Tundu Lissu: Rais Magufuli hana tofauti na Kikwete, Mkapa kwenye usiri kuhusu madini

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Nimemsikia Waziri wa Sheria na Katiba, Dr. Palamagamba Kabudi akiliambia Bunge kwamba Serikali ya Rais John Magufuli haitatoa hadharani, na kwa hiyo Bungeni, taarifa zinazohusu fedha tulizolipwa na makampuni ya kigeni ya madini. Serikali ya Magufuli inahofu kwamba fedha hizo zikitangazwa hadharani basi wadai wetu mbali mbali watatufungulia kesi nyingi za madai, kwa sababu watajua sasa tuna fedha. Aidha, fedha hizo hazitalipwa kama maduhuli ya Wizara ya Madini. Maana yake ni kwamba taarifa ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini inayotolewa Bungeni kila mwaka, haitaonyesha mapato yanayotokana na madini.

Kwenye suala hili na kwa kauli hii ya Waziri Kabudi, sasa ni wazi kwamba Serikali ya Magufuli haina tofauti yoyote ya kimsingi, na pengine ni ya hovyo zaidi ukilinganisha, na Serikali za watangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete na Ben Mkapa. Nitafafanua.

1. Usiri ulitawala masuala yote ya leseni, mikataba na malipo serikalini yaliyotokana na uchimbaji madini wakati wote wa tawala za Kikwete na Mkapa. Bunge lilinyimwa kuangalia na kuchunguza mikataba ya madini kama sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kikatiba ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

2. Usiri huu ulitengeneza mazingira yaliyozaa mikataba mibovu na ufisadi mkubwa katika sekta ya madini, ulioligharimu taifa letu mabilioni ya fedha za kigeni.

3. Kwa kauli ya Prof. Kabudi, usiri huu sio tu utaendelea, bali sasa utakuwa mkubwa zaidi kwa sababu leseni za uchimbaji madini zitatolewa na Baraza la Mawaziri, badala ya watendaji wa serikali. Kama inavyojulikana, majadiliano na maamuzi ya Baraza la Mawaziri ni siri kwa mujibu wa sheria zetu na Mawaziri wote hula kiapo cha kutunza siri hizo.

4. Usiri uliotangazwa na Prof. Kabudi unavunja wazi wazi Sheria za Rasilmali za Nchi zilizopitishwa kwa mbwembwe kubwa na majidai mengi Bungeni mwaka jana. Mpiga Mbwembwe Mkuu alikuwa Prof. Kabudi mwenyewe.

(a) Kifungu cha 12 cha Sheria ya Milki ya Kudumu ya Utajiri na Rasilmali za Asilia ya 2017 kinaruhusu Bunge kupitia mikataba yote inayohusu uchimbaji (extraction), utumiaji (exploitation) au upataji (acquisition) wa utajiri na rasilmali asilia kupitiwa na Bunge. Sasa, kwa kauli ya Prof. Kabudi, haitawezekana tena kwa Bunge kuipitia mikataba hiyo na hivyo kuiweka hadharani kwa wananchi.

(b) Wakati Prof. Kabudi amedai bungeni kwamba itakuwa ni marufuku kwa Serikali kuingia mikataba ya uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) kwa sababu mikataba hiyo imetuletea matatizo mengi sana, vifungu vyote muhimu vya Sheria ya Milki ya Kudumu ya Utajiri na Rasilmali Asilia vinahusu utaratibu wa 'mikataba' ya utajiri na rasilmali asilia, ikiwemo madini. Angalia tafsiri ya maneno 'arrangements or agreement' katika kifungu cha 3. Vifungu vingine husika vinavyohusika na mikataba ni 5(4), 6, 7, 8, 9, 10(1), 11(3) na 12.

(c) Ni sahihi, kwa hiyo, kusema kwamba Sheria ya Milki ya Kudumu ya Utajiri na Rasilmali Asilia imeweka utaratibu mpya wa 'mikataba', wakati Prof. Kabudi na wanafunzi wake wa sheria - Naibu Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu Kilangi - wanadai bungeni kwamba kuanzia sasa ni marufuku kuingia mikataba ya uendelezaji madini. Heri wale ambao hawakufundishwa na wabobezi hawa wa sheria!!!

(d) Kifungu cha 5(2) cha Sheria hii kinasema kwamba "utajiri na rasilmali asilia zitashikiliwa na Rais kama dhamana kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano." Haya pia ni masharti ya kifungu kipya cha 5(1) cha Sheria ya Madini kama ilivyorekebishwa mwaka jana.

(e) Ukiachia Sheria ya Ardhi ya 1999, hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kujitwalia kisheria umiliki wa utajiri na rasilmali asilia zote za nchi yetu, ikiwemo madini. Ukijumlisha na kauli kwamba sasa leseni zote za madini na, by extension, utajiri na rasilmali asilia nyingine zote zitatolewa na Baraza la Mawaziri, sasa madili yote ya kifisadi yatahamia Ikulu ya Magufuli na hatutayajua, kwa sababu tukiyajua wadai wetu watatushtaki mahakamani!!!

(f) Utaratibu huu wa kifisadi kwenye masuala ya rasilmali asilia za nchi yetu haukuwepo kabisa wakati wa Kikwete na Mkapa, ambao ndio wanaowajibika kwa kiasi kikubwa na hali aliyoikuta Magufuli alipoingia madarakani.​

5. Msimamo wa sasa wa Serikali ya Magufuli unakinzana moja kwa moja na matakwa ya Sheria ya Kupitiwa na Kujadiliwa Upya kwa Masharti Yasiyofaa ya Mikataba ya Utajiri na Rasilmali Asilia ya 2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts (Review na Re-Negotiation of Unconscionable Terms) Act, 2017).

(a) Wakati Prof. Kabudi amesema bungeni kwamba itakuwa ni marufuku kwa Serikali kuingia mikataba ya uendelezaji madini, Sheria hii yote inahusu kupitiwa na kujadiliwa upya kwa mikataba iliyopo sasa.

(b) Wakati Prof. Kabudi na Serikali ya Magufuli haitaki mikataba hii na fedha zinazopatikana kwa mujibu wake zijulikane kwa wananchi kupitia kwa wabunge wao, kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kinasema: "Kwa ajili ya utekelezaji kwa ufanisi wa kazi zake za usimamizi na ushauri zilizotajwa chini ya ibara ya 63(2) ya Katiba, Bunge linaweza kupitia taratibu zozote au makubaliano yaliyoingiwa na Serikali kuhusiana na utajiri na rasilmali asilia."

(c) Kifungu cha 5(1) kinaitaka Serikali kupeleka Bungeni mikataba yote ya utajiri na rasilmali asilia iliyoingiwa na Serikali ndani ya siku sita za Mkutano wa Bunge unaofuata kuingiwa kwa mikataba hiyo.

(d) Kwa vile Prof. Kabudi amekiri kwamba Serikali imekwishaingia makubaliano ya msingi na Barrick Gold kuhusu makinikia ya Bulyanhulu na Buzwagi; na pia na Tanzanite One kuhusiana na tanzanite ya Mererani, Serikali inawajibika kisheria, na wabunge wanatakiwa kudai, kuwasilishwa mikataba hiyo Bungeni katika Mkutano huu wa Bunge, ili Bunge liweze kuipitia na, ikihitajika, kuishauri Serikali kuanzisha majadiliano mapya kuhusu mikataba hiyo, kama inavyotakiwa na vifungu vya 5(2) na (3) vya Sheria hiyo.

Kutofanya hivyo ni kuendeleza ufisadi na usanii ule ule wa miaka ya Kikwete na Mkapa ambao Magufuli anajidai kuwa anapambana nao.​

6. Prof. Kabudi amesema bungeni kwamba kuanzia sasa leseni zote za uchimbaji madini zitatolewa na Baraza la Mawaziri. Kama kawaida yake, Waziri huyu msomi anapotosha wabunge au anafanya maandalizi ya kukiuka sheria alizoziwasilisha bungeni yeye mwenyewe na mbwembwe nyingi na madaha makubwa.

(a) Baraza la Mawaziri halijatajwa mahali popote katika Sheria ya Madini kama ilivyorekebishwa mwaka jana. Badala yake, wajibu wa kutoa leseni zote za uchimbaji madini umekabidhiwa kwa Tume ya Madini, kwa usimamizi wa Waziri wa Madini. Angalia kifungu kipya cha 19(f) cha Sheria ya Madini.

(b)Tume ya Madini ndiyo uwezo wa kusimamisha au kufuta kabisa leseni yoyote ya madini. Angalia kifungu kipya cha 24(m) cha Sheria ya Madini. Itakuwa maajabu ya Tanzania kwa Tume iliyoteuliwa na Rais kufuta leseni iliyotolewa na Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Rais.

Haya ndiyo ya Magufuli na watu wake wanaojifanya kwa wananchi kuwa ndio watetezi wa madini na rasilmali asilia za nchi yetu.
Ni usanii mtupu. Ni ukiukaji mtupu wa sheria walizozipitisha wenyewe na wanazozipigia debe kila kukicha. Ni maandalizi ya ufisadi mkubwa zaidi; au mwendelezo wa ufisadi wa miaka ya Kikwete na Mkapa. Waheshimiwa wabunge na Watanzania wanatakiwa kuyaelewa haya na kuyachukulia hatua.
Tundu AM Lissu (MB)

University Hospital Leuven at Gasthuisberg, Leuven, BELGIUM
 
Dragoon

JAJI FELESHI – UTEUZI UNAODHIHIRISHA KUTIKISIKA KWA MHIMILI WA MAHAKAMA


Mhimili wa Mahakama ni moja ya nguzo kuu za dola. Hata hivyo teuzi zinazofanywa na watawala, hususani zinazogus aongozi wa mahakama, zinadhoofisha umoja na mshikamano katika mhimili huu, ikiwa ni pamoja na ufanisi wa utendaji kazi.


Hivi karibuni Raisi wa Jamhuri kafanya uteuzi wa Jaji Kiongozi- ndugu Feleshi ambae anachukua nafasi ya Jaji FKL Wambali. Kabla ya hapo kulikuwa na teuzi zingine za majaji wa mahakama kuu, zikimuweka katika ujaji aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali, George Masaju. Japo Mahakama ina siri zake, lakini nitaweka wazi ili tu mamlaka husika zifahamu na zifanyie kazi suala hili.

1. UTEUZI WA FKL WAMBALI KUWA JAJI KIONGOZI

Kwa macho na masikio ya nje ingekuwa si rahisi kufahamu muonekano wa jaji wambali kwa majaji wengine katika mhimili wa mahakama. Kipindi Wambali akiwa Naibu msajili wa Mahakama ya rufani, majaji wengi walikuwa wakimchukia kwa vitendo vyake vya kinafiki. Alikua kila asikiapo jambo linalomhusu basi atalifikisha kwa jaji mkuu mara moja. Pindi alipoteuliwa kuwa jaji wa Mahakama kuu (2012) alipata wakati mgumu sana. Hata majaji wenzake walimtenga na ilimbidi ashinde ofisini tu. Wakati mwingine wakati wa chakula ilibidi apelekewe chakula ofisini kwake wakati majaji wengine wakijumuika mesini kupata chakula.


Uvumilivu ulimsaidia. Taratibu majaji walimkubali, ukijumlisha na wale wapya walioteuliwa kipindi kimoja na wale majaji wasio wazawa (wahamiaji). Kuteuliwa kwake kuwa jaji kiongozi kulikaribishwa ka mikono miwili kwa sababu kuu mbili. Kwanza kwa utendaji wake mzuri wa kazi. Pili kwa kufurahia kuondoshwa kwa mtangulizi wake.


Kiutendaji jaji wambali ni mzuri. Ni mchapa kazi na hana simile katika masuala ya kazi. Kupekekwa kwake mahakama ya rufani bila shaka kutakuwa na tija. Sijajua sababu zilizofanya apandishwe na kuondolewa katika nafasi yake kabla hata hatujaona matunda yake yakiiva.


2. UTEUZI WA PROF. JUMA KUWA JAJI MKUU

Uteuzi huu ulikuja kama suala la kushangaza kwa wale majaji wazawa. Ingawaje ilitazamiwa (kwa sababu alitumikia u-naibu jaji mkuu kwa takribani mwaka mzima), wapo ambao hawakupendezwa. Jaji huyu amepewa uongozi wa mhimili wa mahakama mapema mno-wakati bado angali mchanga na akiwa na ombwe la kuifahamu vizuri mahakama. Ukizingatia si mzawa wa mahamaka.

3. UTEUZI WA SHABAN LILA KUWA JAJI KIONGOZI

Uteuzi huu ulileta kashkash na patashika katika mhimili wa mahakama. Mara tu ya kupata uteuzi, Hamisha hamisha ya majaji wa mahakama kuu ulianza. Wasajili nao walishuhudia wakati mgumu, wachache wakineemeka. Alikuwa na uhusiano hasi na mtangulizi wake, jaji F. Jundu. Mara tu ya kuingia ofisini alianza kupangua mipango yote iliyowekwa na mtangulizi wake, na ilifikia wakati Jundu aligoma kuondoka ofisini kwa kuhofia kuharibiwa kwa mipango yake, na pengine kufuchuliwa kwa baadhi ya mambo. Ugomvi wao ulikuwa bayana kiasi kwamba ulionekana dhahiri mbele ya watumishe wa Mahakama.

Kuondolewa kwake katika nafasi hii kuligeuka ahueni kwa watumishi wa Mahakama, hasa majaji, mahakimu na wasajili. Walifurahia, wakijua kwamba sasa hakuna tena utendaji wa kukomoana na utawala wa makundi. Kutokudumu kwake katika kiti hiki ni kwa makusudi ya kokoa jahazi la mahakama.

4. UTEUZI WA M CHANDE KUWA JAJI MKUU

Huyu alipata uteuzi wa kuwa jaji mara tu Kikwete alipopata kuwa Raisi wa Jamhuri. Aliteuliwa wakati akiwa na majukumu mengine, tena nje ya nchi. Alipoanza kutumikia ujaji kwa kweli utendaji wake ulikuwa wa kutegemea gia au spana. Watumishi wa mahakama walifanya jitihada kumfundisha namna ya kufanya kazi maana alikuwa hafahamu. Makarani waligeuka kua majaji, na majaji walikuwa waalimu.

Uzuri wake hakuwa mkorofi. Watumishi walimpokea na kumpenda. Tatizo lake alipenda sana wanawake (ngono). Alichukua watumishi wa mahakama na kuwageuza wake zake. Alipanda madaraja haraka hadi akateulewa kuwa jaji mkuu. Uteuzi wake ulileta songombingo kama sio kasheshe ndani ya mahamaka. Kwanza majaji wa rufani hawakupendezwa na kupanda kwake harakaharaka. Pili aliwaacha wazawa wakishangaa shangaa tu wasijue la kufanya, wakilalamika tangu lini mahakama inaongozwa na mtu asiye mzawa na mdogo kabis amiongoni mwa majaji? tatu mtu waliyemweka tayari (jaji A.S. Bwana) kwa ajili ya kuchukua mikoba ya ujaji mkuu alitupiliwa mbali.


Uteuzi wake ulisababisha majaji wa rufani kugoma na kutishia kujiuzuru. Kwa vile ingekuwa ni aibu kubwa duniani nzima kwa majaji wa rufaa wa nchi kujiuzuru, na kumuondoa jaji mteule madarakani si rahisi, juhudi kubwa zilifanyika kuinusuru Tanzania na kadhia hii. Muafaka ulifanyika, na moja ya makubaliano ni kupunguza madaraka ya jaji mkuu. Hata hivyo majaji wawili wa rufaa walishikilia msimamo wao na wakang’atuka,- sababu za uongo zikatolelewa na ukweli ukafichwa kuhusu kujiuzuru kwao.

Mheshimiwa huyu alifanya ubadhirifu na upendeleo mkubwa katika uongozi wake. Mfano ni pale alipochota kiasi cha TSh. 100,000,000 (millioni mia moja) za mahakama kwa ajili ya mazishi ya ndugu yake. Pia alishinikiza kupewa tenda kwa mtu mmoja (jina kapuni) kwa ajili ya chakula cha majaji na kantini ya mahakama ya Rufani.


5. UTEUZI WA E. FELESHI KUWA JAJI KIONGOZI

Feleshi si mzawa wa mahakama. Ni miongoni mwa majaji junior kabisa katika idara ya mahakama. Hata hivyo hili si suala la msingi hapa. Cha msingi ni utendaji kazi wa mheshimiwa huyu. Sitajikita sana katika utendaji wake kazi kipindi alipokuwa DPP, zaidi ya kusema kwamba alukumbatia mafisadi, wala rushwa na wauza mihadarati (madawa ya kulevya) katika utawala wake. Mafaili mengi yalifika kwake kwa ajoli ya mashtaka kufunguliwa kwa mujibu wa sheria lakini mwisho wake yaliishia kuwekwa kabatini tu.


Feleshi si mchapa kazi: tokea ateuliwe kuwa jaji Mheshimiwa huyu hajaonesha msingi wowote ule katika maamuzi yake. Kuwa na maamuzi ya kukumbuwa na yenye ubora ni moja ya silaha kuubwa kabisa kwa wanasheria. Kwa huu jaji ni hohehahe! Hana maamuzi yoyote na hukumu zake ni za kinyonge tu. Pia si adjudicator mzuri (mwamuzi). Kesi zilizopo kwa jaji feleshi hazimaliziki kwa wakati.

Feleshi hama mshikamano: jaji huyu hana desturi ya kushirikiana na majaji wenzake. Sijui kana ni sababu ya ubinafsi au anazo sababu anazozijua yeye. Mahakama ni mhimili unaohitaji ushirikiano, hasa baina ya viongozi.

Feleshi ni mbadhirifu: amekuwa akiweka shinikizo kwa watawala na watumishi wengine wa mahama kufanikisha malipo ya masuala yake binafsi. Ameshinikiza kufanyiwa malipo kwa ajili ya hawara yake anayemtumia kumsaidia kazi zake. Hawara huyu si mwajiriwa wa Mahakama wala taasisi yeyote ya serikali, lakini amekuwa akishinda ofisini asubuhi hadi jioni. Tena anasafiri na mheshimiwa katika safari za kikazi. Mtu huyu amekuwa akilipwa na mahakama malipo mbalimbali kama vile posho, pesa ya kujikumu na pesa ya safari. Hii inakuja sababu tu yuko nyuma ya jaji Feleshi!

Feleshi ni fuska: amekuwa akiendekeza ngono hadi ofisini. Anajifungia katika ofisi ya umma, tena wakati wa kazi na hawara yake na kukwamisha shughuli za kimahakama. Hawara yake anafahamika.


6. HITIMISHO

Uzawa ni jambo la msingi sana katika mhimili wa mahakama. Majaji wazawa wanaijua mahakama vizuri na namna ya kuiendesha. Majaji wasio wazawa siku zote wamekuwa kero na chanzo cha migogoro katika mhimili wa mahakama. Utendaji kadhi umeshuka, nidhamu imeshuka na hata makundi yanarudi. Hii ni sababu tu ya teuzi zinazofanya zisivyozingatia seniority.

Pamoja na jaji wambali (ambaye kwa nafasi aliyokuwa nayo anastahili) kupandishwa kwenda mahakama ya rufani, yupo Jaji Mwanaisha Kwariko. Huyu ni jaji wa mda kidogo. Hata hivyo hakuna sababu za kumpeleka mahakama ya rufani. Narudia tena, hakuna sababu yakumpeleka mahakama ya rufani. Kwanza ni jaji wa kawaida sana, maamuzi yake ni ya kawaida yasiyo na hoja yeyote. Mahakma ya rufani ataenda kurekebisha maauzi ya nani wakate yeye mwenyewe si mzuri kichwani?

Pili jaji Kwariko ana kiburi (pengine kwa kutegemea ma-godfather). Ni mara ngapi jaji kwariko anapangiwa kitua cha kazi anakataa kwenda kwa sababu anazozijua yeye? Ni mara ngapi anahamisha anakataa kuhama? Mara nyingine jaji huyu anajopangea kituo cha kazi anachokitaka yeye. Leo anapandishwa kwenda rufaa, tutegemee nini?

Mahakama ya enzi zile (enzi za kina Nyalali na kina Samata) ilikuwa ni mahakama. Majaji walikuwa ni majaji, mahakimu walikuwa majakimu na watumishi walikuwa ni watumishi kweli. Si Mahakam ya leo, inayonuka rushwa, ngono na upendeleo. Nidhamu hakuna na ufanisi wa kazi unashuka kila kukicha.

Kwa msingi huu basi, uteuzi wa viongozi hawa wa juu wa mahakama (ukiachilia mabali nafasi ya ujaji wa Mahakam kuu) ufanywa kwa uangalifu na kwa kuzingatia matakwa ya mhimili wa mahakama. Mahakama si kama taasiti zingine kama vile TRA ua TANROADS. Ina maadili yake na ina utukufu wake, kama tu ilivyo kwa bunge na ikulu. Utaratibu wa zamani urejewe na uheshimiwe. Mahakama isifanywe kitengo cha Ikulu au kitengo cha usalama wa taifa.
Mwisho wa kunukuu
 
Huyo naye
Hivi vipi anafikiri awamu hii atahongwa pesa!!!.. bora anyamaze maana hana nondo bali amebakia kujaribu na kujaribu tu na kutoka bureeee..

Badala ya kuwachunguza wenzake nani haswa walimtenda kuwepo alipo huko. Kila anachoandika kinaishia kilipo chama chake huko ndani ya futi sita..
 
Huyo naye
Hivi vipi anafikiri awamu hii atahongwa pesa!!!.. bora anyamaze maana hana nondo bali amebakia kujaribu na kujaribu tu na kutoka bureeee..

Badala ya kuwachunguza wenzake nani haswa walimtenda kuwepo alipo huko. Kila anachoandika kinaishia kilipo chama chake huko ndani ya futi sita..
Ama kweli kuna watu na viatu
 
Huyo naye
Hivi vipi anafikiri awamu hii atahongwa pesa!!!.. bora anyamaze maana hana nondo bali amebakia kujaribu na kujaribu tu na kutoka bureeee..

Badala ya kuwachunguza wenzake nani haswa walimtenda kuwepo alipo huko. Kila anachoandika kinaishia kilipo chama chake huko ndani ya futi sita..
Bibi hoja za lissu zinajieleza hapo juu,lakini kwakuwa unajua wazi huwezi kuzijibu,au hata kuzijadili hoja hizo umeamua kwa makusudi kwenda nje ya mada husika.hii inadhihirisha ulivyo masikini wa fikra JIBU HOJA NA SIO KUMJADILI MTOA HOJA.
 
Huyo naye
Hivi vipi anafikiri awamu hii atahongwa pesa!!!.. bora anyamaze maana hana nondo bali amebakia kujaribu na kujaribu tu na kutoka bureeee..

Badala ya kuwachunguza wenzake nani haswa walimtenda kuwepo alipo huko. Kila anachoandika kinaishia kilipo chama chake huko ndani ya futi sita..
Jadili alichosema Lissu na sio personal attacks..
Bado upo mweupe tu Kichwani??
 
Kwenye heading isomeke ni Tundu Lissu ndio kayasema haya/katoa bandiko hili.

CC: JamiiForums

Back to the topic, Mungu alikunusuru kwasababu alijua kuna kazi aliyokutuma ambayo bado hujaikamilisha.

Endelelea kufanya kile Mungu alichokusudia ukifanye kwa niaba ya watanzania na Taifa hili.

Niseme tu kuwa,Tundu Lissu is a special God's envyo to Tanzania.

Bandiko hili ni ushahidi mwingine kuwa yale yanayosemewa kuhusu Mererani huenda ni ya kweli kabisa.
 
Mbona wao wanafanya usiri hawatuambii bado operation ngapi kila siku inaibuka mpya!
 
Huyo naye
Hivi vipi anafikiri awamu hii atahongwa pesa!!!.. bora anyamaze maana hana nondo bali amebakia kujaribu na kujaribu tu na kutoka bureeee..

Badala ya kuwachunguza wenzake nani haswa walimtenda kuwepo alipo huko. Kila anachoandika kinaishia kilipo chama chake huko ndani ya futi sita..
We sheria za madini unazijua?wakati mwingine muwe mnatafakari hata kidogo basi
 
Back
Top Bottom