Tundu Lissu: Prof. Kabudi anajipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote

  • Thread starter Missile of the Nation
  • Start date
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,938
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,938 2,000
*Inaandikwa na Mhe Tundu Lissu*

Katika kitabu chake 'Intellectuals at the Hill' (kilichapishwa miaka ya kati ya '90), Prof. Issa G. Shivji aliwahi kusema kuwa kuna tabia ya wasomi wetu kujipendekeza na kujikomba kwa watawala na kufanya mambo ya hovyo kuliko warasimu wa kawaida, hasa wanapopewa vyeo vya uteuzi na Rais.

Prof. Pala Kabudi ni mfano mzuri wa wasomi wa aina hii. Ni mtu ambaye amejipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote ya kitaaluma.

Ukiachia msimamo wake akiwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambao mimi binafsi niliushangaa sana, Prof. Kabudi hana historia yoyote ya msimamo huru katika masuala muhimu ya nchi.

Ana akili za kitaaluma nyingi sana, lakini ana tabia ya kujikomba na kujipendekeza inayotia kinyaa na kufuta sifa zote za usomi wake.

Alitumiwa sana na Serikali ya Jakaya Kikwete na ya Ben Mkapa kabla ya hapo kama consultant wa masuala mbali mbali ya kisheria. Kwa hiyo anahusika kwa kiasi fulani na uchafu wa Kikwete na Mkapa ambao yeye na Magufuli wanajifanya kuukataa sasa.

Alikuwa mwandishi habari wa Uhuru/Mzalendo wakati wa Vita ya Kagera na, aliwahi kutuambia akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya LEAT, alitunukiwa zawadi na Mwalimu Nyerere kwa uandishi wa makala za propaganda zilizokuwa zinahusu Vita hiyo.

Prof. Kabudi amekuwa Chuo Kikuu cha Dar, kama mwanafunzi na kama mwalimu, tangu mwaka '80 hadi alipostaafu mwaka '16. Amekaa Ujerumani na kusomea Frei Universiteit Berlin, mojawapo ya vyuo vikuu maarufu kabisa barani Ulaya na duniani, kwa miaka 9.

Amekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar, na mjumbe wa Tume ya Katiba aliyeteuliwa na Rais Kikwete.

Huyu mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la Anglican, sio mtu aliyezaliwa kwenye vumbi na kuishi kwenye ufukara. Hakutolewa jalalani kokote na Rais Magufuli. Amekuwa na bado ni sehemu ya top elite ya Tanzania.

Alichokisema mbele ya Rais Magufuli sio cha kweli hata kidogo, lakini ni ishara kamili ya hulka yake ya kujidhalili na kujikomba ili aendelee kutumikia Jimbo lake kuu la uchaguzi: tumbo lake.

Pamoja na kuwa ni Mgogo, Prof. Pala Kabudi ni Msingida mwenzetu. Bibi yake ni Mnyaturu wa kwetu. Baba na Mama yake ni wazaliwa wa Kilimatinde, na yeye mwenyewe amesomea shule ya msingi mojawapo ya Singida mjini.

Kujikomba na kujidhalili mbele ya Rais Magufuli kumechafua sifa na hadhi ya wasomi wetu kwa ujumla. Kwa sisi Wasingida wenzake, ametushushia heshima yetu sana. Tuna kila sababu na haki ya kumzodoa na kumkanya kwa upumbavu wake huu.
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
29,376
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
29,376 2,000
Profess kabudi katengeneza ajira kwa watanzania nje wakati Yeye Tundu Lisu anazurura na bakuli kuwaomba walioajiriwa wamchangie pesa ya kula,pango,nguo na ada za kusomesha watoto!!! Anayeaibisha hapo? Ni Nani Ni Lisu.Tabia ya kuomba omba sio ya wanyaturu.Lisu ndie omba omba wa kwanza mnyaturu Mimi kumwona toka nizaliwe.Sijawahi kutana na omba omba wa kinyaturu zaidi ya Tundu Lisu
Nafikiri baada ya kuandika na kupost umesoma tena ulichoandika na kugundua ni upumbav mtupu
 
S

Sandinistas

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2013
Messages
1,942
Points
2,000
S

Sandinistas

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2013
1,942 2,000
Nimekuwa nikipata shida kutokana na Prof. Kabudi wa aina mbili niliowafahamu katika siasa za nchi yetu miaka hii ya mfumo wa vyama vingi. Wa kwanza ni Kabudi mhafidhina rafiki wa mahakama ya rufani ya Tanzania kwenye shauri la Mtikila ambapo aliishauri mahakama dhidi ya mgombea binafsi! Wa pili ni Kabudi mwanamageuzi wa Tume ya Katiba Mpya. Lissu ameniongezea ufahamu kukusu Prof. Kabudi.!
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
17,851
Points
2,000
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
17,851 2,000
Mimi siamini kabisa kuwa Prof Assad na huyu wamesoma chuo kimoja
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
29,376
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
29,376 2,000
Sikufahamu kwamba Kabudi aliwahi kuwa mwandishi wa Gazeti la Uhuru .
Lissu anajuwa historia ya nchi hii na watu wake vizuri sana.
Ndio maana akiandika jambo linasimama wima bila konakona.
Hebu tujiulize itakuwa baraka ya kiasi gani nchi hii ikija kuwa na Rais kama Lissu!
 
K

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
440
Points
500
K

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
440 500
ninachofurahi ni Mhe.Lissu kukiri uwezo mkubwa wa kitaaluma na akili aliyonayo Prof. Kabudi, na hili halina ubishi na ninakiri kusema CHADEMA na ACT nzima hakuna mtu anayeweza kusimama mbele ya huyu mzee katika hoja , nasema hakuna.

hata wewe Mhe.Lissu 'tink tank' ya ufipa, umeshupaza shingo kuwa mpumbavu( ni maneno ya Prof Kabudi aliyosema wakati wa tume ya katiba' mpumbavu hushapaa, mjinga hushangaa')?

Jaribu kulipa uzito unaostahili kila neno la Prof. Kabudi na usichukulie ni sawa na maneno ya Mdee au Sugu. Prof. Kabudi alisema baada ya kustaafu alikuwa jalalani kwenye kijiji cha vumbi na hili umekiri mwenyewe alistaafu 2016. labda nikuulize, baada ya kustaafu ulijua ni wapi alipokuwa prof. kabla ya kupewa uwaziri?
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
40,105
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
40,105 2,000
Profess kabudi katengeneza ajira kwa watanzania nje wakati Yeye Tundu Lisu anazurura na bakuli kuwaomba walioajiriwa wamchangie pesa ya kula,pango,nguo na ada za kusomesha watoto!!! Anayeaibisha hapo? Ni Nani Ni Lisu.Tabia ya kuomba omba sio ya wanyaturu.Lisu ndie omba omba wa kwanza mnyaturu Mimi kumwona toka nizaliwe.Sijawahi kutana na omba omba wa kinyaturu zaidi ya Tundu Lisu
Sawa mkuu ila tunaomba kujua ni jalala gani hilo alilotolewa Mh.Palamagamba Kabudi?
 
K

KIM JOHN UN

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2017
Messages
590
Points
1,000
K

KIM JOHN UN

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2017
590 1,000
*Inaandikwa na Mhe Tundu Lissu*

Katika kitabu chake 'Intellectuals at the Hill' (kilichapishwa miaka ya kati ya '90), Prof. Issa G. Shivji aliwahi kusema kuwa kuna tabia ya wasomi wetu kujipendekeza na kujikomba kwa watawala na kufanya mambo ya hovyo kuliko warasimu wa kawaida, hasa wanapopewa vyeo vya uteuzi na Rais.

Prof. Pala Kabudi ni mfano mzuri wa wasomi wa aina hii. Ni mtu ambaye amejipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote ya kitaaluma.

Ukiachia msimamo wake akiwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambao mimi binafsi niliushangaa sana, Prof. Kabudi hana historia yoyote ya msimamo huru katika masuala muhimu ya nchi.

Ana akili za kitaaluma nyingi sana, lakini ana tabia ya kujikomba na kujipendekeza inayotia kinyaa na kufuta sifa zote za usomi wake.

Alitumiwa sana na Serikali ya Jakaya Kikwete na ya Ben Mkapa kabla ya hapo kama consultant wa masuala mbali mbali ya kisheria. Kwa hiyo anahusika kwa kiasi fulani na uchafu wa Kikwete na Mkapa ambao yeye na Magufuli wanajifanya kuukataa sasa.

Alikuwa mwandishi habari wa Uhuru/Mzalendo wakati wa Vita ya Kagera na, aliwahi kutuambia akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya LEAT, alitunukiwa zawadi na Mwalimu Nyerere kwa uandishi wa makala za propaganda zilizokuwa zinahusu Vita hiyo.

Prof. Kabudi amekuwa Chuo Kikuu cha Dar, kama mwanafunzi na kama mwalimu, tangu mwaka '80 hadi alipostaafu mwaka '16. Amekaa Ujerumani na kusomea Frei Universiteit Berlin, mojawapo ya vyuo vikuu maarufu kabisa barani Ulaya na duniani, kwa miaka 9.

Amekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar, na mjumbe wa Tume ya Katiba aliyeteuliwa na Rais Kikwete.

Huyu mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la Anglican, sio mtu aliyezaliwa kwenye vumbi na kuishi kwenye ufukara. Hakutolewa jalalani kokote na Rais Magufuli. Amekuwa na bado ni sehemu ya top elite ya Tanzania.

Alichokisema mbele ya Rais Magufuli sio cha kweli hata kidogo, lakini ni ishara kamili ya hulka yake ya kujidhalili na kujikomba ili aendelee kutumikia Jimbo lake kuu la uchaguzi: tumbo lake.

Pamoja na kuwa ni Mgogo, Prof. Pala Kabudi ni Msingida mwenzetu. Bibi yake ni Mnyaturu wa kwetu. Baba na Mama yake ni wazaliwa wa Kilimatinde, na yeye mwenyewe amesomea shule ya msingi mojawapo ya Singida mjini.

Kujikomba na kujidhalili mbele ya Rais Magufuli kumechafua sifa na hadhi ya wasomi wetu kwa ujumla. Kwa sisi Wasingida wenzake, ametushushia heshima yetu sana. Tuna kila sababu na haki ya kumzodoa na kumkanya kwa upumbavu wake huu.
YULE NI MWANA WA MUHUNZI AMBAE AMEKOSA NAFASI YA KUSANA SASA AMEONA NJIA NZURI KWAKE NI KUFUKUTA
 
M

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Messages
1,930
Points
2,000
M

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2018
1,930 2,000
Kuwa fuatilia wanasiasa ni kazi sana.

Lisu na Kabudi wote ni wale wale, kama ni mbwa wote ni mbwa sema tofauti yao mmoja yupo kwenye nyumba mwingine anaishi na kuokoteza jalalani.
Sio kweli hoja yako
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
18,023
Points
2,000
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
18,023 2,000
By the way, hilo jalala alilolizungumzia ni lipi...!? Uraiani huku mtaani, UDSM au huko Singida............!!? Maana huko Singida kuna vumbi la kufa mtu!!
Kuna mji usiokuwa na vumb Tanzania?
 
kajunjumele

kajunjumele

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2014
Messages
1,813
Points
1,500
kajunjumele

kajunjumele

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2014
1,813 1,500
Kuwa fuatilia wanasiasa ni kazi sana.

Lisu na Kabudi wote ni wale wale, kama ni mbwa wote ni mbwa sema tofauti yao mmoja yupo kwenye nyumba mwingine anaishi na kuokoteza jalalani.
..Hahahaaaaa
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
2,938
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
2,938 2,000
ninachofurahi ni Mhe.Lissu kukiri uwezo mkubwa wa kitaaluma na akili aliyonayo Prof. Kabudi, na hili halina ubishi na ninakiri kusema CHADEMA na ACT nzima hakuna mtu anayeweza kusimama mbele ya huyu mzee katika hoja , nasema hakuna.

hata wewe Mhe.Lissu 'tink tank' ya ufipa, umeshupaza shingo kuwa mpumbavu( ni maneno ya Prof Kabudi aliyosema wakati wa tume ya katiba' mpumbavu hushapaa, mjinga hushangaa')?

Jaribu kulipa uzito unaostahili kila neno la Prof. Kabudi na usichukulie ni sawa na maneno ya Mdee au Sugu. Prof. Kabudi alisema baada ya kustaafu alikuwa jalalani kwenye kijiji cha vumbi na hili umekiri mwenyewe alistaafu 2016. labda nikuulize, baada ya kustaafu ulijua ni wapi alipokuwa prof. kabla ya kupewa uwaziri?
Alikuwa anafundisha chuo kikuu UDSM kwa mkataba, hata yeye alisema kuwa alipata taarifa za uteuzi akiwa katoka kupiga lecture
 
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
2,454
Points
2,000
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
2,454 2,000
Afadhali amempaza USO yaani jitu linajipendekeza bila aibu kabisa limebakiza kidogo tu lianze kumsujudia ,mwenzio Jordan lugimbana alikuwa anamsujudia lakini alitimuliwa .
 
Killmonger

Killmonger

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2015
Messages
1,383
Points
2,000
Killmonger

Killmonger

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2015
1,383 2,000
Daaa huyu professor? Shida ipo wapi.
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
17,851
Points
2,000
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
17,851 2,000
Hii nchi inauwawa kwa mbwembwe.
 
Forum statistics

Threads 1,307,094
Members 502,332
Posts 31,601,544
Top