Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
Tunataka Tanganyika yetu! Lissu moto juu kanyaga twende
na mimi nataka Tanganyika yetu lakini sio kwa kukimbia vikao vitakavyotuwezesha kupata tanganyika yetu bora kama Lissu
Tunataka Tanganyika yetu! Lissu moto juu kanyaga twende
tundu lissu alikosa maarifa kwa kukimbia vikao hivyo sasa anapiga kelele za nini?
Kama aliona mapema kwa nini hakuyasema hayo mapema na kwa maana hiyo asingeweza hata kuhudhuria vikao vya bunge tangu mwanzo. Alilalamika wapi kwamba kamati wamepanga mambo yaende wanavyotaka wao?Lisu ana haki kuwasilisha mawazo yake. Kwa wale unaoona anapiga kelele mmekosea. alichofanya Celina ni kumattack kujaribu kufunika uozo.. yani unaacha kujadili content unamjadili mtu tena unatafuta sababu dhaifu kabisa. alifanya sahihi kutokwenda. utashirikije wakati unajua watu tayari wamepanga mambo yaende wanavyotaka wao? angekuwa msindikizaji tu!!
hawa jamaa walifanya fujo jana kwenye mdahalo , naona bado wanaendeleza pumba humu
Mkuu hizo siasa za cuf ndio zilivyo. Jana nilikua naangalizia mdaharo huo kwenye kijiwe kimoja mashuhuri yaani, kuna dini fulani inakisakama cdm sana. Na hata ukiangalia kwa umakini wengi wanaopinga cdm huwa na ajenda ya udini. Angalia sana hili au lifanyie kazi.
Lissu kwa hilo umebanwa kama hulitolei maelezo litakumaliza
kama hakuhudhuria vikao ulitaka akae kimya bungeni na kusinzia kama wengine...? tulimchagua ili atusemee.. popote, kama sio kwenye kamati basi bungeni na kama sio bungeni basi mikutanoni...
aluta kuntinua.. acha awaamshe watz, na sasa wameanza kuamka mmojammoja mpaka nchi nzima iamke..!
Low reasoning ability is killing CCM
Lisu ana haki kuwasilisha mawazo yake. Kwa wale unaoona anapiga kelele mmekosea. alichofanya Celina ni kumattack kujaribu kufunika uozo.. yani unaacha kujadili content unamjadili mtu tena unatafuta sababu dhaifu kabisa. alifanya sahihi kutokwenda. utashirikije wakati unajua watu tayari wamepanga mambo yaende wanavyotaka wao? angekuwa msindikizaji tu!!
" Chloroquine ni Chungu lakini ni Dawa"chadema wameshikwa pabaya wabishi hao hata kwenye hoja iliyo wazi ni heri tusio na chama. kama mnabisha kuwa Tundu hakukosea basi hakuna haja ya kushika dola mtakuwa wabishi zaidi na hamtashaurika kama CCM
Kitu ambacho Celina Kombani na mleta mada hii hawajasema ni kama Lissu alikuwa Tarime siku zote ambazo kamati ilikuwa inakutana! Kwa maneno mengine madai ni kwamba Lissu hakuwahi kuhudhhuria vikao vya Kamati kwa sababu alikuwa Tarime!
Sasa turudi nyuma, Lissu alikwenda Tarime wakati wa sakata la mauaji ya Nyamongo na baada ya kufikishwa mahakamani Jaji alimuamuru asikanyage eneo hilo wakati wote wa kisa. Kesi bado haijaisha. Hivyo ili haya madai yawe sahihi inabidi Celina Kombani na mleta mada aseme kuwa vikao vyote vya kamati vilifanyika kabla ya Lissu kupewa amri na mahakama ya kukanyaga Tarime? Au Lissu aliendelea kukaka Tarime licha ya amri ya jaji ya kutafanya hivyo. Je hili ni kweli?
Pili, kwenye mdahalo jana (Star Tv) Lissu alisema kuwa hoja alizotoa bungeni na anazosema kwenye mdahalo ndizo hizo hizo alizotoa kwenye kamati. Je, Celina Kombani anaweza kutuambia Lissu alitoaje mchango wake kwenye kamati? kupitia kwenye simu? au video conference toka Tarime?!
Na mwisho, Lissu alisoka vikao siku ngapi? zote? kama ni siku moja au mbili hiyo inamfanya mtu asijue nini kiliongelewa? kamati haichukui minute? na je kuna wajumbe wengine waliokosa vikao? kwa muda gani? kukosa kwao kumewafanya wasijue nini kinaendelea? Na kama mjumbe hayupo kwenye kikao (physically) ina maana hana ruhusa ya kutoa maoni?
kumlinda lissu kakati hoja hii tunakuwa hatumsaidii kujirekebisha