Tundu Lissu umetuangusha kwa nini hukuhudhuria vikao vya kamati za katiba

Status
Not open for further replies.
" Chloroquine ni Chungu lakini ni Dawa"

Kwa hiyo kama ni wabishi hatuhitaji mabadiliko"Kwa hiyo unaridhika na hali tete ya nchi ilivyo chini ya Uongozi wa CCM? Kwa hiyo kama Tindu hakuwepo kwenye kikao mabadiliko muhimu ya Katiba hayawezi mpaka awepo yeye?Naona unaongea kama vile umetoka kuanguka kwenye mti.

Tundu Lissu alimdaka akiwa anaanguka kwenye mti hakufika chini ndio maana anaweza kujenga hoja za nguvu mimi naona yuko salama ila wewe ni kama umeibukia kusikojulikana
 
Kitu ambacho Celina Kombani na mleta mada hii hawajasema ni kama Lissu alikuwa Tarime siku zote ambazo kamati ilikuwa inakutana! Kwa maneno mengine madai ni kwamba Lissu hakuwahi kuhudhhuria vikao vya Kamati kwa sababu alikuwa Tarime!

Sasa turudi nyuma, Lissu alikwenda Tarime wakati wa sakata la mauaji ya Nyamongo na baada ya kufikishwa mahakamani Jaji alimuamuru asikanyage eneo hilo wakati wote wa kisa. Kesi bado haijaisha. Hivyo ili haya madai yawe sahihi inabidi Celina Kombani na mleta mada aseme kuwa vikao vyote vya kamati vilifanyika kabla ya Lissu kupewa amri na mahakama ya kukanyaga Tarime? Au Lissu aliendelea kukaka Tarime licha ya amri ya jaji ya kutafanya hivyo. Je hili ni kweli?

Pili, kwenye mdahalo jana (Star Tv) Lissu alisema kuwa hoja alizotoa bungeni na anazosema kwenye mdahalo ndizo hizo hizo alizotoa kwenye kamati. Je, Celina Kombani anaweza kutuambia Lissu alitoaje mchango wake kwenye kamati? kupitia kwenye simu? au video conference toka Tarime?!

Na mwisho, Lissu alisoka vikao siku ngapi? zote? kama ni siku moja au mbili hiyo inamfanya mtu asijue nini kiliongelewa? kamati haichukui minute? na je kuna wajumbe wengine waliokosa vikao? kwa muda gani? kukosa kwao kumewafanya wasijue nini kinaendelea? Na kama mjumbe hayupo kwenye kikao (physically) ina maana hana ruhusa ya kutoa maoni?

FJM,

Siku zote kinachoandikwa Bungeni basi kinakuwa sahihi. Na kama kuna mush'kira wowote basi Tundu Lissu ana nafasi ya kukanusha na hata kumwambia Spika kuwa waziri amemsingizia na kulidanganya Bunge. Na hatua zitachukuliwa.

Lakini pia Tundu Lissu sio pekee yupo katika kamati ya sheria pasi na shaka wapo wengine kama akina Halima Mdee na wengine. je hao wengine hawakuwakilisha mawazo ya Chadema katika kamati kuhusu muswada huo. Au Tundu Lissu ndio kila kitu ndani ya Chadema?

 
" Chloroquine ni Chungu lakini ni Dawa"

Kwa hiyo kama ni wabishi hatuhitaji mabadiliko"Kwa hiyo unaridhika na hali tete ya nchi ilivyo chini ya Uongozi wa CCM? Kwa hiyo kama Tindu hakuwepo kwenye kikao mabadiliko muhimu ya Katiba hayawezi mpaka awepo yeye?Naona unaongea kama vile umetoka kuanguka kwenye mti.

kumsema tundu ni dawa chungu inabidi kumesa inaweza kuwa inawaponya
 
tundu Lissu kilichosemwa na Kombani kuhusu wewe bungeni kimeingia kwenye hansard za bunge baadhi ya wafuasi wako wanaona hili ni jambo dogo. nakusihi kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili
 
Tundu Lissu anaendeshwa na siasa za kali. Nadhani itafika hata Chadema watamchoka. Ninachofahamu siasa ni vikao. Lakini lazima ifikie wakati mkubaliane. Haiwezekani yeye ni kubisha tuuuuuu.
 
chadema wameshikwa pabaya wabishi hao hata kwenye hoja iliyo wazi ni heri tusio na chama. kama mnabisha kuwa Tundu hakukosea basi hakuna haja ya kushika dola mtakuwa wabishi zaidi na hamtashaurika kama CCM
Wewe ni kipepeo kama jina lako, hutulii sehemu moja eti huna chama kwa hiyo unabishana nini?????????? Lisu hazungumzii CHADEMA anatetea maslahi ya nchi ya Tanzania, chama kipo na kesho kinaweza kisiwepo, serikali ni miaka mitano kama katiba inavyo sema, lakini katiba ni kitu cha kudumu!!!!!!!!! Tumia akili wacha ushabiki, huna chama lakini unaishi Tanzania gharama za maisha tulizoingizwa na mafisadi wanaolindwa na katiba feki na wewe zinakuhusu na watoto wako!!!!!!!!!! Tunahitaji katiba itakayo dhibiti wezi wa nchi hii, CCM hawawezi kujikaanga na mafuta yao wenyewe, umeelewa?????????? ISIWE NAONGEA NA MTU KUMBE KATUMWA KAZI HAPA!!!!!!!
 
Kama nilimsikia Lisu vizuri, alisema muswada ulipelekwa kwenye kamati 24 october ili kamati iujadili, lakini kamati (yeye akiwemo) ilikataa kwa maana ulitakiwa upelekwe kwa wananchi kwanza watoe maoni. Kwa maana hiyo kamati nzima ilikataa. Sababu za kukataa ni kuwa kamati iliona ni muswada mpya ambao ulitakiwa kusomwa mara ya kwanza na si mara ya pili. (Yaani kama unatakiwa kusomwa mara ya pili ndipo haurudishwi kwa wananchi). Utaratibu huo hata Mnyaa alikubalia kuwa ndio sahaihi. Baada ya kamati kukataa na kumjulisha spika, spika alichukua jukumu la kuchakachua na kulazimisha usomwe eti mara ya pili na hivyo kuiskip kamati ya bunge.
Chadema kwa kuona wananchi hawajatendewa haki ndipo waliona watoke nje ili wasiwe sehemu ya upitishwaji wa muswada ambao haukufuata taratibu.
Kama ni kulaumu, then ilaumiwe kamati nzima ya bunge.
Tutoke huko tuje kwenye muswada wenyewe : Je mnaona mamlaka aliyopewa raisi kuwa ni sawa katika nchi inayotegemewa kujenga demokrasia?
Kifungu cha 5: Raisi ataanzisha hiyo tume
Kifungu cha 6(1): Raisi atawateua wajumbe wa hiyo tume
Pamoja na vigezo vya kuteua wajumbe watume kuwekwa, bado kifungu 6(3)(e) kinamruhusu huyo raisi kuweka vigezo atakavyoona inafaa! Ukisoma vyema kifungu hiki cha 6 ni wazi tume itakuwa ni ya rais; ni vyema ingeitwa the presidential commission of...
Kifungu cha 8 raisi ndiye ataiambia hiyo tume nini cha kufanya (hadidu za rejea). Hakuna wa kuhoji!
Kifungu cha 13 kinaanzisha secretariat ya tume, katika kifungu cha 13(2) raisi anamteua katibu.
Madaraka ya hatari ni kifungu cha 20:
20(1) raisi atateua bunge la katiba (constituent assembly), wajumbe wa bunge hili tunaowajua ni mawaziri wa masuala ya sheria na katiba wa Tanzania (mteule wa raisi) na yule wa Zanzibar na mwanasheria wa serikali ya Tanzania (mteule wa raisi) na yule wa Zanzibar-20(2). Wajumbe wengine wote watateuliwa na raisi kwa kujibu wa 20(3) -Hakuna wa kuhoji uteuzi wa mtu yeyote!
Kifungu cha 27: kura ya maoni itaendeshwa na tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti wake huteuliwa na raisi!

Hivi kweli watanzani wenzangu hapo mnatarajia mpate katiba ya wananchi au katiba ya raisi?

Tafakari and think greatly
 
FJM,

Siku zote kinachoandikwa Bungeni basi kinakuwa sahihi. Na kama kuna mush'kira wowote basi Tundu Lissu ana nafasi ya kukanusha na hata kumwambia Spika kuwa waziri amemsingizia na kulidanganya Bunge. Na hatua zitachukuliwa.

Lakini pia Tundu Lissu sio pekee yupo katika kamati ya sheria pasi na shaka wapo wengine kama akina Halima Mdee na wengine. je hao wengine hawakuwakilisha mawazo ya Chadema katika kamati kuhusu muswada huo. Au Tundu Lissu ndio kila kitu ndani ya Chadema?

Una majibu ya Lema aliposema waziri mkuu kadanganya Bunge?
 
magwanda ya mgambo kweli vichwa maji hayaelewi kabisa wala kuona,sijui nani kayaroga kama waleeee wa kipindi kile cha mtume paulo...........wagalatia
 
Una majibu ya Lema aliposema waziri mkuu kadanganya Bunge?


Hata akiwa sawa na majibu ya lema kuwa bado kutolewa lakini Massage SENT. na inakuwa imenukuliwa katika ansard za Bunge. hata vizazi vijavyo wataweza kujua.
 
FJM,

Siku zote kinachoandikwa Bungeni basi kinakuwa sahihi. Na kama kuna mush'kira wowote basi Tundu Lissu ana nafasi ya kukanusha na hata kumwambia Spika kuwa waziri amemsingizia na kulidanganya Bunge. Na hatua zitachukuliwa.

Lakini pia Tundu Lissu sio pekee yupo katika kamati ya sheria pasi na shaka wapo wengine kama akina Halima Mdee na wengine. je hao wengine hawakuwakilisha mawazo ya Chadema katika kamati kuhusu muswada huo. Au Tundu Lissu ndio kila kitu ndani ya Chadema?


Kwa bahati nzuri tunaishi zama za science na technology, zama ambazo mtu unaweza kupata habari kwa haraka bila kupitia kwa mtu mwingine yoyote kama vile kuangalia vipindi vya bunge live. Sasa unless neno sahihi limepata tafsiri mpya siku hizi mbili, bunge letu na hasa hili la Makinda limejaa uwongo na kadhia ya kutisha. Mawaziri wanasema uwongo kuanzia waziri mkuu huku Spika akishindwa (amekusudia?) kuweka mambo sawa. Unakumbuke issue ya Lema? Unakumbuka ushahidi wa Zito kuhusu CHC? Usahihi uko wapi hapa?
 
hujamwelewa mtoa hoja sio kwamba anataka wewe umjibiye anataka Lissu atoe majibu ya shutuma dhidi yake kwani Kombani alisema alikuwa hahudhurii vikao vya kama na mtuma post kasema juni alikuwa tarime. Lissu aseme alihudhuria vikao vingapi na hakuhudhuria vikao vingapi na kwa nini ili na sisi tupime kama kuna uzito au alikosa kuwajibika. Unaona sasa mitaa wanasema Lissu alipewa milioni 4 ili afanye usanii wa kuwashawisha wenzake watoke bungeni kusudi CCM wabaki peke yao kuunda katiba?


Kwa uelewa wangu maana ya kuweka hoja hapa jamvini ni ili wadau wachangie.
 
Umewahi kufikiri waziri anawahutubia watanzania kuhusu Tundu Lissu kukosa kuhudhuria kikao kimoja tena hakuwa beach na familia yake. Alikuwa anahangaika na watu waliopigwa risasi wakauawa Tarime na alikuwa huko kwa maagizo ya bosi wake Mbowe ili awasaidie wanatarime kisheria.
 
uzuri wa chadema huwa hawakosei wala hawataki kurekebishwa
Jirekebishe kwanza wewe halafu ndio uanze kurekebisha wengine. Nyie CUF si mmekubali kuolewa na CCM sasa mnawezaje kurekebisha wengine wakati mmenogewa na mahaba:A S-heart-2:
 
huyu mama asitake kujiosha kwa kupitia migongo ya wengine. Eti maoni yake yangesikilizwa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom