Tundu Lissu kama ipo ipo tu, usitulazimishe!

Tundu Lissu kama ipo ipo tu, usitulazimishe!

Tundulisu si wa chama chako wee inakuuma nn? Anatuaminisha sisi na sisi tunamkubali ili usiumie dawa ni kuttomfuatilia akili ya kupauka haiwezi kumuelewa
 
Haka kajamaa kanatutisha eti tutashitakiwa. Vizuri wazungu haohao anaowaogopa wamemuumbua mchana kweupee.
 
Kama wewe ni Kiongozi mzuri na una damu ya kupendwa utapendwa tu, hauna haja kulazimisha watu wakukubali na wala hauhitaji kujitetea kwa chochote, namuongelea Tundu Lisu, he's is all over kutaka kujiuza na kulazimisha Watanzania wamkubali, Magufuli alienda kuchukuwa Fomu ya Uraisi peke yake na kuzunguka nchi nzima kutafuta Wadhamini yeye na gari lake, leo hii ni Raisi wa JMTZ,, Waswahili tunasema kama ipo ipo tu, kama watu wanakukubali na kukupenda watakupenda tu wala huhitaji kutumia nguvu, ...

Sijaelewa unachowasilisha. Uwasilishaji wa hoja una skills zake na siyo kuweka weka tu maneno pamoja.
 
Ukikua kiakili utaacha
Saizi bado unaviroba kichwani!
Mtu mwenye utimamu hawezi muunga mkono lisu kwa ujinga wake anao ufanya kwa sasa.
Pole sana.Naona umeshahitimisha kuwa anayemuunga mkono Lissu hana akili timamu. Nakuuliza:

Kulazimisha kila MTU afikiri,anene na atende utakavyo wewe ni utimamu?

Ingekuwa hivyo sisi tuliozaliwa karne baada ya gharika (kwa wanaoamini) tungekuwepo?

Kama Muumba anavumilia wote wanaomkiri na kinyume chake hafanyi wala kutoa maamuzi hayo kiumbe mwingine tu iweje ajitweze zaidi?

Zaidi ni umbumbumbu wa kupindukia kujiona kuwa ni mjuvi na muweza kuliko wengine.

Kama binadamu,kila mmoja ana mapungufu yake.Tuyatumie hayo kujisahihisha ili tupate suluhu ya vikwazo hivyo kwa pamoja. Kuzuia mawazo ya tusiopendezwa nao haitasaidia zaidi ya kuchochea mgawanyiko.

Na hakuna sehemu/nchi yenye watu wenye mawazo ya " kuunga" mkono kila lisemwalo na "mtawala!". Vinginevyo tutaishia kuumizana tu.
 
Back
Top Bottom