Tundu Lissu: Paper Tigers wanatushauri tususie chaguzi zijazo ili CCM wapite bila kupingwa

Tundu Lissu the righteousness, brought to this land by Almighty God to guide and teach his fellowmans.
His lips does present the word of God.
 
Mimi sishauri hata mara moja kususia uchaguzi 'under hooks and crooks'. Ni kubanana tu humo humo mpaka kieleweke.

Lakini nimesoma kwa umakini mkubwa taarifa iliyotolewa hapa ili kupata jibu, na sikuliona, wala hata kule kugusia tu sababu zinazofanya matukio yote hayo ya kukanyaga sheria waziwazi kabisa na udhalilishaji kufanywa, lakini wapinzani hawaoni haja ya kwenda mahakamani. Jambo hili silielewi kabisa. Je, kuna siri gani? Ucheleweshaji, au nini!
Je, kuna matatizo gani yanayowazuia kupeleka yote haya mahahakamani? Hata kama mnajua huko pia hakuna haki, lakini kuna shida gani kuyafikisha haya huko ili kuongeza uzito wa ushahidi wanaouona wananchi juu ya kuonewa kwenu? Hebu funua kidogo siri hii kama inawezekana ili tusiendelee kulaumu kwa kutojua.

Vita inakuwa ngumu zaidi unapopigana na adui wa nje anayesaidiwa na unayedhani ni mwezako uliyenae ndani. Vita ya namna hiyo huwezi ukaishinda hata siku moja. 'Malignant cancer' mara nyingi dawa ni kuondoa sehemu inayoliwa kwa haraka. Vinginevyo uhai wa vyama vyenu utapotea, hasa chini ya utawala huu uliojiapiza CCM kutawala milele.
 

Taratibu. Soma na uelewe Tanzania na waTanzania ni watu wa namna gani kabla hujaenda huko. Hivi sasa huyo jamaa, mtesi wenu mkubwa hilo ndilo analolisubiri kwa hamu sana ili awamalize. Msimpe mwanya huo kirahisi hivyo. Kufika huko kunahitaji mikakati ambayo haipo kabisa sasa hivi. Kwa hiyo tuliza kichwa upate njia bora zaidi kuliko hiyo. Njia mbadala zipo.
 
Dawa ya ccm ni kutumia akili ya ziada kuliko ile wanayoifikiria wao.Nasema tena kiboko ya ccm ni Jacob meya wa ubungo awe katibu mkuu utaona mapambano yatakavyo kuwa
Bila katiba mpya na wananchi kuwa tayari kusimamia haki yao..hata kiongozi awe nani hakutakuwa na jipya...ukiniuliza safu sahihi ya uongozi,
Mkiti-Tundu lissu
Mmkiti-John Mnyika
Katibu mkuu-John Heche
Katibu msaidizi-Upendo Peneza
 
Hii tabia ya wasimamizi wa chaguzi zetu ktk ngazi za majimbo na kata kukimbia ofisi zao wakati wa mchakato wa urejeshaji fomu za wagombea hususani wa kutoka vyama vya upinzani yafaa kukomeshwa.
 
Mmmmmh
 
Tundu Lisu na Mbowe ni CCM original...Wako na mkakati wa kuhakikisha wanaiua Chadema
 
Tundu Lisu na Mbowe ni CCM original...Wako na mkakati wa kuhakikisha wanaiua Chadema
Umetimuliwa u DC umerudi tena JF akili za ma ccm hovyo kabisa na hao wanawafanya ccm msilale usiku kucha kiboko ya mkoloni mweusi ccm
 
Keyboard warrior..
..hakuna wa kumchuuza leo aache familia yake yatima akauawe na polisi eti kwa kuamini yuko hatarini.Hizi wishes zenu za kishetani will never come to pass.hakuna misukosuko popote kwenye Tanzania yetu na wewe na wenzio mkianzisha 'misukosuko' you wont take time before you're made extinct!
Tusitishane na kuharibiana amani hapa eti kwasababu kuna watu wamelewa siasa!!!
 
Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu, aliye kwenye matibabu nchini Ubelgiji, akiongea na Mwananchi, amewakoromea kwa mara nyingine Viongozi na wanachama wa CHADEMA wanaotaka kujitoa kwenye Uchaguzi wa Marudio.

Lissu alisema kuwa, "Tulijua Uchaguzi ni vita na vitani kuna kushinda ama kushindwa; kuna kufa ama kujeruhiwa au kutekwa na kuna kuua au kujeruhi au kuteka." Lissu aliongeza kuwa, "Marafiki waliokuja jana na leo asubuhi, wameshuhudia wakipigwa na sasa tayari wanatushauri tunyanyue mikono juu na kusalimu amri mbele ya watesi wetu." Wanatushauri tususie chaguzi zijazo ila CCM ipite bila kupingwa kwenye nafasi zote Nchi nzima."

Aidha, Lissu Alidai kuwa, (marafiki) ... "Wanatumia maneno makali yenye kuonyesha wana msimamo mkali na ujasiri ambao hatujawahi kuona wakiuonyesha kwa vitendo mahali popote."

Tamko hilo la Lissu limekuja wakati Makamu Mwenyekiti, Prof. Safari akiwa amekishauri CHADEMA kususia chaguzi zote nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kudai Tume huru ya Uchaguzi. Hata hivyo, Lissu alikana kuwa tamko lake lilimlenga Prof. Safari kwa kuwa alikuwa hajamsikia.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alifafanua kuwa, CHADEMA inashiriki kwenye Uchaguzi kutokana na wengi kutaka hivyo. "Wapo wanachama wanaodai ukimsusia asiyejali demokrasia kwake ni kicheko."

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…