Tundu Lissu umetuangusha kwa nini hukuhudhuria vikao vya kamati za katiba

Status
Not open for further replies.

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,976
784
Wakati wa kufunga muswada wa katiba, Waziri wa sheria na katiba Celina kombani alituambia watanzania kwamba anamshangaa Tundu Lissu anafunguka leo na kutoka bungeni na wanachadema wenzake wakati hakutokea kwenye vikao vya kamati ambako angeweza kutoa maoni yake. Kombani alisema, kwa mfano katika kikao cha mwezi juni, 2011 Lissu alikuwa Tarime wakati wajumbe wengine wakikutana kuandaa mchakato huo kwa ajili ya kuwakilishwa bungeni lakini pia Waziri alisema anayo orodha ya mahudhurio kuthibitisha kwamba Lissu hakuhudhuria. Katika hitimisho lake hilo Kombani alisema, wajumbe wengine kama Halima Mdee na wabunge wengine wa upinzani walihudhuria na walitoa maoni yao ambayo yamepokelewa na kufanyiwa kazi.

Kumbuka kamati hii iliundwa baada ya kukataliwa kwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza ili kutatibu mchakato huo upya kabla hujasomwa kwa mara ya pili miongoni mwa wajumbe alikuwa Tundu Lissu ambaye taifa limetangaziwa kwamba hakuhudhuria vikao.


my take: 1. Ni kazi gani muhimu zilimbana Lissu kuliko unyeti wa katiba (moyo wa nchi)
2. lissu analetaje maoni yake bungeni wakati maoni hayo angeyatoa kwenye kamati
3. Lissu angehudhuria vikao vya kamati ya katiba angetuambia alitoa maoni gani ambayo hayakupokelewa.
4. Tundu Lissu huwezi kulitumia bunge kama kamati ndogo unawarudisha nyuma wengine.
5. Lissu tuombe radhi watanzania kwa kushindwa kutuwakilisha kwenye kamati
6. Lissu wewe ulikuwa muhimu sana kuanzia ngazi ya kamati ambako hukuhudhuria
7. tundu lissu ulitoa kipambele kwa mamabo mengine kuliko katiba?
 
Unapojiongelea mwenyewe tafadhali tumia 'nafsi yako' siyo nafsi za wengine...Kama amekuangusha ww mimi hajaniangusha, after all wewe ni mwanamagamba!
 
tundu lissu alikosa maarifa kwa kukimbia vikao hivyo sasa anapiga kelele za nini?
 
pipijojo ana hoja lakini wapambe mnapindisha kwa sababu mnazojua, kwa nini Tundu Lissu yuko kimya wakati wengi tulisikia shutuma za waziri dhidi yake
 
Kabla ya kuja kuandika hapa ulipata nafasi ya kujua majibu ya Lissu kabla ya kutaka wewe hayo majibu?Au kwako kauli ya Waziri ndio unaiamini?Nakumbuka kuona picha humu ya moja ya vikao vya kamati na Lissu pekee ndiye aliyekuwa akitumia laptop,hivyo sidhani kama hakuwahi hudhuria.
 
Hata angeingia hakuna ambacho kingebadilika,
acha tuone na dunia ijue kwamba katiba hatujarizika nayo,
na ikiwezekana tuingie barabarani tuseme hayo.
 
wakati wa kufunga muswada wa katiba, waziri wa sheria na katiba celina kombani alituambia watanzania kwamba anamshangaa tundu lissu anafunguka leo na kutoka bungeni na wanachadema wenzake wakati hakutokea kwenye vikao vya kamati ambako angeweza kutoa maoni yake. Kombani alisema, kwa mfano katika kikao cha mwezi juni, 2011 lissu alikuwa tarime wakati wajumbe wengine wakikutana kuandaa mchakato huo kwa ajili ya kuwakilishwa bungeni lakini pia waziri alisema anayo orodha ya mahudhurio kuthibitisha kwamba lissu hakuhudhuria. Katika hitimisho lake hilo kombani alisema, wajumbe wengine kama halima mdee na wabunge wengine wa upinzani walihudhuria na walitoa maoni yao ambayo yamepokelewa na kufanyiwa kazi.

Kumbuka kamati hii iliundwa baada ya kukataliwa kwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza ili kutatibu mchakato huo upya kabla hujasomwa kwa mara ya pili miongoni mwa wajumbe alikuwa tundu lissu ambaye taifa limetangaziwa kwamba hakuhudhuria vikao.


My take: 1. Ni kazi gani muhimu zilimbana lissu kuliko unyeti wa katiba (moyo wa nchi)
2. Lissu analetaje maoni yake bungeni wakati maoni hayo angeyatoa kwenye kamati
3. Lissu angehudhuria vikao vya kamati ya katiba angetuambia alitoa maoni gani ambayo hayakupokelewa.
4. Tundu lissu huwezi kulitumia bunge kama kamati ndogo unawarudisha nyuma wengine.
5. Lissu tuombe radhi watanzania kwa kushindwa kutuwakilisha kwenye kamati
6. Lissu wewe ulikuwa muhimu sana kuanzia ngazi ya kamati ambako hukuhudhuria
7. Tundu lissu ulitoa kipambele kwa mamabo mengine kuliko katiba?

akili zako kama jina lako
 
Huu ni upotoshwaji mwingine toka kwa CCM na hasa Celina Komabani. Kama Lissu alikuwa haudhurii vikao vya kamati alijuaje kuwa Spika anaingilia shuguli za kamati?
 
Kabla ya kuja kuandika hapa ulipata nafasi ya kujua majibu ya Lissu kabla ya kutaka wewe hayo majibu?Au kwako kauli ya Waziri ndio unaiamini?Nakumbuka kuona picha humu ya moja ya vikao vya kamati na Lissu pekee ndiye aliyekuwa akitumia laptop,hivyo sidhani kama hakuwahi hudhuria.


umeambiwa Lissu ametuhumiwa bungeni ulitaka nani amuulize tena wakati yeye kakaa kimya
 
Mnaongea ongea tu hamjui what real happened, Hebu mtafuteni Lissu ana majibu ya Uhakika!
 
sikupata kusikia hili lakini kama ndivyo Tundu ana kila sababu ya kujibu itamuongezea haiba ya kukubalika
 
tumeona sasa CCM wanajenga hoja kwamba alikimbia vikao vya kamati sasa ndio anaona ana maoni ya kubishana kipi kiwemo na kipi kisiwemo ni kama kweli Tundu hakuwajibika
 
wewe na huyo pipijojo mna matatizo sana.....na huo u -ccm wenu utawatafuna sana


chadema wameshikwa pabaya wabishi hao hata kwenye hoja iliyo wazi ni heri tusio na chama. kama mnabisha kuwa Tundu hakukosea basi hakuna haja ya kushika dola mtakuwa wabishi zaidi na hamtashaurika kama CCM
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom