Pakawa
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 7,680
- 13,170
NonsenseTUNDU LISSU JITAFAKARI JUU YA SUMU ULIYOIMWAGA #ULAYA NA #MAREKANI KUHUSU NCHI YETU NA SERIKALI YAKE KABLA YA KUREJEA KUGOMBEA URAIS:
Nataka niseme bila kumung'unya maneno kwamba, raia yeyote, wa nchi yeyote duniani, iwe Marekani, China, Ujerumani au Uarabuni, mwenye kujaribu au kuthubutu kufanya usaliti dhidi ya nchi yake, haijalishi ni usaliti wa kiusalama au wa kiuchumi, kamwe hajawahi kuwa sehemu ya watakatifu wala hakuna serikali mahali popote duniani iliyowahi kushirikiana na mtu au watu wa aina hiyo.
Hii tafsiri yake ni kwamba, ukishaamua kuisaliti nchi yako, basi ujuwe kwamba umejitangazia vita wewe mwenyewe. Huo ndiyo ukweli na utabakia kuwa ukweli mchungu.
#Baba wa taifa hayati Mwl. Nyerere aliwahi kutuonya kwenye moja ya hotuba zake kwamba, kama kweli tumedhamiria kujenga taifa la haki lisilo la wanyonyaji, kamwe hatuwezi kuogopa kelele za wapumbavu na wanyonyaji.
Tutapata matatizo, tutapata misukosuko, Tutapata majizi humu humu, Tutapata watetezi wa mabepari humu huku, lakini nchi itakwenda. Na mimi nirejee kauli ya Rais wangu Dkt. John Pombe Magufuli kwamba, Tumechelewa mno, #Tumechezewa sana, Tudhamiria nchi iende, atakaye jaribu kutukwamisha, atakwama yeye.
Katika vita ya kiuchumi iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Jemadari Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiwemo kukamata makontena ya mchanga wa dhahabu zaidi ya 200 yaliyokuwa bandari ya Dar es Salaam, Rais Magufuli kwa uchungu mkubwa alisema:-
#Namnukuu. Nimeamua kuyatoa maisha yangu sadaka kwa ajili ya kuwapigania watanzania ikibidi hata nife. Maisha yangu hayatakuwa na thamani kama Rais kwa kuona watanzania wakifa kwa kukosa dawa hospitali, watoto wa masikini wakikosa elimu, hali ya usafiri ikiwa mbaya, halafu mimi niwe sehemu ya wanaoshiriki kuhujumu taifa hili kwa kufukuzana na machinga barabarani huku tukiacha kukusanya kodi kwa wanaokwepa kulipa kodi ya serikali. Nimeamua nchi iende na atakayejaribu kutukwamisha, atakwama yeye mwenyewe. #MwishoKunukuu.
Wakati Rais wetu #akiapa kiapo cha kulitumikia taifa, mwenzetu Tundu Lissu aliamua kusimama upande wa wanyonyaji ACACIA na BARRICK badala ya kusimama upande wa nchi. Tena alienda mbali kwa kumtishia nyau Rais wetu kwamba, kitendo alichofanya cha kukamata mali za wawekezaji kitapelekea nchi kushitakiwa kwenye mahakama za Kimataifa za usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji kwa mujibu wa mikataba iliyopo.
Kitendo cha kutetea #unyonyaji wa rasilimali za taifa ziendelee kuporwa kwa kunufaisha wachache badala ya kulinufaisha taifa, hiyo peke yake ilitosha kumtambulisha Tundu Lissu kwa watanzania kwamba yeye ni adui namba moja kuliko walivyo wanyonyaji wa uchumi wetu ikiwemo kampuni ya kuchimba dhahabu ya ACACIA tuliyoambiwa ilikuwa ikichimba dhahabu nchini bila kusajiliwa popote.
Nataka niseme kwamba, kama taifa tumepigana vita ya kutetea rasilimali za nchi yetu ikiwemo madini kwa kuanza na kutunga sheria, tukasimama kidete, kuzungumza na wawekezaji, Mungu akasimama upande wetu, na hatimaye tukashinda. Sasa tunayo kampuni ya kizalendo ya ubia kati ya Tanzania na Barrick iitwayo Twiga ambayo tunagawana faida 50x50.
#Lisu alikuwa tayari kwa lolote ili kutengeneza Nchi ikose Utulivu na Mungu alivyo wa pekee leo mpango huo muovu ulioupanga umegharibu maisha yake.
Wakati #serikali ikipambana kutetea rasilimali zake ili ziwanufaishe wananchi, kwa upande wake yeye Tundu Lissu alikuwa akipambana kuzunguka Ulaya na Marekani kumwaga sumu kwa nchi wafadhiri ili nchi yetu inyimwe misaada, iwekewe vikwazo vya kiuchumi. Kama vile hiyo haikutosha, akajitoa kimasomaso kwa ajili ya kusaidia wenye madeni na Tanzania kukamata ndege zetu huko Canada na Afrika kusini, lengo likiwa ni kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inakwama. Wahenga walisema Mungu si Athumani, hatimaye licha ya figisu figisu, tumeingia uchumi wa kati.
#Napata taabu sana, #ninapomtafakari mtu wa aina hii, anapata wapi ujasiri na nguvu za kufikia hatua ya kutangaza kugombea Uraisi wa nchi ambayo ameshiriki kuibomoa tena kwa mikono yake mwenyewe? Hivi ni nani aliyemshauri Tundu Lissu atangaze kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kama hakushauriwa na mtu isipokuwa ni mawazo yake, wakati anawaza kugombea uraisi alikuwa ndotoni au? Yaani uje ugombee urais, ufaidi matunda ya vita ya kiuchumi ambayo hukuipigania? Wewe ni nani? Nina hasira, Sitaki kusema sana, Wakati ni ukuta, tunamsubiri.
Nimecopy kutoka kwa mdau mmoja uko facebook ILA UJUMBE UWAFIKIE VIJANA WOTE WAFUATA UPEPO NA MANENO YA VIJIWE WA CHADEMA MJITAFAKALI