Kama wewe ni Kiongozi mzuri na una damu ya kupendwa utapendwa tu, hauna haja kulazimisha watu wakukubali na wala hauhitaji kujitetea kwa chochote, namuongelea Tundu Lisu, he's is all over kutaka kujiuza na kulazimisha Watanzania wamkubali, Magufuli alienda kuchukuwa Fomu ya Uraisi peke yake na kuzunguka nchi nzima kutafuta Wadhamini yeye na gari lake, leo hii ni Raisi wa JMTZ,, Waswahili tunasema kama ipo ipo tu, kama watu wanakukubali na kukupenda watakupenda tu wala huhitaji kutumia nguvu, ...
Mimi sioni kama Tundu Lisu anajiuza au kutumia nguvu! Wewe unatumia nguvu ili sisi tuamini hivyo na tukubaliane na wewe! Siyo lazima wewe au mtu yeyote akubaliane na Lisu, na siyo lazima sisi tukubaliane na wewe au ccm. Watanzania twapaswa kujifunza kuwa huru kutoa mawazo binafsi hata kama yanapingamana na mwingine.
Tatizo letu hatuna constructive arguments, na hiyo husababisha wabunge kuzomeana na kutolewa nje kama mbwa au majizi. Watanzania hatuna hile culture ya to agree to disagree. Ndiyo maana mtu akikupinga basi amekuwa adui. Kwa kweli, niwapumbavu sana! Tazama bunge la waliotutawala, Waingereza! Mara nyingi wanajadili mambo kwa uwazi bila kunyanyasana au speaker kupendelea, wakimaliza bunge marafiki!
Tanzania bado sana. Magufuli will never succeed kwa kubana uhuru wa opposition parties, kubana press freedom, kuto kuleta katiba mpya, na kuto introduce social welfare service kwa wazee na mama wenye watoto. Pia, bila kuwa empower wakina mama nchi haiwezi simama imara. Mark my word today utakumbuka nilichokiandika.
Mwisho, nchi haiwezi progress bila mwanamke au mama zetu. Swala la mama zetu nchi nyingi za Africa hazitilii uzito. Ulaya mwanamke ndiye mwenye power kwa sababu yeye ndiye analea watoto. Kwahiyo, mwanaume hata kama nyumba ni ya kwako alafu unamuacha au mwanamke hakutaki, wakuondoka kwenye nyumba ni mwanaume. Kama tutakuwa na culture hiyo Tanzania itakuwa nchi babukubwa.
Kwa kuongezea, Huwepo wa Chadema, upinzani na Tundu Lisu ni muhimu sana katika nchi ili kukosoa, of course, constructively for the benefit of the country. Sasa tuwache kuona kama Lisu ni adui wa nchi.