Tundu Lissu: Walipotelea wapi waasisi wa Muungano?

Tundu Lissu: Walipotelea wapi waasisi wa Muungano?


SIO OTHMAN NA HANGA PEKE YAO NA WENGINE PIA
KUULIWA KWA WANANCHI WENGINE
Baada ya kumalizika mavamizi hayo Jamuari, 1964 na yakatendwa yaliotendwa, tangu kwa kuuliwa na
kwa kudhalilishwa kwa kila aina, haikutosha bali daima wananchi wakitishwa na kukamatwa kamatwa
ovyo. Katika mwaka 1964, Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar kama kawaida yake iliwavamia na
kuwakamata baadhi ya wananchi. Wananchi hao wengine walikamatwa kutoka majumbani mwao,
wengine kutoka makazini mwao na wengine mabarabarani. Baada ya kuwakamata kwanza waliwapeleka
kwenye kituo cha Jeshi cha Mtoni na baadae waliwaondoa, wengine walipelekwa kwenye Makao Makuu
ya Magereza, Kiinua Miguu na wengine walipelekwa kwenye kituo cha Kijeshi "Army House",
kilichokuweko huko Migombani.

Miongoni mwa waliokamatwa wakati huo walikuwa Mabwana hawa: (akiwemo bibi mmoja)
Muhammed Salim (Jinja)
Amour Zahor
Said Dahoma (Kombanyongo)
Mohammed Hamoud Barwani
Nasser Mansour
Musa Ahmed (Lashoka)
Sultan Binbrek
Ali Mohammed Barwani
Bibi wa Unguja (Mke wa Bwana AbdulRahman Haider[ Maalesh])

Mohammed Salim Jinja, Amour Zahor, Said Kombanyongo, Mohammed Hamoud na Hamza Mohammed,
wao ndiwo walioondolewa kutoka Makao Makuu ya Magereza na kupelekwa "Army House". Tokea siku
hiyo waliyoondoshwa kutoka Makao Makuu ya Magereza hadi hii leo hawa jaonekana tena. Kutokana na
khabari zenye kuaminika na hao wenziwao waliyokuwa pamoja wakati huo zinasema kuwa wote hao

yaani Mohammmed Salim Jinja, Amour Zahor, Said Kombanyongo, Mohammed Hamoud na Hamza
Mohammed, wameuliwa siku moja katika sehemu ya Kama, Unguja kwa kupigwa risasi.

NAMNA WALIVYO ULIWA
Kabla ya kuuliwa, kwanza walitakiwa wao pamoja na hao wenziwao, wachimbe shimo kubwa liwe ndio
kaburi lao, yaani wajichimbie wenyewe kaburi lao. Baada ya kumaliza kulichimba, aliitwa kwanza,
Sheikh Mohammed Salim Jinja na alitakiwa avuwe nguo zote hata chupi, na alizivua. Baada ya kuzivua,
alipewa kalamu na karatasi aandike wasia ikiwa anapenda. Sheikh Mohammed alikataa kuandika.
Aliambiwa afungue kinywa na baada ya kufungua, alitiwa bastola kinywani na alifyatuliwa risasi humo
humo kinywani. Hapo hapo alikufa na alisukumwa ndani ya hilo shimo. Baada yake, wapili alikuwa
Sheikh Amour Zahor. Yeye vilevile alitakiwa avue nguo zote, alizivua, ila yeye alikataa kuvua chupi.
Yeye aliwekewa bastola juu ya kifua upande wa mkono wa kushoto na ilifyatuliwa risasi. Sheikh Amour
yeye alikaiwia kidogo kufa, na alitumbukizwa shimoni akiwa bado anatweta. Mwengine, aliyefuatia
kuuliwa alikuwa, Sheikh Mohammed Hamoud na baada yake alifuatia, Sheikh Said Dahoma
Kombanyongo na wa mwisho alikuwa Seyyid Hamza Mohammed. Wenziwao waliyokuwa pamoja nao
katika siku hiyo, walikuwa, Mabwana Nasser Mansour, Musa Ahmed (Lashoka), Ali Awadh, Awadh Salim,
Idi Juma, Said Ali Hamoud AlHarthy, AbdulRahman Haider (Maalesh), Sultan Binbrek na Bibi wa Unguja.
Walitakiwa wawafukie wenziwao ndani ya hilo shimo walimotumbukizwa likiwa ndio kaburi lao.

Baada ya kumaliza kuwafukia hao wenziwao, waliambiwa, "Nyie siku yenu kesho. Tutakumalizeni kama
tulivyowamaliza hawa wenzenu. Leo mtarudi gerezani na kesho mtaletwa tena hapa. Tunakwambieni,
hatutaki kusikia mmesema lolote katika haya yaliyopita hapa hii leo. Walirejeshwa gerezani katika hali
mbaya sana kwani walikuwa kama wamerukwa na akili kwa khofu zilizowajaa kwa kushuhudia ukatili
kama huo wakitendewa wenziwao. Mungu ndiye Mungu, wao walijiona ndio wenye uwezo wa kufanya
kila walitakalo. Walisahau kuwa Mwenye Enzi Mungu ndiye mwenye nguvu na ndiye muweza wa kufanya
atakalo. Wananchi hao waliyobakia, hawakupelekwa kwenda kumalizwa kama walivyoambiwa. Wengine
kati yao, baada ya kukaa kwa muda gerezani waliachiliwa huru. Katika wao walioachiliwa walikuwa,
Sheikh Ali Ahmed Riami, Sheikh Ali Mohammad Barwani, Sheikh Sultan Binbrek, Bibi wa Unguja na
baadhi ya wengine waliyo kuwa pamoja nao. Waliyokuwa wamebakishwa gerezani walikuwa ni, Musa
Ahmed (Lashoka), Nasser Mansour, Idi Juma, Ali Awadh, Awadh Salim, AbdulRahman Haider (Maalesh)
na Said Ali Hamoud AlHarthy, wao walifungwa vifungo vya miaka 10 kwa kila mmoja. Wananchi hao,
wadhulumiwa wamekaa katika magereza toka mwaka huo wa 1964 mpaka 1972 walipoachiliwa huru
pamoja na wenziwao wengine.


KUULIWA WANANCHI MSIKITINI

Mnamo taarikhi 9 Septemba, 1964 katika kiasi cha saa tatu za usiku, mmoja katika wakuu wa Serikali ya
Mavamizi ya Zanzibar, Mohammed Abdalla Kaujore, baada ya kupiga bangi zake na kunywa ulevi wake
aliwaingilia wananchi waliyokuwa wakifanya ibada zao ndani ya Msikiti wa Ithinaashiri wa Kiponda na
kuwauwa kwa kuwapiga marisasi bure bilashi. Watu watano waliuwawa siku hiyo. Mmoja kati ya hao
alikuwa mtoto wa miaka minane akiitwa, Abbas Kassim. Wengine walikuwa, Seyyid AbdulMuttalib
Hashim, Seyyid Ali Asghar, Haj AbdulHusain Tejani na Babu Haji.

Edington Kisasi akiwa miongoni wa wakuu wa hiyo Serikali ya Mavamizi na ndiye wakati huo aliyekuwa
mkuu wa Polisi, alitangaza katika Radio ya Zanzibar, "Serikali inasikitishwa sana kwa kitendo kilicho
fanyika katika Msikiti wa Ithinashiri, Kiponda. Na Serikali inafanya uchunguzi juu ya tokeo hilo na mara
tu baada ya kupatikana matokeo ya uchunguzi huo, Serikali itachukuwa khatua za kutosha juu ya
ukhalifu uliyo tendeka". Mpaka naziandika khabari hizi ndani ya hiki kijitabu, imeshapita miaka 30
tokea kutokea tokeo hilo, na hata hilo uwaji lenyewe nalo limesha kufilia mbali, na bado Serikali ya
Mavamizi haijaweza kutoa natija ya hakika juu ya huo uchunguzi waliyokuwa wameusema kuwa
waufanye! Katili hilo liliachiliwa likitembea kwa marefu na mapana kama kwamba halikufanya
lolote,bali lilibaki katika cheo chake vilevile. (Mwizi mgema, askari mgema, na hakimu mgema. Jee
mwenye mnazi atapata haki hapo?)

Bado utamsikia Mwalimu Nyerere na waongozi wake wa Serikali ya Mavamizi ya Zanzibar na hata hao
ndugu zetu wajiitao, "progressives" ati nao husema kuwa, "tumefanya Mapinduzi kwa ajili ya kuleta
usawa na kuondoa dhulma zilizo kuwa zikifanywa na Masultani na Mabwanyenye!" Masultani gani hao na
Mabwanyenye wepi hao waliyo wahi kuingia Misikitini au Makanisani, licha ya kuwauwa au kuwapiga
waumini katika nyumba zao za Ibada, bali hata kuwazuilia kufanya Ibada zao? Hayajawahi kutokea hata
mara moja katika maisha yote.
 
Ushahidi kwenye kitabu!!!!..... Kitabu si yeyote anaweza kuandika??? Tukisema tuamini kila kitabu vipo vitabu vinatetea ndoa za jinsia moja. Mkiletewa Link humu Mtaaamini kwa kuwa imeandikwa kwenye kitabu???
 
Ushahidi kwenye kitabu!!!!..... Kitabu si yeyote anaweza kuandika??? Tukisema tuamini kila kitabu vipo vitabu vinatetea ndoa za jinsia moja. Mkiletewa Link humu Mtaaamini kwa kuwa imeandikwa kwenye kitabu???

Ushahidi upo kila mahali.kitabu ni reference tu.
Ushahidi ni kuoneshwa pale mnazi mmoja akiwa na pingu akahukumiwa kosa lake ni urafiki wake na Kambona.
Kama ulikua bado hujaja Dar au hujazaliwa muilize nyanya wako.
 
Lissu ni miongoni mwa watu mashuhuri kuwahi kutokea katika Taifa hili
 
Back
Top Bottom