Tundu Lissu: Prof. Kabudi anajipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote

Lisu naye ni wale wale tu, alikuwa anajipendekeza kwa wazungu kwa kututishia kuwa tukiwachukulia hatua yeyote ile watatushitaki Miga.
 
Kumbe na wewe ni mpumbavu!!
 
Kuna Professor kutoka jalalani (UDSM) aliongoza uchunguzi wa makinikia na masuala ya madini akaja na report ya tume aliyoiongoza. Tundu Lissu alipoisoma hakukaa kimya, ali comment kwa kuiita Professorior Rubbish.

Wote tunatambua na kukubaliana kuwa Rubbish kwake ni jalalani. Inakuwaje hivi sasa watu wanatumia nguvu nyingi kumuandama Prof. Kabudi kwa kukiri kwake kuwa ameokotwa kutoka Jalalani (UDSM)? Ina maana mara hii wamesha sahau kuwa wakati fulani waliwahi kumshangilia Tundu Lissu?

Kwa wale wanaomtetea Prof. Kabudi hivi sasa ina maana na wao mara hii wamesahau kuwa wakati fulani waliwahi kumshambulia Tundu Lissu kwa kuthubutu kumsema Professor kuwa alichokifanya kilikuwa ni Professorior Rubbish?

Hebu makundi haya mawili yakae chini na kushikana mikono, kwani hadi hivi sasa mshindi ni Tundu Lissu, ninyi mashabiki hakuna mshindi kati yenu, mmetoshana nguvu.
 
Umewaza mbali na sahihi kabisa. Bravo!
 
Nafikiri unapaswa kuelewa hili.

Kuna utofauti wa kimuktadha, Proffesor Kabudi kama sehemu ya kamati ni tofauti na Proffesor Kabudi kama mtu binafsi.

Lisu ali attack ripoti ya kamati na opinions zake zilikuwa professionally , Kabudi yeye amejizungumzia personally na experience yake.

Ni sawa na mwanaume kama mume wa mke na mwanaume kama baba wa familia ni mazingira tofauti, mtu huyo mmoja anaweza kufanya jambo lile lile lakini tafsiri ikawa tofauti kwasababu amefanya ktk nafasi tofauti za kimamlaka.

Every situation is situational.
 
Nimekumbuka zamani jinsi ambavyo mitaani tulioishia darasa la saba tulivyokuwa tunawaogopa watu wanaoitwa maprofesa. Anapita Profesa akitembea kwa miguu mtaani kwenu, tunanong’onezana ‘profesa huyo!’.

Unadhani ni kwa nini ilikuwa hivyo? Zamani tuliwaheshimu maprofesa kwa elimu yao. Wengi hawakuwa matajiri. Tulihofia zaidi akili zao. Tulifikiria jinsi ambavyo walikuwa wana uwezo wa kufikiria mambo kwa upana zaidi bila ya kuyageuka siku za usoni.

Kadri siku zinavyosonga sisi tulioishia elimu ya darasa la saba Shule ya Msingi Mapambano na kwingineko hatuna hofu sana wala wivu juu ya akili zao. Wala hatuna wivu sana kwamba lazima tufike walikofika.

Wengi, hasa walioingia katika siasa, akili zao ni sawa na zetu wa darasa la saba. Unamkuta Profesa uliyekuwa unamheshimu sana anaongea vitu vya ajabu. Afadhali angekuwa anaongea hayo huku akiwa ni msimamo wake wa muda mrefu uliopita. Hapana, ni mtu ambaye miezi 36 nyuma alikuwa anaongea lugha nyingine. Unajiuliza ni huyu huyu Profesa Njaakali au mwingine?

Kuna watu ambao majina yao yanaanzia na Dk yaani dokta, nao ni hivyohivyo. Unamshangaa mtu ambaye miezi 36 uliiamini akili yake. Ulikuwa unapenda kumuona akiongoza mijadala. Leo ghafla akili yake na mimi wa darasa la saba zimefanana. Mara nyingi katika ubongo wa mwanadamu akili huanzia chini kwenda juu. Ukibakia darasa la saba unabakia hivyo hivyo. Lakini siku hizi kuna watu ambao akili zao zinatoka juu zinakuja chini. Zinatukuta darasa la saba kama walivyotuacha.

Nadhani akili zao tungeendelea kuziheshimu kama wangeachwa wafanyie kazi mambo waliyosomea. Wakiingia katika siasa wanarudi kuwa darasa la saba. Mtu ambaye majuzi alidai Katiba ni lazima halafu leo anasema sio lazima, ana tofauti gani na mimi darasa la saba ambaye sijui kama Katiba ni lazima au sio lazima?

Matokeo yake ule wivu wetu kwa maprofesa umeondoka. Wivu wetu kwa madokta haupo. Wakati mimi wa darasa la saba nipo katika kituo cha basi nikikaba abiria na kuchomoa pochi zao na wao kumbe ni kama wanakaba tu katika maeneo mengine ya heshima kwa ajili ya kusaka riziki. Acha maisha yaendelee.
 
Ajira zipi mkuu, hata miezi mitatu hajamaliza wizara ya mambo ya nje,au na wewe ndiyo wale wapumbavu wa Magufuli
 
Maelezo haya nayakubali na ni vizuri kutoa changamoto kwa viongozi ambao wanapotoka. Lakini Kabudi sasa hivi ni mwanasiasa kama alivyo Lissu. Je, Lissu mwenyewe ni mkweli kiasi anachokitaka? Nauliza tena Lissu ni mkweli kiasi cha kumporomoshea mwenzake matusi na kumpa sifa ya kujikomba?

Ktk uandishi huu Lissu anajionyesha kwamba alimjua sana Kabudi tangu siku za nyuma na kwamba msimamo wake ktk tume ya katiba aliushangaa. Naamini huo ni uongo. Kwa mdomo wa Lissu, kama angeushangaa basi angesema wakati ule. Lissu ni mtu asiye na 'kaba' ya miaka 5 hadi leo ndo atoe maelezo ya tabia ya Kabudi kwa miaka 5 iliyopita. Ni kutafuta sifa asizokuwa nazo yeye mwenyewe.
 
Tukianzisha timu ya mpira wa miguu ya maprofesa itakuwaje?
Key players ni; Golini analinda Dr Benson Bana, wakati beki mstaarabu ni Profesa Kitila Mkumbo, midfielder anakiputa propesa Lipumba na striker Kabudi mwenyewe!
Hiyo yaweza kuwa na slogan ya KUFUNGWA TWAFUNGWA LAKINI CHENGA TWAWALA
 
hata siku moja Lissu hawezi kumuita wala kuita kilichoandikwa na prof.Kabudi rubbish , huyo Lissu anaijua shughuli ya profesa vizuri. Mabeberu waijua shughuli ya Kabudi na wameanza kutumia vibeberu kumtikisa, ule ni mwamba wa win-win situation
 
Kabla hayajashambuliwa alikuwa anamwomba nani? Au kabudi nae kashambuliwa?(compromised) tuwe wakweli ili nchi iende mbele Rais apate watu sahihi!.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…