Tundu Lissu rudi Shule

 
Aisee wewe ni msomi wa sheria mzuri hata kwa maandishi tu inatosha Ku justify,Tindu Lissu ametumwa aje aiue chadema narudia tena pili ni mgonjwa upstairs
 
Hiyo ndiyo katiba ya CHADEMA na ndiyo imeshasajiliwa kwa msajili wa vyama vya siasa nchini...una lingine?
Kama huna lingine vizuri, haya nenda kasome katiba/sheria ya FIFA

Katiba ya CDM Leo hii ya kuifananisha na FIFA?
 
lissu mroho wa madaraka anaka yeye awe naibu katibu mkuu
 
Umaarufu wa zitto mwanzo ulitokana na kupinga ufisadi na umaarufu wake umeshuka kwa yeye kujifungamanisha na ufisadi.
 
Mpe moyo ila kumbuka katiba hiyo naye alishiriki kuitunga so kama sheria ujuavyo ni msumeno na safari hii imekula kwake
 
Kwan hii katiba ya CCM 1977 sio nayo inayozuia watu kupinga matokeo ya uraisi mahakamani? Sio hii inayomuweka Rais juu ya wote kuwa hawezi shitakiwa?

Enyi misukule je hilo la katiba ya CCM si kubwa zaidi ya ilo la katoba ya CDM?
 
Mimi hata sijaelewa unachokitetea. Cdm walishamalizsns na Zitto, akate rufaa asikate awe mbunge asiwe mbunge haifanyi tofauti. Elewa jambo dogo tu Chadema wanasema zzk sio mwanachama wao.
 
Katiba ya CDM haikatazi mwanachama kukishitaki mahakamani chama chake pale anapoona hakitendi haki au kimemkosea. Ukweli ni kuwa endapo mlalamikaji dhidi ya chama akishindwa shauri alilofungua, basi anapoteza uwanachama au kwa lugha nyingine akishinda kesi anaendelea na uwanachama wake kama kawaida. Mleta uzi unaelekea kuwa unampenda sana ZZK, tatizo la kupenda sana HUPOFUSHA. Haya uliyoandika yenye mtizamo wa upande mmoja ni matunda ya kupenda sana, angalia kote kote na uilinde taaluma yako kama kweli wewe ni Mwanasheria uongoze kundi la kurudi shule na nyuma yako awepo Msajili wa vyama vya siasa na vijana wake ndipo waje akina TL nyuma yenu.
 
Zito kama ni msafi, kwanini asiende ccm?

mwambie mzinzi slaa aludishe kadi ya ccm.zito siyo malaya wa siasa kama lema na msigwa mabele na slaa.hajawai miliki kadi ya chama kungine cha siasa zaidi ya cdm.
 
Hakuna mwanasheria mahiri kama Tundu Lisu,wewe sheria zako za kusomea chuo cha kata usizilite hapa utapata aibu.
 
sijawahi kuona chadema wakikurupuka ninauhakika wapo sahihi!!:embarassed2:
 
Duhh, Hivi ni kweli hapa Jamii Forums ni Home of Great Thinkers? Ingawa sijafanya utafiti, nashawishika kuhisi ni only 10-20% ndio wanaoweza kuwa great thinkers, Walio wengi uwezo wao unanipa mashaka makubwa... Ni uwanja wa matusi, Eneo la kampeni na sehemu ambayo watu wanarespond dhidi ya mtu/mchangiaji na siyo hoja... Kuna wakati mtu akishatupia hoja yake, analazimika kujitetea kabisa, eti 'naomba jamani watu tuchangie hiyo hoja, msinishambulie tafadhali', I see... Tubadilike Watanzania..
Kungekuwa na vigezo vya kujiunga na JF siyo kila mtu, Wengine wengi wangebaki kuwa Wasomaji tu, si kuchangia..
Hilo ni pendekezo langu kama kweli tuna malengo ya mabadiliko.. Kuna tofauti kubwa sana kati ya jamii forums na twitter..
Issue kubwa, Watu tunataka kujua nani hasa kapost pia, ID ziwe za ukweli, Sasa watu wanajiita Er.th.oc.te, Qu.n.ne, Tuj.te.em.e n.k. unaficha nini???
 
#team zzk mnasumbuka bure tuu..jamaa leo anaenda zake ATC alikowatanguliza kina mkumbo....
 
Wewe nadhani ni mwanasheria duni kupindukia.

Hivi hujawahi kuona hata baadhi ya mikataba ambayo huwa inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na kutokuelewana kati ya waliofunga mkataba, kwanza watakutana ndani ya vyombo vyao, na hivyo vyombo vyote vikishindwa ndipo watakwenda court of Law. Wewe ni mwanasheria gani usiyelijua hata hili?

Nilivyoelewa ni kuwa katiba ya CHADEMA imeeleza migogoro itatatuliwa vipi, rufaa itakatwa vipi ndani ya vyombo vya chama. Sasa endapo vyombo vyote vya chama, vya mwanzo na rufaa, vimetoa maamuzi yake na bado huridhiki, huzuiliwi kwenda mahakamani lakini kama mahakama itatoa ruling against you, utafukuzwa uanachama. Mimi nadhani huu uamuzi ni sahihi kabisa kwa chama cha siasa ili kuzuia watu wanaolala na kuamka kwenda mahakamani kuzuia maamuzi ya vikao halali vya chama kutendeka.

Lakini pia kuna taasisi ambazo zina miongozo inayotamka wazi kuwa kama hukukubaliana na uamuzi wa ngazi fulani, unaenda ngazi ipi mpaka ya mwisho, na kwa namna gani, na uamuzi wa ngazi ya mwisho hauhojiwi mahakamani. Na miongozo kama hiyo huwa ipo katika mambo ambayo maumuzi yanayotolewa huwa hayakiuki sheria za nchi na wala hakuna hitaji la kisheria la moja kwa moja. Sasa Zito kwa ujinga wake, alienda mahakamani kuzuia taratibu cha ndani ya chama zisifanyike yaani chama kisifuate katiba. Hutaki chama kifuate katiba wakati sheria ya vyama vya siasa inatamka ni lazima vyama vya siasa viendeshe mambo yake kwa kufuata katiba, wewe unayepinga vyama visifuate katiba, una akili?

Wewe naona ni mwanasheria wa sampuli za akina Ngeleja. Pole sana.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…