Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Tundu Antipas Mungwali Lissu, (Mb-Chadema) na msemaji wa kambi ya upinzani katika wizara ya katiba na sheria, jana akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani ya wizara ya hiyo alisema kati ya mengi mambo ya upotofu, upotoshaji hivyo itahalis tukisema Tundu Lissu amepotoka.
Katika hotuba hiyo , wakati akitoa maelezo kuhusu mswada wa kuandaa utaratibu wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya ya JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Mhe. Lissu alisema muswada huo bado una dosari hivyo kambi ya upinzani haikubaliani nao.
Kati ya dosari nyingi alizozitaja miongoni mwao ni uwepo au ushiriki wa Zanzibar kama mshiriki kamili wa mustakbai wa mabadiliko ya katiba hiyo. Mhe. Lissu alipotoka na kujipotosha aliposema:
a). kuwa mamlaka sawa aliyopewa rais wa Zanzibar na rais wa muungano hayakubaliki kwa kuwa yamefanywa "...kuwaonea huruma Wazanzibari baada ya kulalamika, kwa vile ilitosha rais wa zanzibar "...kuhusishwa tu.." na siyo kuwa na mamlaka sawa na rais wa muungano.
b). Wazanzibari wasishirika katika mchakato wa marekebishoa ya katiba katika mambo ya Tanzania bara kama vile Tanzania bara ilivyokuwa haikushirika katika mabadiliko ya katiba yao (mabadiliko ya kumi ya ktiba ya zanzibar ya 1984).
c). Katika uamuzi wa kupitisha katiba kilelezo "utaweka rehani " mustakbali wa mabadiliko hayo kwa vile iwapo Wazanzibari wakikataa na wabara wakikubali katiba hiyo haitapita, hivyo mchakato huu usiwekwe reheni na "siasa za Zanzibar".
MAWAZO YANGU:
Naamini Mhe. Tundu Lissu amefanya upotofu wa makusudi na anayefanya upotofu wa makusudi hawa amepotoka yy mwenyewe kwa vile:
a. Mhe. Lissu anajuwa kuwa muungano huu umeundwa kwa mkataba na siyo katiba na mkataba huo ndiyo unaotoa usawa wa mamlaka za nchi mbili kati ya Jamhuri ya watu wa zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika, katika yale mambo tuliyokualiana likiwamo la katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b. Ushiriki wa Zanzibar katika mabadiliko ya katiba ya muungano siyo wa "hisani" bali haki yao na usawa walionao kwa mujibu wa makubaliano ya muungano na katiba hii hii mbovu, Mhe Lissu, kusema kuwa Zanzibar isihusike na mambo yasiyo kuwa ya muungano katika katiba hii ni kauli yakichekesho na aibu (nachelea kusema ya kipumbavu) kutoka kwa kinywa cha mwanasheria msomi aliyebobea. Mhe. Lissu anajuwa kuwa kinachofanyiwa marekebisho/mabadiliko hapa ni KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SIYO YA TANGANYIKA?
Hapa alikuwa Mhe, Lissu, aje na hoja nyingine ya IPO WAPI KATIBA YA TANGANYIKA WAKATI ZANZIBAR WANAYO KATIBA YAO? ambayo itakuwa na mambo ya Tanganyika kama vile Zanzibar na Wazanzibari haitawahusu.
Ndiyo hapa wazanzibar wanapata na watapata uhalali wa kuikubali au kuikataa katiba ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ambayo hatutakubali tena iingizwe mambo yasiyokuwa ya muungano, hivyo wala hatutakuwa na sababu ya kuyagusa.
c. Mhe. Lissu, anasema mambo kwa ujumla jumla, nani ataweka rehani hapa upitishwaji wa katiba hii? ni Wazanzibari au walioweka utaratibu huo kuwa katiba hiyo haitatumika mpaka ipate ridhaa ya pande mbili za muungano na kila upande kivyake! kwa akili ya Tundu Lissu watakao kataa ni wazanzibari tu,wakikataa Watanganyika je? si na wao watakuwa wameweka rehani mustakabali wa mabadiko haya kwa "siasa za Tanganyika?"
Hata hivyo, bado nakubaliana na maelezo mengine ya Mhe. Tundu Lissu kuwa mchakato huu uwape fursa watanzania waamuwe kama wanautaka muungano na wa aina gani?