Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Leo Tarehe 7 Septembre, imetimia miaka 4 kamili tangu Tundu Lissu ashambuliwe na watu wasiojulikana ambao mpaka leo ni miaka 4, bado hawatajulikana.

Shambulio hilo lilifanyika mwezi mmoja na nusu baada ya bandiko hili. Kwa vile hakuna ajuaye sababu za kushambuliwa usikute...

Tumuombee Lissu afya njema na kwenye kuikumbuka siku hii, Mungu amuepushe kupata kitu kinachoitwa "stigimatta"

Pole sana Lissu, survival yako tuu ni muujiza, mwacheni Mungu aitwe Mungu, mengine yote mwachie Mungu.

P.
 
tulikosea Sana kumwamini lissu kuwa anafaa kuwa rais wa nchi ,tulikosea Sana, mwanaharakati,lissu Hana japo chembe ya hekima ,anatukana Kila kitu mtu, siasa haziwezi tulikosea Sana.
Kama hoja hii ni ukweli, then naomba mnisamehe sana, maana, mimi ni miongoni mwa tuliomchagiza Lissu agombee!.
P
 
Kwa jinsi nilivyomsikia Tundu Lissu na namna anavyoongea, then huyu Tundu Lissu ni typical yuko kama Magufuli type tena yeye ni zaidi ya Magufuli!.

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Lisu hana maana kabisa sifa kubwa ni Hasira. huyu jamaa ni magufuli mwingine
Mkuu NTIGAHELA , Hili la Lissu kufanana na JPM, hata mimi niliwahi kulisema humu.
P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Je tumchagize na kushinikiza Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili John P. Magufuli? kwa sababu mpaka sasa, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana uwezo wa kumkabili Magufuli kwa vile uwezo wake ni zaidi ya Magufuli?

Kama kawaida yangu, kwenye kila

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Mayalla yeye tujiulize yeye kayajuaje Mambo ya Chadema wakati sio mwana Chadema kumbuka anayoyajua ndani ya Chadema hua ni Yale mabaya tuu hajawahi ona mazuri hata siku Moja
Mkuu MAPITO Mwanza, jee wajua mimi ni miongoni mwa waliomshauri Lissu agombee?. Hili sio jema?.
P
 
Wanabodi,

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu, kama, Magufuli ameweza kuchaguliwa kihalali na kumshinda Edward Lowassa, kwenye uchaguzi Mkuu huru na wa haki, then you cannot tell about Watanzania huwa wanachagua nini, hivyo Tundu Lissu ambaye ni zaidi ya Magufuli, akisimama na Magufuli, you can never tell what will happen!, Magufuli naweza akaachwa mbali sana! , ila litabaki swali moja tu dogo, with reference ya kilichotokea Zanzibar, hata huku bara, je ikitokea kweli Chadema ikamsimamisha Tundu Lissu na ikatokea Tundu Lissu akishinda, jee atapewa?.

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Huyu mwamba ameingia leo, kwavile ni mimi nilimshauri Tundu Lissu amkabili Magufuli ile 2020, kwa vile 2025 mgombea urais wa CCM ni Mwanamke, hii hamasa kubwa kumpokea Lissu ni kiashiria Lissu anaweza kushawishiwa uchaguzi wa 2025 Lissu amkabili mgombea Mwanamke wa CCM!.

That will be a mistake!. Chadema imuweke Tundu Lissu standby iwapo CCM itasimamisha mgombea mwanamume, then Chadema impitishe Lissu, lakini CCM ikimsimamisha mgombea urais Mwanamke ili kumlindia heshima Lissu na kuepushia kufadhaika kwa kugalagazwa kwa kushindwa na Mwanamke, Chadema nayo iteue na kumsimamisha mgombea Mwanamke maana sio busara kumshindanisha jianadume zima na Mwanamke, kushindwa na Mwanamke ni aibu, ata aibika, atadhalilika, kufedheheka, kutahayari, kunyong'onyea na kusononeka!.

Dear School mate Tundu Lissu, najua umepitia makubwa. Welcome back home. Nakuomba sana upunguze kidogo kuliishi jina lako, usimsumbue huyu Mama kama ulivyomsumbuaga yule Madam, Mwenyekiti wako Mbowe tayari ameisha onyesha uungwana na ustaarabu mkubwa, wa hali ya juu@, please do the same!, tufanye siasa za kiungwana na kistaarabu. Kubebwa bebeka, ukipedwa pendeka, ukishikwa shikamana, ukiaminiwa jiaminishe!.
Yaliyopita si ndwele, samehe, tugange yajayo tusonge mbele!.
Welcome back home.
Your school mate
Pasco
 
Ukweli unaujua kinachopigwa katika box la kura kwa upande wa urais kwa Tanzani bado ni geresha tu , policcm na vyombo vingine rais wanakua nae tayari.

Kama huamini jiulize kwanini CCM hamuitaki tume huru ya uchaguzi kama ile ya hapo jirani Kenya.

Kenya kesi tu ya kura za urais ilisikilizwa kortini huku na wewe ukiwa shabiki na mfatiliaji huku ukisahau kwa Tanzania hiyo haipo je unaona hapo kuna uchaguzi wa urais au ni geresha?

Pasco huyu wa sasa akikutanishwa na Pascal wa enzi zile za kitimoto hakika atamshangaa sana..
 
Maigizo ya uchaguzi na ya wanasiasa yanatosha, tunchokiomba sasa tuangaliye maslahi ya wananchi wengi ambao hawajapta kufaidi rasilimali za nchi yao nao wapate mema ya nchi yao.
 
Huyu mwamba ameingia leo, kwavile ni mimi nilimshauri Tundu Lissu amkabili Magufuli ile 2020, kwa vile 2025 mgombea urais wa CCM ni Mwanamke, hii hamasa kubwa kumpokea Lissu ni kiashiria Lissu anaweza kushawishiwa uchaguzi wa 2025 Lissu amkabili mgombea Mwanamke wa CCM!.

That will be a mistake!. Chadema imuweke Tundu Lissu standby iwapo CCM itasimamisha mgombea mwanamume, then Chadema impitishe Lissu, lakini CCM ikimsimamisha mgombea urais Mwanamke ili kumlindia heshima Lissu na kuepushia kufadhaika kwa kugalagazwa kwa kushindwa na Mwanamke, Chadema nayo iteue na kumsimamisha mgombea Mwanamke maana sio busara kumshindanisha jianadume zima na Mwanamke, kushindwa na Mwanamke ni aibu, ata aibika, atadhalilika, kufedheheka, kutahayari, kunyong'onyea na kusononeka!.

Dear School mate Tundu Lissu, najua umepitia makubwa. Welcome back home. Nakuomba sana upunguze kidogo kuliishi jina lako, usimsumbue huyu Mama kama ulivyomsumbuaga yule Madam, Mwenyekiti wako Mbowe tayari ameisha onyesha uungwana na ustaarabu mkubwa, wa hali ya juu@, please do the same!, tufanye siasa za kiungwana na kistaarabu. Kubebwa bebeka, ukipedwa pendeka, ukishikwa shikamana, ukiaminiwa jiaminishe!.
Yaliyopita si ndwele, samehe, tugange yajayo tusonge mbele!.
Welcome back home.
Your school mate
Pasco
Umezeeka vibaya,hivi kwa umri wako hujawahi kujua kuwa CCM wanaiba kura za Urais,ubunge na madiwani. Ashindane kwa tume ipi ya uchaguzi,sisi wa juzi tumejionea watendaji wa serikali na vyombo vya usalama vikipora mabox ya Kura eti wameelekezwa bila hivo kazi hawana. Alfu wewe na uzee wako unaropoka ni vema ujielekeze kuishauri CCM ikubali katiba Mpya kwa Nini inaiogopa,We ni Mnafiki na kwa akili hizo hupaswi kushauri chochote.
 
One cannot steal from himself, Tanzania ni mali ya CCM, hivyo CCM haiwezi kuiba chochote bali ni inachukua tuu!.
P
 
Back
Top Bottom