Tundu Lissu: Tutanyolewa bila maji suala la mchanga wa madini, tusikurupuke

Hakuna kitu kama hicho bado mashauriano yanaendelea walichokubali kulipa ni hiyo bil700 huku mashauriano zaidi yakiendelea
Endelea kuota tu , bilioni 700 unaijua au unaropoka tu , you won't be paid a penny of it .Wazungu si mazuzu nyau nyie
 
Tundu, Tundu, Tundu...... Nimekuita mara tatu. Kesi inaendeleaje tuliyoshtakiwa?

..tumedai usd 191 billion halafu Magufuli amekubali "ahadi" ya malipo ya usd 300 million.

..ni sawasawa na udai sh 636 halafu mdaiwa wako akwambie atakulipa sh 1.

..acacia/barrick hawakuwa na haja ya kuendelea na kesi. sisi wenyewe tumesalimu amri.

..John, John, John,...nimekuita mara tatu. Mbona umetusaliti?
 
..madai usd 191 billion.

..malipo usd 300 million.

..ni sawa na udai sh 630, halafu ulipwe sh 1.

..hiyo ndiyo maana halisi ya kunyolewa kwa chupa.
 
Lisu hafai kuwa Rais kabisa, kuna maamuzi mtu unapaswa kuwa jasiri namna hii ujasiri ambao hana.
 
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu

"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu

Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini

Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.

"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu

Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati

Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...

"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu


Bwabwa la Robert Amsterdam. Puuu, mbona twapokea angalau 100Bil
 
jamaa anaogopa wazungu balaa
Hakuna nchi ya kiafrika hata moja isiyomuogopa mzungu ila kiburi tuu kinawaaminisha kuwa hamuwaogopi,tunawategemea wazungu kwa kila kitu tunaanzaje kuacha kuwaogopa,hata huku kuandika na kusoma bila wao tusingejuwa
 
Back
Top Bottom