Ndio maana maneno ya Lisu yanaonekana kama ni uchochezi, kama kitabu kinaeleza watu jinsi walivyouwawa na kuzikwa, leo Lisu anaulizaje kuwa 'watu hao wako wapi?'
Kitabu kinaeleza waliuwawa na kuzikwa kwenye KABURI la pamoja, Lisu anasema walizikwa ktk HANDAKI inamaana msomi huyu wa sheria hajui tofauti ya Kaburi na handaki. Hii inaonyesha Siasa mtu ikimshinda anaamua kuharibu LIWALO na LIWE. Nasema kila mara CHADEMA hawana malengo ya dhati kisiasa kwani, haiwezekani chama kinachotaka uwingi wa uungwaji mkono ya kipata uongozi wa nchi ukatengeneza uadui na baadhi ya wananchi waliomuhimu ktk kukupatia uongozi.
Chadema ktk utaratibu huu kinapoteza wingi wa wapenzi kwa kosa kubwa la kuwafitinisha wananchi.