Tundu Lissu na Aboud Jumbe

Nitakupinga wewe hadi ........ kwa kuwa wewe ni mchochezi na mnafiki.
 
Karume senior kauawa kwa umajununi wake, wala si habari za siasa.

Kamuua baba yake Humudi halafu kampa Humudi cheo kwenye intelligentsia.

Humudi akampigilia risasi mbali kwenye kikao cha bao.
Sii wengi wanaozungumzia sababu ya Karume kumuua baba yake Humudi, ila habari zisizothibitishwa zinaeleza kuwa Baba yake Hamud ni asili ya Kiarabu, Karume akamhitaji binti yake aolewe kinguvu na mmatumbi, Baba Mtu akagoma, Karume akamuua Baba na kumtwaa binti kinguvu, akamuoa, akamzalisha kisha kumtelekeza!,hivyo Hamudi alikuwa ni shemeji yake Karume!.

Niliwahi kusikia mama mmoja akihojiwa Clouds alijitaja yeye ni mke wa rais, niliuliza humu, [h=3]Mke wa "President"Ashiriki Shindano Clouds!.[/h]Wanzanzibar, hawakujibu chochote.

Baadaye nikasoma mahali humu humu jf kuwa Karume alikuwa na wake 6!, nikauliza humu [h=3]Je, Abedi Amani Karume alikuwa na Wake 6?!, sikujibiwa!.[/h]Pasco
 
Kwa kuwa hajaanza kuwashughulikia tunaomba elimu yako
Mimi nimesoma sana mpaka nimefika darasa la 7 enzi za UPE, nilipasi ila sikuchaguliwa kuendelea fomu wani, hivyo nikaishia daasa la saba!, na hiki ndicho kiwango halali cha elimu kwa Tanzania!.
Pasco
 

we unachekesha kama kweli hajawekews vikwazo kigamboni ndiko alikozaliwa? amekwenda kuishi pale kwa matakwa yake. Acha fikira mgando
 

Kama hivyo ndivyo ilikuwaje baada ya kupigwa risasi wanajeshi waliokuja kuuondoa mwili wake ni wale waliopaswa kuwa huku bara? Walitoka wapi kule unguja kwenye tukio hilo?
 

kumjadili kichaa ni zaidi ya uchizi.
 
Last edited by a moderator:
Kama hivyo ndivyo ilikuwaje baada ya kupigwa risasi wanajeshi waliokuja kuuondoa mwili wake ni wale waliopaswa kuwa huku bara? Walitoka wapi kule unguja kwenye tukio hilo?

Habari hiyo umeipata wapi na ina uhakiki gani?

Isitoshe, hata ikiwa kweli siwezi kushangaa, kwani Zanzibar haina jeshi, moja ya sababu iliyomfanya Karume akubali kirahisi sana muungano na bara. Na Karume hakuiamini sana intelligentsia ya usalama ya Zanzibar, ambayo.ndiyo hiyo ya kina Mahfudh / Humudi. Ilijaa makomredi waliosoma nchi za kikomunisti ambao walimuina Karume kama dikteta ambaye si msomi na hafai kuwa rais.

Kwa hiyo siwezi kushangaa kama wanajeshi wa bara walitumika in a forensic way, kupreserve evidence etc. Kwa sababu wa Zanzibar ndio hao waliomuua na hawakuaminika.

Zanzibar inategemea strategic military support kutoka bara mpaka kesho.

That's why unakuta watu kama kina Brigedia Mwakanjuki wamelowea huko miaka na miaka.
 

Mkuu issue yenyewe ni kwamba: Abdul Jumbe wakati Yuko madarakani, kama Rais wa Zanzibar na makamu wa rais ya Tanzania, alichapisha pesa, bendera za serikari ya mapinduzi Zanzibar, kisha akaenda UK akamwambia waziri mkuu Kuwa Tanzania bara inampango wa kuivamia Zanzibar na kuikalia kwa nguvu akaomba na msaada! Waziri akamuahidi kutuma jeshi kama itatokea kama ilivyofanya UK jeshi letu lilipoasi,
Aliporudi huku akamwambia Ml. Nyerere Kuwa kuna fununu kuna jeshi linataka kuivamia Zanzibar! Inahitaji ulinzi, Nyerere akatuma jeshi na vifaru Zanzibar kwa ulinzi,
Baada ya majeshi kujipanga Jumbe akapiga simu kwa Waziri mkuu wa UK Kuwa Yale aliyomwambia yametimia, UK haikufanya pupa, PM akampigia simu Nyerere kumuuliza sababu ya kuivamia Zanzibar na kuikalia kwa mabavu, Nyerere akashanga ndiyo ilibidi wakutanishwe ukweli ujulikane, ndiyo Jumbe akaonekana mchonganishi, kwa heshima yake akaombwa ajiuzuru na kukaa pembeni, Seif S Hamad alikuwa anauma huku na kule kwa lengo la kuchukua madaraka ya Jumbe ndiyo Rungu likamwangukia, na Urais wa Zanzibar ukamwangukia Alli Hassan Mwinyi kwa kipindi mpaka uchaguzi baada ya hapo akagombea bara na hatimae Kuwa rais wa Tanzania,
Kama mlisikia machafuko ya Zanzibar ndiyo hayo, hata UK wanalijua lililomwondoa Jumbe na kumuweka pembeni kisiasa.
 

umeingilia suna za mtume!
 
Umeandika kiudaku udaku sana ingawa ujumbe umefika. Hii historia imeandikwa wapi?

Kabisa siyo kiudaku hiyo inaeleweka kwa wale wazanzibari wenye age kama yangu ambao walikuwa part ya hiyo historia (nilikuwa form two). Scenarios za Humudi kumuua father K zilikuwa zinaelezwa kwenye ile kesi ya uhaini ambayo ilichukuwa muda mrefu na TVZ ilikuwa inaitangaza kila siku (of course siyo live).

Baba yake Humudi alimuua aliyekuwa Chief Inspector wa Polisi Zanzibar (nadhani sawa na IGP) kutokana na kupingana katika siasa. Jina lake akiitwa Sultan Ahmed Mugheir. Wakati ule wa ukoloni wa muingereza yule mzee alionekana kutokuwa na hatia (sina uhakika wa sababu kamili zilizomfanya asamehewe). Baada ya Mapinduzi father K akafufua kesi ile na baba yake Humudi akahukumiwa kifo. Na hapo ndipo issue ya kulipiza kisasi ilipoanza.

Na stori yake ndefu ilitoka kwenye gazeti la drum (enzi zileeee) mimi mwenyewe niliisoma na hata picha zake na familia yake zilitolewa.
 

Mkuu hii umeitoa wapi?
 
Kama hivyo ndivyo ilikuwaje baada ya kupigwa risasi wanajeshi waliokuja kuuondoa mwili wake ni wale waliopaswa kuwa huku bara? Walitoka wapi kule unguja kwenye tukio hilo?

Waliokuwa bara wapi na ni akina Ali Mahfudh ndiyo waliosimamia kuondoa mwili wa Humudi? I wish zile cassettes za ile kesi zingehifadhiwa maana pale waliongelea mambo mengi sana wakati wa mahojiano.
 

Sababu za Humudi kumuua father K nimeeleza hapo juu.

Kuhusu wake zake kwa ninaowakumbuka mimi ni kama wafuatao:
1. Fatma Karume mama yao Amani na Ali
2. Moza Nassor (marehemu) kutoka Ole Pemba (muarabu na hakubahatika kupata mtoto)
3. Nasreen (muhindi ithnasheri) wa Unguja mama yake Ahsa Karume
4. Fadya (muarabu) wa Unguja mama yake Asha Karume
5. Helemu (muarabu) wa Wete Pemba mama yake Ahadi Karume.

Inasemekana huyu first lady alikuwa tayari amepewa talaka ila hakuna uthibitisho.
 
"Kama kuna watu wanasema kuwa Zanzibar sio nchi, basi wasiishie hapo. Waeleze jee Zanzibar ni Mkoa, au ni Wilaya, au ni kijiji au ni kitongoji?" by Seif Sharif Hamad ... Huyu Jamaa kwa kurusha Ngumi Jiwe ni Hodari kweli kweli ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…