Tundu Lissu kurejea nchini

Tundu Lissu kurejea nchini

Le mutuz yupo kwa mganga wa kienyeji tokea juzi akinahaha maana anajua Lisu akirejea atawataja wote walitumwa Dodoma kwenda kumpiga Risasi

le mutuz kaishiwa nguvu baada ya bwana philipo ''inzagi'' mpango kuwaharibia deal lao. wamepakia kuandika kitabu ili kujifariji.
 
Safari hii sijui watamnunua? Subutuuu!
Lakini ya Mungu 'Mengi'
 
Wenye jukumu la kumthibitisha kuwa ni msaliti ni chombo cha Mahakama pekee...

Sasa nyinyi mnawezaje kujitwalia jukumu la Mahakama na kutaka kuondoa maisha yake??
Mwenye jukumu la kudhibitisha usaliti wake sio mahakama bali ni nafsi yake mwenyewe. KILA MJA NI SHAHIDI WA NAFSI YAKE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chonde sirikali, mtuache huru siku hiyo tumpokee shujaa wetu. kutuzuia kumpokea itatufanya tuwaelewe vibaya kwa kweli!
 
Kutokana na taarifa iliyotolewa asubuhi hii na shirika la utangazaji la BBC, amenukuliwa mwanasiasa maarufu wa Chama cha Chadema, Tundu Lissu, akisema kuwa hivi sasa ameshatoka hospitalini na anatarajia kurejea nchini wakati wowote kuanzia sasa

Ikumbukwe kuwa Tundu Lissu alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi zisizopungua 30, mwezi September mwaka jana huko jijini Dodoma na watu wasiojulikana

Amekuwa akitibiwa nje ya nchi jijini Nairobi na baadaye nchini Ubelgiji kwa takribani miezi 11 hivi sasa

Alipoulizwa na mtangazaji Zuhura Yunus, kuhusu usalama wake akirejea nchini Tanzania kwa sasa, mwanasiasa huyo alijibu kuwa ni kweli analazimika kuchukua tahadhari kubwa sana ya usalama wake atakaporejea nchini kwa kuwa wale waliotaka kumwua hadi leo hawajapatikana

Akiongelea hali ya kisiasa hapa nchini, alijibu kuwa wapinzani nchini Tanzania, hususani wa chama cha Chadema, kwa sasa wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana ambayo hayajawahi kutokea tangu turejee katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kwa kuwa viongozi wakuu wote wa Chadema wanasumbuliwa na kesi zisizo kuwa na mwisho karibu kila siku katika Mahakama zetu nchini, ambapo inawapa wakati mgumu sana kuwatumikia wananchi wao waliowachagua katika majimbo yao

Mwenyezi Mungu mjalie na umkinge na watesi wake Tundu Lissu, ambaye ndiye shujaa wa kisiasa nchini Tanzania hivi sasa
Jiwe akisikia hivyo homa inampanda anaogopa lissu anaweza kuwataja makonda na genge lake
 
Kwa watu wa makamo watakumbuka jina la Oscar Kambona aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU enzi hizo. Alifungasha mizigo yake na kwenda kuishi Uingereza kwa miaka kadhaa. Baadaye kwa kupima upepo akatangaza anataka kurudi Tanzania. Mwalimu alipoulizwa kuhusu hilo akajibu kwamba Oscar hakuniaga wakati anaondoka. Sasa anasema anataka kurudi muulizeni yeye. Mimi hakuniuliza mawazo yangu kama arudi au la. Muda si muda kweli akarudi na kuanzisha chama cha upinzani. Akaitisha mkutano wa waandishi wa habari atangaze hadharani namba za akaunti za benki za Mwalimu na Rashidi Kawawa. Mkutano ukaendelea kwa masaa na kila wakati waandishi wa habari wanamkumbusha suala la akaunti. Hakuna akaunti yo yote iliyotajwa. Ilikuwa ni uzushi tu. Baada ya hapo akaugua na kufa na chama chake kikafia mbali. Tuone na Lisu mambo yatakuwaje.
 
Back
Top Bottom