Tundu Lissu: Madini mengine ya Tanzania si yetu Kisheria

Duh Mambo ya Wabunge wa Ccm Kila Kitu Kusema Ndiyoooooo.....!!!
Hayo Ndiyo Madhara Yake.
... Hahaaa, inanikumbusha enzi zake bibi kule mjengoni anawahoji.. '' wanaoafiki waseme NDIOOO nao kwa uwingi wao wanadakia Ndiyoooo tumeliwaa...
 
Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.

Sasa hapo unamlaumu Lissu kwa lipi wakati mlipiga meza na kusema ndioooooooooo ipite kwa umbumbumbu wenu.
Lissu akitaka kusaidia JPM hatakubali maana atadhani kuwa Lissu anapata population ya watanzania
 
"Tunachukua mchanga,tunasafirisha mpaka nchi nyingine ya mahali fulani.Eti wakachambue,wakatoe dhahabu iliyomo,na titarium na vanadium na nini... Wanavichambua huko na mchanga wanabaki nao hukohuko wanakwambia hatukupata kitu, sasa ni marufuku kusafirisha mchanga.kama ni kusafirisha tuulete hata hapa,tujenge kiwanda cha kuchuja,tutakuwa tunaona kuliko kupeleka nje,nataka kwenye utawala wangu hakuna mchanga utakaokwenda nje kusafishwa,wajenge viwanda hapa,vijana wapate ajira hapa,wasafishie madini hapa,tutajua zinc ni kiasi gani,copper kiasi gani,Tanzania tupate pesa,tumechezewa vya kutosha.Hiyo ndio tanzania ninayoitaka"

MY TAKE

Tunataka Rais wa aina gani?kwa hiyo Lissu anataka hali hii iendelee?kamati ya uchunguzi itafanya kazi,tutajua tufanye nini kukabiliana na mikataba mibovu tuliyoingia baada ya kupokea ripoti ya tume,mambo mazuri yanakuja.
 
Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.
... Tayari amesaidia kutukumbusha kwamba tatizo siyo kukata matawi ya Mti bali kung'oa na mizizi!!! Hivyo serikali haraka ipeleke muswaada wa kurekebisha hiyo Sheria mbaya aliyosema Lissu, tena waipeleke kwa dharura kama ilivyo kuwa ule muswaada wa habari...
 
hiyo ni njaa muulizeni amewahi kusupport jambo gani la serikali? huo ni upinzani wa kizamani badilika.
Mijitu mingine hata haieleweki.kama unamapenzi na nchi yako bado unachotakiwa siyo kulaumu bali nikutoa ushauri tuokoe hicho kilichobaki na siyo kulalamika na kulaum waliopita.pley your part!

Amesha PLEY sehemu yake mkuu... Alichofanya Lisu nafikiri ni jambo jema... Hakutoa ushauri ila ni maelezo.
Ulitaka ushauri ampe nani? Serikali eeh!! ... Mkuu wa Serikali ni nani? Huna sababu ya kujibu

Ila jiulize huyo mkuu anahitaji ushauri.. Kwani Lisu alisaidia kuchukua form??
 
Zinavunjwa ndoa sembuse mikataba!
Usilinganishe ndoa na mikataba. Mikataba ina kipengele cha namna gani ya kuvunjwa. Mikataba ina vipengele vya namna ya kusuluhisha migogoro au kutokuelewana kunapotokea mkiwa ndani ya mkataba. Mikataba ina vipengele vya wapi mpeleke kesi yenu endapo mnashindwa wenyewe kuelewana na kama mmoja wenu amekiuka mkataba. Mkataba sio ndoa, pale hakuna anayeoa wala kuolewa.
 
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia sakata la makontena ya mchanga unaodaiwa kuwa na madini uliozuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, akisema madini mengine yaliyomo humo siyo mali ya Tanzania.

Lissu amesema kwa maoni yake Serikali haipaswi kuzuia madini hayo kusafirishwa kwenda nje kwa kuwa ni kukiuka mikataba na sheria ya madini.

“Hili halizungumzwi kabisa na liko katika mikataba. Madini mengine si yetu kwa sababu haihesabiwi katika asilimia mia ya dhahabu,” amesema mwanasheria huyo wa kujitegemea alipotembelea ofisi za Mwananchi.

Mbunge huyo amesema kwamba, kwa hoja za kodi Taifa halina chake katika suala la madini, isipokuwa ni asilimia nne ya pato inayolipwa na mwekezaji kama mrahaba kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 1998.

Lissu ameongeza kuwa sheria hiyo inampa mamlaka mwekezaji kuwa, iwapo anapatiwa leseni ya uchimbaji kile anachopata ardhini kinakuwa ni mali yake.

“Haki yetu ni asilimia nne tu ya mirabaha. Kwa kifupi, kwenye madini tumewapa (wawekezaji) madini bure, tena kisheria,” amesema.

Mwanasiasa huyo amesema anashangaa kuona mchanga unazuiwa bandarini wakati Rais John Magufuli alikuwa katika Baraza la Mawaziri wakati Sheria ya Madini ya mwaka 1998 na 2010 zikipitishwa.


Chanzo: Mwananchi


Raisi anachochukia ndio hiki: Mtu unalalamika tena mwanasheria, Unalalamika tuuu....Toa suluhisho, Shauri nini kifanyike kisheria ukiwa kama wewe ni Mtanzania na unaipenda nchi yako...

Hata mimi nachukia sana watu wanaolalamika km wameachwa...
Kulalamika hakusaidiii...bali SOLUTION ndio inayosaidia.
 
Lissu wacha mambo ya kijinga, mbona GGM wanalipa corporate tax! Na hiyo 4% kwanza sio kodi ni kishika uchumba kama mahari.

Huwezi sema umetoa mahari basi umemaliza, utaendelea kutoa vingine na vingine.

Wanasema walitaka kuuza mgodi kwa 4bilioni hebu tuwalipe hiyo pesa wasepe watuachie tuchimbe wenyewe kama stamigold.
Utakula jeuri yako....
 
Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.

Tatizo husomi Magazeti, alitoa ushauri wa kujitoa kwenye soko na mikataba ya kimataifa ihusuyo madini na kuandika upya mikataba yote.

Unataka afanye nini??Tena alieleza vyema kutoka kisheria na akatolea mfano wa nchi iliyofanya hivyo.
 
Madini yote yetu kisheria, maanake sheria inapingwa kwa vifungu vidogo vidogo vya sheria

ila ki ukweli madini yote ni mali yetu kwa sababu yamechimbwa kwenye ardhi yetu
 
Back
Top Bottom