Tundu Lissu kurejea nchini

Tundu Lissu kurejea nchini

Kuna mtu anajinyea huko, Hahaha. Huyu kapewa talanta yake pekee, huwa akiongea kitu popo wote wanaweweseka mapangoni. Welcome back Komredi.
 
Ana beep na kujipigia yeye mwenyewe. Hatuna haja na siasa zake. Nchi imetulia tangu aondoke . Bora wakae huko huko.
Nchi imetulia??, wanasiasa wa vyama vingine kisiasa kila siku wako mahakani,raia wanabambikiwa kesi kila siku,polisi wamepewa nguvu kupita kiasi,polisi wanaweza kumfanyia chochote raia,Nchi imekuwa "police state" ,halafu unasema nchi imetulia,....sisi raia wa kawaida tunaona nchi imekuwa ya kifashist...
 
Hawezi kubaki ughaibuni......

Hata Mzee Mandela angeweza kubaki Tanzania kule Mazimbu Morogoro, wakati ule wa mapambano ya ukaburu kule Afrika Kusini, lakini aliamua kijasiri kurejea Afrika Kusini na Mahakama za kikaburu zikamuhukumu kifungo cha maisha jela.....

Akakaa Jela miaka 28 na hatimaye Makaburu wa Afrika Kusini wakaona bora yaishe na wakamtoa gerezani na akawa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuwa Rais wa Afrika Kusini na amekuwa ndiye "celebrity" maarufu zaidi duniani katika karne ya 20
Makaburu wazungu,waafrika maamuzi yao ni kupiga au kuuwa,Lissu bora angelibaki huko huko..nchi haina sheria hii,utawala wa sheria hajulikani,"full dictatorship"...
 
Kwa watu wa makamo watakumbuka jina la Oscar Kambona aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU enzi hizo. Alifungasha mizigo yake na kwenda kuishi Uingereza kwa miaka kadhaa. Baadaye kwa kupima upepo akatangaza anataka kurudi Tanzania. Mwalimu alipoulizwa kuhusu hilo akajibu kwamba Oscar hakuniaga wakati anaondoka. Sasa anasema anataka kurudi muulizeni yeye. Mimi hakuniuliza mawazo yangu kama arudi au la. Muda si muda kweli akarudi na kuanzisha chama cha upinzani. Akaitisha mkutano wa waandishi wa habari atangaze hadharani namba za akaunti za benki za Mwalimu na Rashidi Kawawa. Mkutano ukaendelea kwa masaa na kila wakati waandishi wa habari wanamkumbusha suala la akaunti. Hakuna akaunti yo yote iliyotajwa. Ilikuwa ni uzushi tu. Baada ya hapo akaugua na kufa na chama chake kikafia mbali. Tuone na Lisu mambo yatakuwaje.

Kwa kifupi unaiambia duniani kuwa Lissu akirudi mtamuua, haya tumewasikia.
 
Makaburu wazungu,waafrika maamuzi yao ni kupiga au kuuwa,Lissu bora angelibaki huko huko..nchi haina sheria hii,utawala wa sheria hajulikani,"full dictatorship"...
Yeye mwenyewe anajua kuwa anawindwa.....

Dunia nzima hivi sasa inajua anawindwa......

Yeye mwenyewe kwa kauli yake amesema atarudi.....

Halafu mfanye tena jaribio la kumuua.......

Ndipo muijue dunia itareact vipi!

Hivyo viti vya madaraka mnavyovimiki sasa mtaviona vya moto!
 
Jiwe akisikia hivyo homa inampanda anaogopa lissu anaweza kuwataja makonda na genge lake
Wengi wanashinda kwa waganga wa kienyeji mda wote wakiamini pengine watafanikiwa kukwepa kutajwa live.
 
Back
Top Bottom