always wrong!!you must have problem

sasa wanapotokea watu kama nyie kumpa kichwa wakati ni looser haisaidii!! endelea kujifariji
 
mkuu weka bandiko la lissu hapa na la huyo kilangi, word by word compare and contrast

Kilangi kamuacha Lissu mbali sana sana sana , kuleeeee....kigoma na juu ya kilimanjaro

unapokosoa kitu, rudi kwenye basic, jenga hoja, kubaliana na alichofanya huyo mtu , shauri for improvement na acha mhusika aamua

Lissu anajua kukosoa, hata kama anaongea point ataweka personal attacks, atataka kujikuza, kujifanya mjuaji, atamdhalilihs mhusika ili kuwa kusanya wapuuzi kama wewe!!

Lissu nadhani hata mkewe akiwa MP huwa anakosoa uumbaji!

that is what he knows, that is how he is

Lissu angekuwa anakosoa kwa staha, ana appreciate wengine na anatoa solution angekuwa one of great and most influential person in this country, sasa yeye kila wakati ni rigid, uanaharakati na ndio inamfanya anakosa kibali cha kulisaidia taifa, attitude is verything mkuu, hata uwe genius vipi, una attitude mbaya you LOST!! its natural

there is no way you can think others are always wrong!!you must have problem

sasa wanapotokea wajinga kama nyie kumpa bichwa wakati ni looser haisaidii!! endelea kujifariji
Semeni chochote lkn Lissu alishauri the way foward kuhusu tatizo litakalotupata tukivunja mikataba kabla ya kujitoa MIGA the same thing kimesemwa na AG mpya Dr. Kilangi.

Ili kuonyesha uungwana at least mjifunze ku appreciate kinachosemwa na watu msiowapenda, halafu uache lugha za kudhalilisha kijinsia nafikiri wewe ni mtu mzima sasa.
Dr Adelardus Kilangi, AG.

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.
 
Nyerere hakuwa Marxist, Lenninst wala Maoist. Kuna tofauti kubwa Kati ya Ukomunist na Ujamaa (socialism). Hao watatu wa mwanzo walikuwa Wakomunist. Nyerere alikuwa soshalisti. Kwa hiyo hasingetetea falsa zake kwa misingi ya Ukomunisti.
Mkuu, soma vizuri. "Communism is an advaced stage of socialism" . Soma maono na mawazo ya wanafalsafa hao,nenda kwenye kitabu cha Mwl . Nyerere "African Socialism" utapata picha.
 
Niliwahi kuandika humu kuwa watawala waache kupaka damu mikono watoto wetu(ndg zetu walioko kitengoni licensed to kill) kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya Taifa, na tishio la Uhuru...TL hakuwa na tishio lolote ktk maslahi ya Taifa wala tishio la kupindua mtawala, Ila alikuwa na tishio la kisera na Hoja dhidi ya chama tawala na siyo kazi ya watu wakitengo kuzima hoja na sera za vyama mbadala bali kazi ya chama tawala...long live TL
 
Hivi alisemaje kuhusu hela za makinikia? Kiko wapi sasa?
 
U
Niliwahi kuandika humu kuwa watawala waache kupaka damu mikono watoto wetu(ndg zetu walioko kitengoni licensed to kill) kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya Taifa, na tishio la Uhuru...TL hakuwa na tishio lolote ktk maslahi ya Taifa wala tishio la kupindua mtawala, Ila alikuwa na tishio la kisera na Hoja dhidi ya chama tawala na siyo kazi ya watu wakitengo kuzima hoja na sera za vyama mbadala bali kazi ya chama tawala...long live TL
Umesema vizuri. Hao wanaong'ang'ana kuimba wimbo wa uzarendo kila siku hao hao ndio sio wazalendo ktk maslah ya Taifa.
 
Tundu Lissu ni malaika, hakustahili "kuhukumiwa kifo" na watu wasiojulikana kwa maagizo kutoka angani. Aliyoyasimamia Tundu bungeni na kwingineko ni yaleyale aliyosema huyu AG mpya, maana ukweli unatabia ya kutobadiliki. Msikilize hapa chini Tundu Lissu:

mkuu weka bandiko la lissu hapa na la huyo kilangi, word by word compare and contrast

Kilangi kamuacha Lissu mbali sana sana sana , kuleeeee....kigoma na juu ya kilimanjaro

unapokosoa kitu, rudi kwenye basic, jenga hoja, kubaliana na alichofanya huyo mtu , shauri for improvement na acha mhusika aamue.....kavukavu na ukakasi siyo lugha za kisomi, na ndio unaona Kilangi yuko smart, Lissu mpeni kichwa tu

Lissu anajua kukosoa, hata kama anaongea point ataweka personal attacks, atataka kujikuza, kujifanya mjuaji, atamdhalilihs mhusika ili kuwa kusanya wapuuzi kama wewe!!

that is what he knows, that is how he is

Lissu angekuwa anakosoa kwa staha, ana appreciate wengine na anatoa solution angekuwa one of great and most influential person in this country, sasa yeye kila wakati ni rigid, uanaharakati na ndio inamfanya anakosa kibali cha kulisaidia taifa, attitude is verything mkuu, hata uwe genius vipi, una attitude mbaya you LOST!! its natural

there is no way you can think others are always wrong!!you must have problem

sasa wanapotokea wajinga kama nyie kumpa bichwa wakati ni looser haisaidii!! endelea kujifariji
Mkuu hayo unayaona kutokana na position uliyoijiweka,ukisha muona mpinzani wako kisiasa ni adui,kila wakati utafikiria negative tu.Mwanzo mie nilidhani Rais alimwelewa TL ila akaendeleza siasa kumbe hatukuelewa kwa kuwa tulijikita kwenye kuangalia presentation styles badala ya content? Mungu saidia Tanzania
 
Tundu Lissu ni malaika, hakustahili "kuhukumiwa kifo" na watu wasiojulikana kwa maagizo kutoka angani. Aliyoyasimamia Tundu bungeni na kwingineko ni yaleyale aliyosema huyu AG mpya, maana ukweli unatabia ya kutobadiliki. Msikilize hapa chini Tundu Lissu:

LONG LIVE PRESIDENT LISSU.......let the most high assassins see Your truth and Your real patriotism with their own eyes
 
njgoja nilisake lipo humu, kina yehodava na ma nzi mengine ya lumumba yakamtukana sana,the thing is kaongea yaleyale ya Lissu kuhusu MIGA na mali kukamatwa,kushtakiwa,yaleyale ya ndugu yetu lissu,dah inaboa sana hiz nchi za ki SHITHOLE zina majitu mapumbavu yenye IQ ndogo sana
Ni kweli YEHODAYA alimtukana matusi yote anayoweza hadi kumwita mke wa Lissu, Leo ndo AG Wa Ikulu anayoitetea hata ikitoa uharo, sijui atakuja na filamu gani kujikosha maana Lumumba kwa kujipendekeza ni first class.
 
Back
Top Bottom