Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Tundu lissu anashindwa kuelewa kuwa kudeclare kiasi cha madini tofauti na kilichopo katika makontena ni kuvunja mkataba!?...hivyo automatically Acasia wamekuwa wakivunja hiyo mikataba ambayo tobo lisu anadhani itatushinda.
issue ni....je, ni chombo gani independent kimeleta hizo findings? in the context of international commercial contracts, ile kamati ya Rais haina credibility yoyote kwani iliteuliwa kwa 100% na serekali ambao ni upande mmoja tu wa mkataba (aka mlalamikaji).

kwa taarifa yako, zile findings za ile kamati ziko technically skewed (wale wataalamu wa statistical computations mtanielewa).
 
Hawa wakubwa ni wezi siku zote wawe wa nje au wa ndani, na wamejiwekea mpango madhubuti wa kujilinda na kulinda wizi wao. Mfano mubashara wa ndani ni Chenge and his group, hawakamatiki hawashitakiki.
Ipo siku
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.




Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu



Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu



Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu
Nisingependa tuingize siasa hapa! huyu TL ana historia ya sheria hizi muda mrefu!! tuondoe siasa hapa!! Atumike haraka sana kutunasua!! Hapa ni utaifa tu!! Siasa na uvyama off!!
 
issue ni....je, ni chombo gani independent kimeleta hizo findings? in the context of international commercial contracts, ile kamati ya Rais haina credibility yoyote kwani iliteuliwa kwa 100% na serekali ambao ni upande mmoja tu wa mkataba (aka mlalamikaji).

kwa taarifa yako, zile findings za ile kamati ziko technically skewed (wale wataalamu statistical computations mtanielewa).

Yaan umeniwahi kidogo tu,

Je kama ile kamati imefanya kazi kwa kumfurahisha boss wao tutajuaje?
 
Huo ushauri siyo sawa kabisa.

Serikali na hao wawekezaji kwa pamoja wanatakiwa watafute wataalam wa kimataifa ambao watafanya uchunguzi wao ili kubaini yupi yupo sahihi, Kamati ya Magufuli au ACACIA
 
Kwa hiyo mikataba inasema wawe wana danganya kiasi cha madini kilichomo kwenye makanika? Lissu ni chizi kabisa
Acha ujinga wa kulaumiwa si Lisu bali aliyewapa hiyo mikataba ya kubeba michanga, kilio cha Lisu ni kutaka mikataba ipitiwe kwanza ivunjwe ndipo mngekuja na hizo sinema zenu ambazo ni Dili la mkapa kwani anaamini kesi ikienda mahakamani wawekezaji watashinda na kulipwa yy na kikwete watapata ganji lao kubwa.
 
Kwakuwa wametuibia basi tuna haki ya kuvunja hiyo mikataba lasivyo watulipe hicho walichotuibia kwanza, vinginevyo tutajifidia kwa kuchukua Mali zao
 
Tundu lisu ni tobo haelewi lolote. Akina prof kabudi wameshaliona na kumshauri vyema jpm. Halafu anapaswa kujua kuwa kudeclare kiasi tofauti kilichomo ndani ya mchanga ni kuvunja mkataba automatically. Mi niliwaambia tundu lisu ni mweupe Wa Sheri anashindaga vi case vya kitoto sana.
Hata hili anatetea wezi mana ingekuwa yeye angeshindwa mchana kweupe mana anaona maluweluwe. Kilaza.
Lakini huwezi kusimamia huko kwa kuwa lab analysis umefanya mwenyewe tena kwenye lab ambayo haina ISO accreditation. Matokeo yako yatapingwa tu mahakamani, maana ulichukua sampuli mwenyewe kwa utaratibu wako ukafanya analysis mwenyewe kwenye MAABARA ya GST ambayo haina hata ISO, utawashindaje mahakamani huko nje? Ni vyema tupokee mawazo yote kwa sasa kama kweli tunalitakia mema Taifa letu.
 
Back
Top Bottom