Tundu Lissu: Madini mengine ya Tanzania si yetu Kisheria

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia sakata la makontena ya mchanga unaodaiwa kuwa na madini uliozuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, akisema madini mengine yaliyomo humo siyo mali ya Tanzania.

Lissu amesema kwa maoni yake Serikali haipaswi kuzuia madini hayo kusafirishwa kwenda nje kwa kuwa ni kukiuka mikataba na sheria ya madini.

“Hili halizungumzwi kabisa na liko katika mikataba. Madini mengine si yetu kwa sababu haihesabiwi katika asilimia mia ya dhahabu,” amesema mwanasheria huyo wa kujitegemea alipotembelea ofisi za Mwananchi.

Mbunge huyo amesema kwamba, kwa hoja za kodi Taifa halina chake katika suala la madini, isipokuwa ni asilimia nne ya pato inayolipwa na mwekezaji kama mrahaba kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 1998.

Lissu ameongeza kuwa sheria hiyo inampa mamlaka mwekezaji kuwa, iwapo anapatiwa leseni ya uchimbaji kile anachopata ardhini kinakuwa ni mali yake.

“Haki yetu ni asilimia nne tu ya mirabaha. Kwa kifupi, kwenye madini tumewapa (wawekezaji) madini bure, tena kisheria,” amesema.

Mwanasiasa huyo amesema anashangaa kuona mchanga unazuiwa bandarini wakati Rais John Magufuli alikuwa katika Baraza la Mawaziri wakati Sheria ya Madini ya mwaka 1998 na 2010 zikipitishwa.


Chanzo: Mwananchi
 
Wakienda mahakamani, tutaanza kuwalipa kama IPTL, mambo mengine niyakujitakia...

Hii sekta waachane nayo tu, itawashinda...maana ilikuirekebisha inabidi makaburi yafukuliwe na mikataba yote iweke wazi na irekebishwe. Ila ndo hivyo tena, Rais kashasema hafukui makaburi...
 
Huu mchanga utatutokea puani. Tutaingizwa gharama za ajabu. Kama makosa tuliyofanya kwa njia ya mikataba ya kisheria huko nyuma yanaweza kuzuiwa na agizo la raisi kwa nini raisi asianze na zile nyumba za serikali zilizouzwa kwa bei ya kutupa na kuliingizia taifa hasara? Ni lazima tuanzie kwa wawekezaji?
 
Mkuu mbna unakuwa kichwa maji?

Ushaambiwa sheria ya madin ishasainiwa toka 1998 na maguful akikuwapo kwenye baraza la mawaziri na Tanzania hupata 4% tu

Sasa Unataka lissu avunje mkataba?

Ccm mkiwa mnatunga sheria mnajifungia kwenye mahekalu yenu

Yakiwashinda mnatoa macho mnanifanya kuwapenda wananchi

Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.
 
Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.
mbona kashindwa kutoa hata maoni ya nini kifanyike?
angeombwa atoe msaada nafikiri isingekuwa tabu!
Mbaya zaidi ambao wanahitaji msaada ndio wanaotamani hata apotee!
Kila siku anakamatwa kwa makosa ya kijinga hata tukiwa mimi na wewe nafikiri inafika mahali nyongo inachafuka
 
Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.
Yeye anajitahidi sana kutetea nakutoa ufafanuzi bungeni lakini kwasababu bunge linazidiwa na uwingi wa wanaCCM,anashindwa.Ngoja Magu aone impact ya NDIYOOO.... ya CCM hapa anapotaka pesa wakati sheria inampinga.
 
Lissu wewe ni kichwa.
Unalizika taifa kupolwa?
Wewe Kama nguli wa Sheri's Una lisaidiaje taifa katiba dhahama hii?
Kama huwezi Huna maana hats kidogo.

ww kila siku tunapiga kelele kuhusu mikataba ya madini kupekekwa bungeni ifahamike inasemaje. Lakini serekali ya wezi inagoma kwa kusema mikataba ni siri. Wabunge wengi hasa wa upinzani hawajui kwa kina mikataba inasema nini zaidi ya kile wanachoambiwa na serekali. Hiyo mikataba imejadiliwa na mawaziri Magufuli akiwa ndani, alichukua hatua gani kuonyesha hakubaliani na hiyo mikataba? Jiongeze boss
 
Mbunge huyo amesema kwamba, kwa hoja za kodi Taifa halina chake katika suala la madini, isipokuwa ni asilimia nne ya pato inayolipwa na mwekezaji kama mrahaba kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 1998.
Sheria inayotumika ni Sheria ya Madini 2010 hii ya 1998 haipo.

4% Ni Royalty
Aongeze Income tax, humo mbona anakua hayuko updated
 
Back
Top Bottom