Tundu Lissu: Rais Magufuli hana tofauti na Kikwete, Mkapa kwenye usiri kuhusu madini

Ripoti ya makinikia ilianika jinsi TZ ilivyoibiwa na kuibiwa madini ya dhahabu. Rais aliunda ile tume ili kuchukua hatua nchi isiibiwe tena. Sasa mtu anakuja kuiita ile ripoti kuwa ni professorial rubbish hawezi kuwa na nia nzuri na nchi hii. Hawezi kuwa hazina kwa taifa letu. Inawezekana akawa msomi au mwelewa sana lakini kutoa comments kuwahalalisha wezi na kuwatukana wanaotaka kujikwamua wasiibiwe tena ni dalili kuwa wezi wameshafikia bei na wewe uko nao. Hazina gani??? Tena huyo anayetoa comments za kuwaunga mkono wezi ni yule ambaye hapo awali aliujulisha umma wa TZ jinsi hao hao wezi walivyoiibia TZ leo ghafla unakuja kuwaunga mkono na kuwakebehi wanaotaka kujikwamua na huo wizi. Eti hazina.

Uelewa wako unatia shaka, uwezo wako wa kupambanua mambo umefikia kikomo, kama Taifa bado tuna safari ndefu sana ya kuwakomboa watu wa aina yako mpo wengi ndio maana hatupigi hatua za kimaendeleo ikiwemo kujenga viwanda anavyovihubiri jiwe.

Tundu Lisu ni mzalendo wa kweli katika Taifa letu, hilo lipo wazi kupitia jitihada zake za kila leo kutetea watanzania na rasilimali za Taifa hili. Waweza kataa tu kwa kuwa ni hulka na jadi yenu mmejaa chuki na ubinafsi, wote mnao support kila upuuzi toka kwa jiwe.

Lisu anatamani kuona hatua sahihi na stahiki zinachukuliwa dhidi ya wale wote wanao hujumu kwa namna yoyote ile rasilimali za Taifa; na si hatua holela zinazozo weza kuwa na madhara na kulitia hasara nchi kama ilivyo tokea huko siku za nyuma.

Maamuzi holela na ya kukurupuka imeligarimu taifa letu kwa mda mrefu, hivyo Lisu na watanzania wenye mapenzi mema na nchi hii hatutamani kuona maamuzi ya kipuuzi yanaendelea kuligarimu Taifa.
 
Pole sana. Uwezo wako wa kuelewa hauwezi kutofautisha mtu alivyokuwa jana na alivyo leo baada ya kuwa compromized. Tundu ndiye aliyewafumbua macho waTanzania wengi jinsi walivyokuwa wakiibiwa na kina ACACIA n.k. Baada ya serikali hii ya sasa kuanza mapambano na ACACIA yeye huyo huyo Lissu akasema yumeingia nao mkataba eti tutanyolewa kwa chupa bila maji. Hivyo eti tuwaache waendelea kutuibia. Hii ni nini kama sio kuwa compromized??? Alipoona serikali haimsikilizi akaanza kuponda hatua zote zilizochukuliwa na kudai kufuatilia makenikia nikuacha dhahabu ambayo ilikuwa inatoroshwa. Yaani anakosoa kwa nini serikali ifuatilie makinikia badala ya dhahabu wakati yeye alituambia waTanzania tunaibiwa kwenye makenikia. Hivi nakupa news au nawe unatafahamu haya? Je huyu Lissu ni yuleyule? Sasa baada ya serikali kutoyumbishwa akaamua kuwa wakili wake yeye na Fatuma Karume. Ni kweli ACACIA hawajafungua kesi mahakamani japo Lissu na Fatuma wanawashinikiza wafungue kesi eti makinikia yao yamezuiwa bandarini. Kwamba uchunguzi uligundua kuwa ACACIA wali-under declare yeye Lissu kwa vile ni already compromosed anauita ile report kuwa ni professorial rubbish. Bado hapo huelewi ndugu yangu. Najua utauliza ni lini hawa mawakili wameajiriwa na ACACIA. Kumbuka wakati ofisi za Fatuma Karume zilipoungua moto Lissu alisema nini kushawishi mawakili wengine wagome japo nao walimdharau. Kama umesahau aliwaaminisha kuwa hizo ofisi zilihujumiwa na serikali au maajenti wake kwa sababu Fatuma ni wakili wa ACACIA. Sasa jiulize ni nani anayetakiwa akombolewe kifikra? Ni nanai mwenye upeo mdogo au kiduchu cha kumtambua mtu ambaye jana alikuwa mzalendo leo kafikiwa bei amekuwa adui mkubwa wa nchi. Mungu ataendelea kumwadhibu Lissu mpaka ajirudi. Amen.
 
Hata sielewi wewe na mimi tunapishana wapi...! Ila ni hivi ndugu yangu nimegundua kuwa huwa unamfuatilia kwa ukaribu Tundu Lissu ndo maana ukasema amewafungua watanzania wenye juu ya ufisadi kwenye rasilimali za taifa hasa madini.

Hata siku moja Lissu hajawai support mtu yeyote anayeiba rasilimali zetu, anachozungumzia yeye ni kuchukuliwa kwa hatua SAHIHI dhidi ya wezi wa rasilimali za taifa, na si kuchukua hatua holela...!

Mara nyingi amekua akizungumza hizo hatua SAHIHI zianze kwenye kurekebisha SHERIA ndipo tuweze kuwadhibiti maana hao wawekezaji hawajavamia maeneo ya migodi yetu bali wameingia MIKATABA ya KINYONYAJI na watwana/watawala wanaojali matumbo yao na family zao.

Huko kukurupuka kuchukua hatua holela imelitia taifa hasara kwa mda mrefu, hatutaki kuona yakijirudia wakati watu wenye uwezo na maono kama Lissu wapo.

Mfano wa haraka na karibuni wa maamuzi ya kibabe na kukurupuka yalio ligarimu taifa ni pamoja na samaki wa jiwe, kusitishwa kwa mkataba wa makandarasi na jiwe hatimae pangaboi zikadakwa, meli bovu siku hizi lipo kwa wazamiaji ili tusihoji....! Hatupendi kuona hayo yakijirudia....
 
Nikupe pole tu ndugu yangu. Lissu wa wakati ule sio wa leo.
 
Tundu Lissu ni hazina kwa Taifa letu, sijui kwanini Taifa hili linaongozwa kwa hisia na chuki za kisiasa badala ya kuongozwa Na reasoning Na maslahi ya Taifa?
Hamna kitu hapo. Ndo alikuwa anasema tutashtakiwa miga huyo. Serikali inefanya yake acacia wakaamua kutoa $ 300m. Mkaanza kuikebehi serikali eti kila mtu apate noah. Sasa bora serikali ikae kimya tu mtabaki kupiga kelele kwa sababu hamjulikani mnataka nini wabongo
 
Duh!.
Kiukweli kuna wakati Mhe. Lissu yuko vizuri sana kisheria kama hapa
Hamna kitu hapo jamaa muhuni tu. Alisemaga tutashtakiwa miga sasa leo nataka kujua kilichotolowa ili iweje. Kama serikali ingemsikiliza yeye na kutofanya mazungumzo angekuja hapa saa ngapi kutaka kujua kilichotolewa
 
Nikupe pole tu ndugu yangu. Lissu wa wakati ule sio wa leo.
Mkuu watu wamejaa mahaba na mtu hawafatilii kinachoendelea, ila Mbowe na wenzake wanajua alichokifanya Lissu na ndo maana mwoga wa kurudi nchini.Alifikia hatua ya kuwa National threat, serikali inajua na inaona mengi ila watu wanaichukulia poa. Hajiulizi kwanini walipobomu ofisi za EMMMA Lissu alikuwa anajua nni mabox gani yamechukuliwa?,na akakomaa mawakili wote wagome, wenzake wakamuona mpuuzi. In short Tundu Lissu alivuna alichopanda.
 
Nimemsikia Waziri wa Sheria na Katiba, Dr. Palamagamba Kabudi akiliambia Bunge kwamba Serikali ya Rais John Magufuli haitatoa hadharani, na kwa hiyo Bungeni, taarifa zinazohusu fedha tulizolipwa na makampuni ya kigeni ya madini. Serikali ya Magufuli inahofu kwamba fedha hizo zikitangazwa hadharani basi wadai wetu mbali mbali watatufungulia kesi nyingi za madai, kwa sababu watajua sasa tuna fedha. Aidha, fedha hizo hazitalipwa kama maduhuli ya Wizara ya Madini. Maana yake ni kwamba taarifa ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini inayotolewa Bungeni kila mwaka, haitaonyesha mapato yanayotokana na madini.

(e) Ukiachia Sheria ya Ardhi ya 1999, hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kujitwalia kisheria umiliki wa utajiri na rasilmali asilia zote za nchi yetu, ikiwemo madini. Ukijumlisha na kauli kwamba sasa leseni zote za madini na, by extension, utajiri na rasilmali asilia nyingine zote zitatolewa na Baraza la Mawaziri,.......​
Tundu AM Lissu (MB)

University Hospital Leuven at Gasthuisberg, Leuven, BELGIUM
Kama haya ni kweli, (siamini) basi ule usemi kuwa maliasili katika Africa ni laana utakuwa umetimia
 
Hamna kitu hapo. Ndo alikuwa anasema tutashtakiwa miga huyo. Serikali inefanya yake acacia wakaamua kutoa $ 300m. Mkaanza kuikebehi serikali eti kila mtu apate noah. Sasa bora serikali ikae kimya tu mtabaki kupiga kelele kwa sababu hamjulikani mnataka nini wabongo

Hivi wameshatoa hiyo 300$? Duh mahaba mengine hatari sana!!!
 
Mkuu watu wamejaa mahaba na mtu hawafatilii kinachoendelea, ila Mbowe na wenzake wanajua alichokifanya Lissu na ndo maana mwoga wa kurudi nchini.Alifikia hatua ya kuwa National threat, serikali inajua na inaona mengi ila watu wanaichukulia poa. Hajiulizi kwanini walipobomu ofisi za EMMMA Lissu alikuwa anajua nni mabox gani yamechukuliwa?,na akakomaa mawakili wote wagome, wenzake wakamuona mpuuzi. In short Tundu Lissu alivuna alichopanda.

Sikujua kuwa huku JF kuna watu wanafuatilia mambo kisawasawa kama wewe. Naona contributors wengi ni wale wanaomhusudu mtu bila kufanya analysis yoyote ya mantiki ya anachofanya. Inakuwa kama nyumbu ambaye anafuata tu msafara hata kama huko mbele wenzie wanapata maafa, hivyo hivyo anachosema wanaomhusudu wanaona ni sawa kabisa. Yaani juzi mtu kasema hiki ni kibaya na hatari kwa taifa wanakubali 100% leo akigeuka kuwa kitu kile kile ni sahihi na wanaokipinga hawana nia nzuri nao wanasema kweli bwana. Huo ni unyumbu ila nashukuru kukusikia naamini kuwa watu wasiohusudu watu bali wanahusudu hoja wapo. Tujue Mungu anaipenda sana Tanzania na hao wasioitakia mema watasambaratika tu.
 
Huyo naye
Hivi vipi anafikiri awamu hii atahongwa pesa!!!.. bora anyamaze maana hana nondo bali amebakia kujaribu na kujaribu tu na kutoka bureeee..

Badala ya kuwachunguza wenzake nani haswa walimtenda kuwepo alipo huko. Kila anachoandika kinaishia kilipo chama chake huko ndani ya futi sita..
Law is not for the fuckd minded people like you.....jipange.
 
Hamna kitu hapo. Ndo alikuwa anasema tutashtakiwa miga huyo. Serikali inefanya yake acacia wakaamua kutoa $ 300m. Mkaanza kuikebehi serikali eti kila mtu apate noah. Sasa bora serikali ikae kimya tu mtabaki kupiga kelele kwa sababu hamjulikani mnataka nini wabongo
Nyie vijana nahisi munalipwa pesa nzuri sana kama sijakosea kwa mahandisha haya haramu....acha mulipwe tu munamidhambi....
 
ki
Nimemsikia Waziri wa Sheria na Katiba, Dr. Palamagamba Kabudi akiliambia Bunge kwamba Serikali ya Rais John Magufuli haitatoa hadharani, na kwa hiyo Bungeni, taarifa zinazohusu fedha tulizolipwa na makampuni ya kigeni ya madini. Serikali ya Magufuli inahofu kwamba fedha hizo zikitangazwa hadharani basi wadai wetu mbali mbali watatufungulia kesi nyingi za madai, kwa sababu watajua sasa tuna fedha. Aidha, fedha hizo hazitalipwa kama maduhuli ya Wizara ya Madini. Maana yake ni kwamba taarifa ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini inayotolewa Bungeni kila mwaka, haitaonyesha mapato yanayotokana na madini.

Kwenye suala hili na kwa kauli hii ya Waziri Kabudi, sasa ni wazi kwamba Serikali ya Magufuli haina tofauti yoyote ya kimsingi, na pengine ni ya hovyo zaidi ukilinganisha, na Serikali za watangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete na Ben Mkapa. Nitafafanua.

1. Usiri ulitawala masuala yote ya leseni, mikataba na malipo serikalini yaliyotokana na uchimbaji madini wakati wote wa tawala za Kikwete na Mkapa. Bunge lilinyimwa kuangalia na kuchunguza mikataba ya madini kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kikatiba ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

2. Usiri huu ulitengeneza mazingira yaliyozaa mikataba mibovu na ufisadi mkubwa katika sekta ya madini, ulioligharimu taifa letu mabilioni ya fedha za kigeni.

3. Kwa kauli ya Prof. Kabudi, usiri huu sio tu utaendelea, bali sasa utakuwa mkubwa zaidi kwa sababu leseni za uchimbaji madini zitatolewa na Baraza la Mawaziri, badala ya watendaji wa serikali. Kama inavyojulikana, majadiliano na maamuzi ya Baraza la Mawaziri ni siri kwa mujibu wa sheria zetu na Mawaziri wote hula kiapo cha kutunza siri hizo.

4. Usiri uliotangazwa na Prof. Kabudi unavunja wazi wazi Sheria za Rasilmali za Nchi zilizopitishwa kwa mbwembwe kubwa na majidai mengi Bungeni mwaka jana. Mpiga Mbwembwe Mkuu alikuwa Prof. Kabudi mwenyewe.

(a) Kifungu cha 12 cha Sheria ya Milki ya Kudumu ya Utajiri na Rasilmali za Asilia ya 2017 kinaruhusu Bunge kupitia mikataba yote inayohusu uchimbaji (extraction), utumiaji (exploitation) au upataji (acquisition) wa utajiri na rasilmali asilia kupitiwa na Bunge. Sasa, kwa kauli ya Prof. Kabudi, haitawezekana tena kwa Bunge kuipitia mikataba hiyo na hivyo kuiweka hadharani kwa wananchi.

(b) Wakati Prof. Kabudi amedai bungeni kwamba itakuwa ni marufuku kwa Serikali kuingia mikataba ya uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) kwa sababu mikataba hiyo imetuletea matatizo mengi sana, vifungu vyote muhimu vya Sheria ya Milki ya Kudumu ya Utajiri na Rasilmali Asilia vinahusu utaratibu wa 'mikataba' ya utajiri na rasilmali asilia, ikiwemo madini. Angalia tafsiri ya maneno 'arrangements or agreement' katika kifungu cha 3. Vifungu vingine husika vinavyohusika na mikataba ni 5(4), 6, 7, 8, 9, 10(1), 11(3) na 12.

(c) Ni sahihi, kwa hiyo, kusema kwamba Sheria ya Milki ya Kudumu ya Utajiri na Rasilmali Asilia imeweka utaratibu mpya wa 'mikataba', wakati Prof. Kabudi na wanafunzi wake wa sheria - Naibu Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu Kilangi - wanadai bungeni kwamba kuanzia sasa ni marufuku kuingia mikataba ya uendelezaji madini. Heri wale ambao hawakufundishwa na wabobezi hawa wa sheria!!!

(d) Kifungu cha 5(2) cha Sheria hii kinasema kwamba "utajiri na rasilmali asilia zitashikiliwa na Rais kama dhamana kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano." Haya pia ni masharti ya kifungu kipya cha 5(1) cha Sheria ya Madini kama ilivyorekebishwa mwaka jana.

(e) Ukiachia Sheria ya Ardhi ya 1999, hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kujitwalia kisheria umiliki wa utajiri na rasilmali asilia zote za nchi yetu, ikiwemo madini. Ukijumlisha na kauli kwamba sasa leseni zote za madini na, by extension, utajiri na rasilmali asilia nyingine zote zitatolewa na Baraza la Mawaziri, sasa madili yote ya kifisadi yatahamia Ikulu ya Magufuli na hatutayajua, kwa sababu tukiyajua wadai wetu watatushtaki mahakamani!!!

(f) Utaratibu huu wa kifisadi kwenye masuala ya rasilmali asilia za nchi yetu haukuwepo kabisa wakati wa Kikwete na Mkapa, ambao ndio wanaowajibika kwa kiasi kikubwa na hali aliyoikuta Magufuli alipoingia madarakani.​

5. Msimamo wa sasa wa Serikali ya Magufuli unakinzana moja kwa moja na matakwa ya Sheria ya Kupitiwa na Kujadiliwa Upya kwa Masharti Yasiyofaa ya Mikataba ya Utajiri na Rasilmali Asilia ya 2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts (Review na Re-Negotiation of Unconscionable Terms) Act, 2017).

(a) Wakati Prof. Kabudi amesema bungeni kwamba itakuwa ni marufuku kwa Serikali kuingia mikataba ya uendelezaji madini, Sheria hii yote inahusu kupitiwa na kujadiliwa upya kwa mikataba iliyopo sasa.

(b) Wakati Prof. Kabudi na Serikali ya Magufuli haitaki mikataba hii na fedha zinazopatikana kwa mujibu wake zijulikane kwa wananchi kupitia kwa wabunge wao, kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kinasema: "Kwa ajili ya utekelezaji kwa ufanisi wa kazi zake za usimamizi na ushauri zilizotajwa chini ya ibara ya 63(2) ya Katiba, Bunge linaweza kupitia taratibu zozote au makubaliano yaliyoingiwa na Serikali kuhusiana na utajiri na rasilmali asilia."

(c) Kifungu cha 5(1) kinaitaka Serikali kupeleka Bungeni mikataba yote ya utajiri na rasilmali asilia iliyoingiwa na Serikali ndani ya siku sita za Mkutano wa Bunge unaofuata kuingiwa kwa mikataba hiyo.

(d) Kwa vile Prof. Kabudi amekiri kwamba Serikali imekwishaingia makubaliano ya msingi na Barrick Gold kuhusu makinikia ya Bulyanhulu na Buzwagi; na pia na Tanzanite One kuhusiana na tanzanite ya Mererani, Serikali inawajibika kisheria, na wabunge wanatakiwa kudai, kuwasilishwa mikataba hiyo Bungeni katika Mkutano huu wa Bunge, ili Bunge liweze kuipitia na, ikihitajika, kuishauri Serikali kuanzisha majadiliano mapya kuhusu mikataba hiyo, kama inavyotakiwa na vifungu vya 5(2) na (3) vya Sheria hiyo.

Kutofanya hivyo ni kuendeleza ufisadi na usanii ule ule wa miaka ya Kikwete na Mkapa ambao Magufuli anajidai kuwa anapambana nao.​

6. Prof. Kabudi amesema bungeni kwamba kuanzia sasa leseni zote za uchimbaji madini zitatolewa na Baraza la Mawaziri. Kama kawaida yake, Waziri huyu msomi anapotosha wabunge au anafanya maandalizi ya kukiuka sheria alizoziwasilisha bungeni yeye mwenyewe na mbwembwe nyingi na madaha makubwa.

(a) Baraza la Mawaziri halijatajwa mahali popote katika Sheria ya Madini kama ilivyorekebishwa mwaka jana. Badala yake, wajibu wa kutoa leseni zote za uchimbaji madini umekabidhiwa kwa Tume ya Madini, kwa usimamizi wa Waziri wa Madini. Angalia kifungu kipya cha 19(f) cha Sheria ya Madini.

(b)Tume ya Madini ndiyo uwezo wa kusimamisha au kufuta kabisa leseni yoyote ya madini. Angalia kifungu kipya cha 24(m) cha Sheria ya Madini. Itakuwa maajabu ya Tanzania kwa Tume iliyoteuliwa na Rais kufuta leseni iliyotolewa na Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Rais.

Haya ndiyo ya Magufuli na watu wake wanaojifanya kwa wananchi kuwa ndio watetezi wa madini na rasilmali asilia za nchi yetu.
Ni usanii mtupu. Ni ukiukaji mtupu wa sheria walizozipitisha wenyewe na wanazozipigia debe kila kukicha. Ni maandalizi ya ufisadi mkubwa zaidi; au mwendelezo wa ufisadi wa miaka ya Kikwete na Mkapa. Waheshimiwa wabunge na Watanzania wanatakiwa kuyaelewa haya na kuyachukulia hatua.
Tundu AM Lissu (MB)

University Hospital Leuven at Gasthuisberg, Leuven, BELGIUM

ndio mabeberu wako wamekutuma hivyo tena, jaribu tena mbinu nyingine, tumeshakugundua wenye akili, utanyoosha tu maneno kwa serikali hii!
Na watakapo gundua kuwa hawakuhitaji tena watakubwaga kama gunia la mkaa ndipo utawajua hao sio wenzio kabisa.
 
Back
Top Bottom