Tundu Lissu, Nchimbi wawapatanisha Mr Sugu na Ruge wa Clouds FM

Hatimaye mbunge wa mbeya mjini Joseph mbilinyi amemaliza tofauti zake na mkurugenzi wa clouds fm Ruge mutahaba,wameweka tofauti zao chini na kuamua kuanza kuwa kitu kimoja katika tasnia ya music,kikao hicho kilikua kikiongozwa na waziri wa habari na michezo Dr.Nchimbi na Mbunge Tundu Lisu
 
safi sana Mh Sugu,Hii ni kwa faida ya sanaa,faida ya mziki na faida kwa vijana wote

Hongera kwa hilo
 
Tuambieni walichokubaliana kabla hatujahukumu,wanaosikiliza Clouds live!
 
huu mjadala unamsaisiaje mtanzania wa kawaida?? hapa sio mahala pake maana sio tukio la kisiasa hili ni jukwa la siasa!!
 
nadhani ruge ameona anakula loss imebidi amtafute sugu wayamalize

Sugt ndo aliyemuomba Waziri Nchimbi awapatanishe..Muhimu wasiwe wamemaliza tofauti zao kinafiki.
Kwa hy kuanzia leo tunaanza kuwasikia vinega tena Clouds..siku hz mbili tatu watapata promo ya kutosha
 
Nchimbi kasema akiwa bungeni baada ya hotuba yake ya bajeti, alilizungumzi bifu la Sugu dhidi ya Clouds. Ndipo Sugu akalimimina kwenye hotuba yake kama Waziri Kivuli. Baada ya kikao Sugu alimfata Nchimbi na kumfafanulia. Ndipo Nchimbi akakubali kujitolea usuluhishi na leo amefanikiwa kuwakutanisha na kumaliza tofauti zao.
 
Ruge alipozungumza alianza kwa kumshukuru Nchimbi kuwakutanisha na kumshukuru Sugu kukubali mapatano na kusema wao na Sugu wote ni vijana na wanacomand ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya hivyo kupatana kwao ni maendeleo ya muziki huo!.
 
Muziki una mchango wowote kwa pato la taifa? Sijaona bado kama kuna mwanamuziki wetu analeta fedha ya maana kutoka nchi jirani, sana sana tunanyang'anyana humu humu na kuwaalika wakina Kidumu et al kuja kuchuma!
 
Back
Top Bottom