Tundu Lissu jitafakari juu ya sumu uliyoimwaga Ulaya na Marekani kuhusu nchi yetu na Serikali yake kabla ya kurejea kugombea Urais

TUNDU LISSU JITAFAKARI JUU YA SUMU ULIYOIMWAGA #ULAYA NA #MAREKANI KUHUSU NCHI YETU NA SERIKALI YAKE KABLA YA KUREJEA KUGOMBEA URAIS:

Nataka niseme bila kumung'unya maneno kwamba, raia yeyote, wa nchi yeyote duniani, iwe Marekani, China, Ujerumani au Uarabuni, mwenye kujaribu au kuthubutu kufanya usaliti dhidi ya nchi yake, haijalishi ni usaliti wa kiusalama au wa kiuchumi, kamwe hajawahi kuwa sehemu ya watakatifu wala hakuna serikali mahali popote duniani iliyowahi kushirikiana na mtu au watu wa aina hiyo.

Hii tafsiri yake ni kwamba, ukishaamua kuisaliti nchi yako, basi ujuwe kwamba umejitangazia vita wewe mwenyewe. Huo ndiyo ukweli na utabakia kuwa ukweli mchungu.

#Baba wa taifa hayati Mwl. Nyerere aliwahi kutuonya kwenye moja ya hotuba zake kwamba, kama kweli tumedhamiria kujenga taifa la haki lisilo la wanyonyaji, kamwe hatuwezi kuogopa kelele za wapumbavu na wanyonyaji.

Tutapata matatizo, tutapata misukosuko, Tutapata majizi humu humu, Tutapata watetezi wa mabepari humu huku, lakini nchi itakwenda. Na mimi nirejee kauli ya Rais wangu Dkt. John Pombe Magufuli kwamba, Tumechelewa mno, #Tumechezewa sana, Tudhamiria nchi iende, atakaye jaribu kutukwamisha, atakwama yeye.

Katika vita ya kiuchumi iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Jemadari Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiwemo kukamata makontena ya mchanga wa dhahabu zaidi ya 200 yaliyokuwa bandari ya Dar es Salaam, Rais Magufuli kwa uchungu mkubwa alisema:-
#Namnukuu. Nimeamua kuyatoa maisha yangu sadaka kwa ajili ya kuwapigania watanzania ikibidi hata nife. Maisha yangu hayatakuwa na thamani kama Rais kwa kuona watanzania wakifa kwa kukosa dawa hospitali, watoto wa masikini wakikosa elimu, hali ya usafiri ikiwa mbaya, halafu mimi niwe sehemu ya wanaoshiriki kuhujumu taifa hili kwa kufukuzana na machinga barabarani huku tukiacha kukusanya kodi kwa wanaokwepa kulipa kodi ya serikali. Nimeamua nchi iende na atakayejaribu kutukwamisha, atakwama yeye mwenyewe. #MwishoKunukuu.

Wakati Rais wetu #akiapa kiapo cha kulitumikia taifa, mwenzetu Tundu Lissu aliamua kusimama upande wa wanyonyaji ACACIA na BARRICK badala ya kusimama upande wa nchi. Tena alienda mbali kwa kumtishia nyau Rais wetu kwamba, kitendo alichofanya cha kukamata mali za wawekezaji kitapelekea nchi kushitakiwa kwenye mahakama za Kimataifa za usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji kwa mujibu wa mikataba iliyopo.

Kitendo cha kutetea #unyonyaji wa rasilimali za taifa ziendelee kuporwa kwa kunufaisha wachache badala ya kulinufaisha taifa, hiyo peke yake ilitosha kumtambulisha Tundu Lissu kwa watanzania kwamba yeye ni adui namba moja kuliko walivyo wanyonyaji wa uchumi wetu ikiwemo kampuni ya kuchimba dhahabu ya ACACIA tuliyoambiwa ilikuwa ikichimba dhahabu nchini bila kusajiliwa popote.

Nataka niseme kwamba, kama taifa tumepigana vita ya kutetea rasilimali za nchi yetu ikiwemo madini kwa kuanza na kutunga sheria, tukasimama kidete, kuzungumza na wawekezaji, Mungu akasimama upande wetu, na hatimaye tukashinda. Sasa tunayo kampuni ya kizalendo ya ubia kati ya Tanzania na Barrick iitwayo Twiga ambayo tunagawana faida 50x50.

#Lisu alikuwa tayari kwa lolote ili kutengeneza Nchi ikose Utulivu na Mungu alivyo wa pekee leo mpango huo muovu ulioupanga umegharibu maisha yake.

Wakati #serikali ikipambana kutetea rasilimali zake ili ziwanufaishe wananchi, kwa upande wake yeye Tundu Lissu alikuwa akipambana kuzunguka Ulaya na Marekani kumwaga sumu kwa nchi wafadhiri ili nchi yetu inyimwe misaada, iwekewe vikwazo vya kiuchumi. Kama vile hiyo haikutosha, akajitoa kimasomaso kwa ajili ya kusaidia wenye madeni na Tanzania kukamata ndege zetu huko Canada na Afrika kusini, lengo likiwa ni kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inakwama. Wahenga walisema Mungu si Athumani, hatimaye licha ya figisu figisu, tumeingia uchumi wa kati.

#Napata taabu sana, #ninapomtafakari mtu wa aina hii, anapata wapi ujasiri na nguvu za kufikia hatua ya kutangaza kugombea Uraisi wa nchi ambayo ameshiriki kuibomoa tena kwa mikono yake mwenyewe? Hivi ni nani aliyemshauri Tundu Lissu atangaze kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Kama hakushauriwa na mtu isipokuwa ni mawazo yake, wakati anawaza kugombea uraisi alikuwa ndotoni au? Yaani uje ugombee urais, ufaidi matunda ya vita ya kiuchumi ambayo hukuipigania? Wewe ni nani? Nina hasira, Sitaki kusema sana, Wakati ni ukuta, tunamsubiri.

Nimecopy kutoka kwa mdau mmoja uko facebook ILA UJUMBE UWAFIKIE VIJANA WOTE WAFUATA UPEPO NA MANENO YA VIJIWE WA CHADEMA MJITAFAKALI
Nonsense
 
Kwahiyo Kitendo alichofanyiwa unaikiona cha kawaida ni kama kuchinja kuku?
 
Kwa akili yako katiba mpya ndio inaweza kuleta maendeleo tanzania? Au uyo ben alikua ni nan ni mtu anayetoa ajira zaidi ya elfu 1000 Tanzania? .....Mkuu wakati mwengine uwe unaongea mambo makubwa yenye tija kwa Taifa acha ujinga wa kulilia watu wasio na tija yeyote kwa taifa (hayupo na mambo yanaenda safi kabisa). ....Katiba ni ile ile na mambo yanaenda kwa kufuata katiba iliyopo, kenya wamebadili katiba ndio nini cha ajabu kimetokea / Watanzania kwa sasa hatutaki poyoyo tunataka mfanya kazi mtemda kazi kweli sio poyoyo nyingi badilikeni wakuu
Kwahiyo Mlimpoteza sababu hana uwezo wa kuajiri idadi hiyo ya watu? Sasa baada ya kumpoteza.ajira ngapi zimepatikana?
 
Yaani mtu anaongea kwa uchungu wa nchi yake na kusema "nimeyatoa maisha yangu sadaka ikibidi hata kufa na nife".

HALAFU

Anatokea mwanafunzi mmoja ambaye ALIELEWA vibaya mapokeo ya siasa za KILIBERALI utamaduni wa magharibi kuwa unaweza hata kumtukana baba yako na bado ukaitwa UHURU WA KUJIELEZA.....

ANATOKEA mwanafunzi mmoja zwazwa mwenye kuthamini wazungu na mifumo Yao ya siasa ANASHAMBULIA TAIFA LAKE NA VIONGOZI WAKE......

Kule US kulikuwa na mwafrika mtumwa ktka mashamba ya mabwana zake......
Mwafrika huyu aliitwa UNCLE TOM....

UNCLE TOM alipata kujikana,kuikana RANGI yake na kuwakana WENZAKE kufikia kusema YEYE HAJIONI KUWA NI MWAFRIKA MTUMWA.....

AKAENDELEA KUWASHANGAA wanaomshangaa kwa kauli yake hiyo ya "kujimwambafy"....

Uncle Tom alifurutu ADA kwa kunadi ya kwamba MTUMWA MWAFRIKA MWEUSI kamwe hawezi kupata mwaliko wa hafla mezani mwa wazungu,wala kuvaa suti km wazungu,Wala kugonga cheers meza moja na mabwana hao,Wala kusikiliza nyimbo mwanana na vinubi wanavyopigiwa ma masters wa kizungu.....

UNCLE TOM AKAWAKANA wazazi wake nduguze na ALIPOTOKA.....

Inasikitisha ngojea niyafute machozi Kwanza😭😭😭😭😭😭😭😭
Ongeza na ili ..kabla Lissu akawa mbunge alifungulia mashtaka kibao na CCM eti anawasumbua wazungu wa migodi.
Aliwatetea wananchi wanyamongo wapate fidia ambayo ccm ilikua imekataza wapewe.
Lissu huyu alionya kua sheria zinazotungwa kwa hati ya dharura ni mbaya wanaccm tulipinga ila mwisho tumeona kabisa....
Ebu njoo na hoja apa kua ni nani kutoka ccm aliwai kusimama kidete juu ya ayo?
Sheria zenyewe za madini na mikataba mpaka leo hamna jipya..Migodi imefungwa,migodi inauzwa kwakua hamna faida nk...
 
hii nchi inapaswa itunge sheria kali dhidi ya wasaliti wa taifa, yeyote anaeisaliti nchi anapoteza sifa ya uzalendo na uraia hivo anafukuzwa nchini na mali zake kutaifishwa, nadhani hapa kidogo nidham itapatikana.
 
hii nchi inapaswa itunge sheria kali dhidi ya wasaliti wa taifa, yeyote anaeisaliti nchi anapoteza sifa ya uzalendo na uraia hivo anafukuzwa nchini na mali zake kutaifishwa, nadhani hapa kidogo nidham itapatikana.
Nyerere aliwaambia wajumbe wa Nec na Kikwete aliwakumbusha maneno yale ya Nyerere

“Mawazo hayapigwi rungu”

Hoja hujibiwa kwa hoja bora zaidi
 
hii nchi inapaswa itunge sheria kali dhidi ya wasaliti wa taifa, yeyote anaeisaliti nchi anapoteza sifa ya uzalendo na uraia hivo anafukuzwa nchini na mali zake kutaifishwa, nadhani hapa kidogo nidham itapatikana.
"Bwana, kama wewe ungehesabu maovu yetu, Ee Bwana, nani angesimama?" (Zaburi 130:3)
 
"Bwana, kama wewe ungehesabu maovu yetu, Ee Bwana, nani angesimama?" (Zaburi 130:3)
hakuna nchi yoyote duniani inayowachekea wanaoisaliti nchi, upumbavu wa aina hii upo tanzania pekee alafu wajinga wasiofikiria wao nikushangilia tu.
 
Nimejadili kwa hoja badala ya kunichallenge objectively unanitukana while sijakutukana....

Endelea kutukana Pal,nimeshayazoea matusi ktka uwanda huu wa siasa...Tena majukwaani face to face itakuwa humu mzeya?

Uwe na amani ya mwenyezi mungu,aaamin.
 
Mlishawahi kufikiria risasi 16 mlizompiga kwenye mwili wake?

Halafu ulishawahi kujiuliza kwanini Lissu amepona? Huoni kupona kwake ni muujiza? Je alietenda muujiza huo wa lisu unamjua? Wewe unaweza kushinda a na aliemuokoa Lissu na 16 bullets?

Mwisho unaijua risasi lakini?
Mkuu ungetumia mifano mingine tu, Adolf Hitler alipona majaribio ya kuuawa si chini ya mara 42. Alipona kiajabu ajabu na akawa mshenzi tu baadae.
Jamaa atafute vigezo vingine vya kuomba uongozi wa nchi, sio risasi.
 
Mkuu ungetumia mifano mingine tu, Adolf Hitler alipona majaribio ya kuuawa si chini ya mara 42. Alipona kiajabu ajabu na akawa mshenzi tu baadae.
Jamaa atafute vigezo vingine vya kuomba uongozi wa nchi, sio risasi.
Majaribio aliyonusurika HITLER yalihusisha risasi za moja kwa moja kwenye nyama? Na ilikuwa risasi ngapi?
 
Hatuna hofu ila tunataka nyie mtoke uko mliko sio sahihi kwa maslai ya nchi ...muondokane na pepo la kuona mambo mema ni mabaya
Unajua Mwenye MAPEPO huwa anaongea asiyo yajua?. Mbaya zaidi huwa anadhoofisha Afya yake kwa Maslahi ya wengine JIFIKIRIE TENA kea utumwa waki wa fikra ndani ya CHAMA CHA WAFUGA CHATU.
 
Back
Top Bottom