Tundu Lissu: IGP Sirro Usitishe Wakosoaji, Safisha Jeshi la Polisi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
IGP SIRRO USITISHE WAKOSOAJI, SAFISHA JESHI LA POLISI

Nimesikiliza kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro kuhusu kupatikana kwa Mo Dewji. IGP Sirro amesema, pamoja na mengi mengine, kwamba wanaotafuta uadui na Jeshi la Polisi wasije wakalaumu litakapowatokea la kutokea. Kwake yeye, kukosoa utendaji wa Jeshi la Polisi katika masuala makubwa kama utekaji nyara wa raia ni kukosa uzalendo. Amehoji uraia wetu wote ambao tumekosoa sana utendaji wa Jeshi la Polisi katika sakata hili la utekaji nyara wa Mo Dewji na Watanzania wengine, baadhi yao wakiwa hawajapatikana kwa karibu miaka miwili. Badala ya kulaumu wakosoaji, IGP Sirro anahitaji kujiangalia kioo yeye na Jeshi la Polisi analoliongoza.

1. Kwa ushahidi wa hili la Mo Dewji peke yake, Jeshi la Polisi limeonyesha hadharani udhaifu mkubwa katika utendaji kazi wake na katika mawasiliano yake na umma:

(i) Je, Mo Dewji alitekwa na Wazungu wawili (RPC Mambosasa, Oct. 11, 2018); au na watu wanaozungumza mojawapo ya lugha za makabila ya Afrika Kusini (RPC Mambosasa, leo alfajiri Oct. 20, 2018); au na watu wanaozungumza Kiingereza na Kiswahili cha hovyo hovyo (IGP Sirro, asubuhi ya leo Oct. 20, 2018)???

(ii) Je, gari iliyotumika kumtekea Mo Dewji (picha zilitolewa na IGP Sirro jana Oct. 19, 2018) ni ile ile iliyotumika kumrudisha uraiani (picha za leo) kweli??? Hata kwa muuza mihogo wa barabarani Dar, picha za gari hilo zilizotolewa na Jeshi la Polisi zinaonyesha tofauti kubwa sana.

(iii) Je, Mo Dewji aliwasilianaje na ndugu zake baada ya kuachiliwa usiku wa leo??? Tuliambiwa na RPC Mambosasa (Oct. 11, 2018) kwamba alidondosha funguo na simu yake wakati anatekwa nyara. Leo tumesikia kwa ndugu zake kwamba baada ya kuachiwa usiku ule, aliwapigia simu ndio wakaenda kumchukua alikotupwa bila kulitaarifu Jeshi la Polisi. Je, alidondosha simu yake siku ya kutekwa, au alikuwa nayo muda wote wa siku tisa akiwa mateka, au watekaji walimrudishia simu yake wakati wanamwachia??? Je, ni kitu kinachoingia akilini kwamba alikuwa na simu yake kwa siku tisa bila kuichaji??? Je, inaingia akilini kwamba watekaji wake walimwachia akae na simu yake muda wote huo??? Je, inaingia akilini kwamba watekaji wake watakuwa wamempa simu ili awasiliane na ndugu zake baada ya kumwachilia huru???

(iv) Gari iliyotumika kumtekea iliingia kutokea Kenya (IGP Sirro, Oct. 19, 2018), lakini namba za usajili (AGC 404 MC) zinasemekana ni za Msumbiji. Namba za usajili za gari ya leo (?304 AXX) ni za wapi??? Hii habari mbona haijakaa sawa Afande IGP???

(v) Picha za gari tulizoonyeshwa tangu Oct. 11 hadi leo ni za CCTV au ni za SisiTV??? Kama ni za CCTV kweli mbona zinatofautiana sana na zinazoonyeshwa na BBC, CNN au Al Jazeera katika sakata la mwandishi wa habari Jamal Khashoggi??? Kama ni za SisiTV, nani amezitengeneza, na kwa malengo gani???

2. Kutekwa kwa Mo Dewji sio tukio la kawaida lakini sio la kwanza tangu Rais Magufuli aingie madarakani. Wanaokosoa utendaji wa Jeshi la Polisi wamehoji na kuunganisha na matukio mengine ya aina hii ambayo hayajapewa uzito wowote ule na Jeshi la Polisi:

(i) Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Ben Saanane, ametoweka toka November 2016 hadi sasa, na Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yoyote rasmi kwa umma; na, licha ya madai ya Wabunge, Serikali haijatoa taarifa yoyote rasmi kwa umma. Kama alivyo Mo Dewji, Ben Saanane ni Mtanzania na ana ndugu na familia vile vile.

(ii) Mwandishi wa habari Azori Gwanda wa gazeti la Mwananchi, aliyekuwa anachunguza taarifa za mauaji ya askari na raia Kibiti, Mkuranga na Rufiji, amepotea tangu February 2017, baada ya kuchukuliwa nyumbani kwake Dar Es Salaam na watu waliokuwa kwenye gari yenye vioo vyeusi. Na yeye pia ni raia wa nchi mwenye ndugu na familia.

(iii) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Simon Kanguye, naye amepotea baada ya kuchukuliwa nyumbani kwake na watu wanaodaiwa kuwa wa vyombo vya dola. Hadi leo hii mwaka umepita na hajaonekana na hakuna taarifa yoyote rasmi ya Jeshi la Polisi na au ya Serikali kuhusiana na kupotea kwa mwanaCCM huyu.

(iv) Kuna raia zaidi ya 300, kwa taarifa zilizotolewa Bungeni, ambao wametoweka baada ya kuchukuliwa na askari polisi kutoka majumbani, mashambani na madukani kwao, na wengine hata misikitini, katika maeneo mbali mbali ya Kibiti, Kilwa, Mkuranga na Rufiji. Hadi sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya Jeshi la Polisi na au ya Serikali kuhusu kutoweka kwao. Hawa wote ni Watanzania waliokuwa na haki ya kulindwa na Jeshi la Polisi na wana ndugu na familia vile vile.

(iv) Wasanii Roma Mkatoliki na Ney wa Mitego nao walitekwa nyara lakini wakaachiliwa katika mazingira yanayofanana na hili la Mo Dewji, baada ya kelele kubwa ya umma mitandaoni na kwingineko. Hadi leo hii Jeshi la Polisi liko kimya na matukio hayo.

3. Zaidi ya utekaji nyara, kuna matukio ya mauaji yenye sura ya kisiasa ambayo Jeshi la Polisi limeyanyamazia hadi sasa.

(i) Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alfons Mawazo, aliuawa kwa kukatwa mapanga mchana kweupe mwezi November 2015. Hadi sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya Jeshi la Polisi.

(ii) Diwani Luena wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero (CHADEMA) naye aliuawa kwa kukatwa mapanga usiku. Hadi leo hii Jeshi la Polisi liko kimya.

(iii) Katibu Kata ya Hananasif (CHADEMA) Daniel John alitekwa nyara na baadae maiti yake kuokotwa Coco Beach Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi liko kimya hadi leo.

(iv) Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Dar Es Salaam (DIT), Aquilina Aquiline, aliuawa mchana kweupe na askari polisi maeneo ya Kinondoni. Polisi waliohusika na mauaji hayo wamesafishwa na Jeshi la Polisi na hivyo hakuna taarifa yoyote rasmi juu ya nani hasa ndiye mhusika hadi sasa.

4. Mashambulio ya mabomu (mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa marudio Soweto, Arusha, Kanisa Katoliki Olasiti, Arusha, na ofisi za kampuni ya mawakili ya IMMA Advocates ya Dar Es Salaam, 26 July 2017); na mashambulizi ya risasi dhidi yangu Dodoma, 7 September, 2017, yamenyamaziwa na Jeshi la Polisi hadi sasa.

Katika mazingira haya, IGP Sirro anawezaje kushangaa watu wanapohoji utendaji na uadilifu wa Jeshi la Polisi???

Tunahitaji majibu ya maswali haya, sio vitisho vya wale tunaowalipa mshahara ili wawe na majibu sahihi badala ya propaganda.

Tuna wajibu wa kuhoji. Kuyanyamazia haya ni kuungana na watekaji nyara na wauaji. Tunakataa kunyamaza kimya.

Tundu Lissu.
 
IMG-20181021-WA0002.jpg
 
Japo siafiki zoezi zima la movie lilivyoenda lakini pia napata mashaka na huu uandishi wa kamanda, kufuatilia habari kwa umakini. Kwa upande wangu siwezi kuandika kitu kama ndivyo kilivyo hadi niwe na taarifa sahihi au ntaweka wazi kwamba nafikiria hivyo au kama sikosei.

Mathalani kwenye suala la simu, tumeambiwa na viongozi wetu wazalendo kwamba alitumia simu ya walinzi wa gymkana, kwanini tena kwenye haya maelezo habari za simu kudondoka hadi kuhoji aliwasilianaje na ndugu zake zinakujaje? Nimerejea maelezo ya sehemu ya (iii)

Mie nnachouliza, hao walinzi wanaolinda hilo eneo walijua wakati gani kuna gari imeingia hapo, wakaenda kuliangalia na kukuta jamaayuko ndani, wakamfungua, wakampa simu bila hata kutoa taarifa polisi? Tukumbuke hapo dau la 1 Bln lilikua bado lipo hewani.
Inamaana hawakuona kabisa waliokuja na gari waliondokaje na nini kiliendelea?

Mwisho, ina maana yale maelezo yote kwamba kuna watu wanapitia mafunzo au zoezi la kuwasaka wahusika ndio limeishia hapo kwa kutishiwa kwamba jeshi letu liko imara?
 
Binafsi nalaumu kutokua na sera ya kuonyesha tunadeal vipi na watekaji/ magaidi. Nchi zisizo za Afrika nyingi zina sera ya kutokuoongea na mtekaji.

Kuna kipindi watoto walitekwa na kupelekwa Uganda kisha mzazi anadaiwa fedha ili mtoto aachiwe. Nilichoshangazwa ni kwamba, wazazi ndiyo walikua wanafanya negotiation na askari walijiweka kando kabisa.

Mtekaji alitaka dola 1000 baada ya kuongea na wazazi akakubali dola 600 mtoto akasafirishwa ila hakukua na askari wa kulifuatilia tukio kinyume mpaka huko Uganda. Wote tukasema mradi karudi salama basi haina shida.

Kama Mo alitekwa ni muendelezo wa tatizo la kukosa sera. Ninachoona ni kwamba jamaa walilipwa pesa ndiyo maana kaachiwa na nina asilimia za kuamini kua wazazi wa Mo ndiyo walioendesha negotiation mpaka drop point ikapangwa.

Hivyo Mo hajapatikana ila ameachiliwa.
 
IGP SIRRO USITISHE WAKOSOAJI, SAFISHA JESHI LA POLISI

Nimesikiliza kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro kuhusu kupatikana kwa Mo Dewji. IGP Sirro amesema, pamoja na mengi mengine, kwamba wanaotafuta uadui na Jeshi la Polisi wasije wakalaumu litakapowatokea la kutokea. Kwake yeye, kukosoa utendaji wa Jeshi la Polisi katika masuala makubwa kama utekaji nyara wa raia ni kukosa uzalendo. Amehoji uraia wetu wote ambao tumekosoa sana utendaji wa Jeshi la Polisi katika sakata hili la utekaji nyara wa Mo Dewji na Watanzania wengine, baadhi yao wakiwa hawajapatikana kwa karibu miaka miwili. Badala ya kulaumu wakosoaji, IGP Sirro anahitaji kujiangalia kioo yeye na Jeshi la Polisi analoliongoza.

1. Kwa ushahidi wa hili la Mo Dewji peke yake, Jeshi la Polisi limeonyesha hadharani udhaifu mkubwa katika utendaji kazi wake na katika mawasiliano yake na umma:

(i) Je, Mo Dewji alitekwa na Wazungu wawili (RPC Mambosasa, Oct. 11, 2018); au na watu wanaozungumza mojawapo ya lugha za makabila ya Afrika Kusini (RPC Mambosasa, leo alfajiri Oct. 20, 2018); au na watu wanaozungumza Kiingereza na Kiswahili cha hovyo hovyo (IGP Sirro, asubuhi ya leo Oct. 20, 2018)???

(ii) Je, gari iliyotumika kumtekea Mo Dewji (picha zilitolewa na IGP Sirro jana Oct. 19, 2018) ni ile ile iliyotumika kumrudisha uraiani (picha za leo) kweli??? Hata kwa muuza mihogo wa barabarani Dar, picha za gari hilo zilizotolewa na Jeshi la Polisi zinaonyesha tofauti kubwa sana.

(iii) Je, Mo Dewji aliwasilianaje na ndugu zake baada ya kuachiliwa usiku wa leo??? Tuliambiwa na RPC Mambosasa (Oct. 11, 2018) kwamba alidondosha funguo na simu yake wakati anatekwa nyara. Leo tumesikia kwa ndugu zake kwamba baada ya kuachiwa usiku ule, aliwapigia simu ndio wakaenda kumchukua alikotupwa bila kulitaarifu Jeshi la Polisi. Je, alidondosha simu yake siku ya kutekwa, au alikuwa nayo muda wote wa siku tisa akiwa mateka, au watekaji walimrudishia simu yake wakati wanamwachia??? Je, ni kitu kinachoingia akilini kwamba alikuwa na simu yake kwa siku tisa bila kuichaji??? Je, inaingia akilini kwamba watekaji wake walimwachia akae na simu yake muda wote huo??? Je, inaingia akilini kwamba watekaji wake watakuwa wamempa simu ili awasiliane na ndugu zake baada ya kumwachilia huru???

(iv) Gari iliyotumika kumtekea iliingia kutokea Kenya (IGP Sirro, Oct. 19, 2018), lakini namba za usajili (AGC 404 MC) zinasemekana ni za Msumbiji. Namba za usajili za gari ya leo (?304 AXX) ni za wapi??? Hii habari mbona haijakaa sawa Afande IGP???

(v) Picha za gari tulizoonyeshwa tangu Oct. 11 hadi leo ni za CCTV au ni za SisiTV??? Kama ni za CCTV kweli mbona zinatofautiana sana na zinazoonyeshwa na BBC, CNN au Al Jazeera katika sakata la mwandishi wa habari Jamal Khashoggi??? Kama ni za SisiTV, nani amezitengeneza, na kwa malengo gani???

2. Kutekwa kwa Mo Dewji sio tukio la kawaida lakini sio la kwanza tangu Rais Magufuli aingie madarakani. Wanaokosoa utendaji wa Jeshi la Polisi wamehoji na kuunganisha na matukio mengine ya aina hii ambayo hayajapewa uzito wowote ule na Jeshi la Polisi:

(i) Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Ben Saanane, ametoweka toka November 2016 hadi sasa, na Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yoyote rasmi kwa umma; na, licha ya madai ya Wabunge, Serikali haijatoa taarifa yoyote rasmi kwa umma. Kama alivyo Mo Dewji, Ben Saanane ni Mtanzania na ana ndugu na familia vile vile.

(ii) Mwandishi wa habari Azori Gwanda wa gazeti la Mwananchi, aliyekuwa anachunguza taarifa za mauaji ya askari na raia Kibiti, Mkuranga na Rufiji, amepotea tangu February 2017, baada ya kuchukuliwa nyumbani kwake Dar Es Salaam na watu waliokuwa kwenye gari yenye vioo vyeusi. Na yeye pia ni raia wa nchi mwenye ndugu na familia.

(iii) Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Simon Kanguye, naye amepotea baada ya kuchukuliwa nyumbani kwake na watu wanaodaiwa kuwa wa vyombo vya dola. Hadi leo hii mwaka umepita na hajaonekana na hakuna taarifa yoyote rasmi ya Jeshi la Polisi na au ya Serikali kuhusiana na kupotea kwa mwanaCCM huyu.

(iv) Kuna raia zaidi ya 300, kwa taarifa zilizotolewa Bungeni, ambao wametoweka baada ya kuchukuliwa na askari polisi kutoka majumbani, mashambani na madukani kwao, na wengine hata misikitini, katika maeneo mbali mbali ya Kibiti, Kilwa, Mkuranga na Rufiji. Hadi sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya Jeshi la Polisi na au ya Serikali kuhusu kutoweka kwao. Hawa wote ni Watanzania waliokuwa na haki ya kulindwa na Jeshi la Polisi na wana ndugu na familia vile vile.

(iv) Wasanii Roma Mkatoliki na Ney wa Mitego nao walitekwa nyara lakini wakaachiliwa katika mazingira yanayofanana na hili la Mo Dewji, baada ya kelele kubwa ya umma mitandaoni na kwingineko. Hadi leo hii Jeshi la Polisi liko kimya na matukio hayo.

3. Zaidi ya utekaji nyara, kuna matukio ya mauaji yenye sura ya kisiasa ambayo Jeshi la Polisi limeyanyamazia hadi sasa.

(i) Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alfons Mawazo, aliuawa kwa kukatwa mapanga mchana kweupe mwezi November 2015. Hadi sasa hakuna taarifa yoyote rasmi ya Jeshi la Polisi.

(ii) Diwani Luena wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero (CHADEMA) naye aliuawa kwa kukatwa mapanga usiku. Hadi leo hii Jeshi la Polisi liko kimya.

(iii) Katibu Kata ya Hananasif (CHADEMA) Daniel John alitekwa nyara na baadae maiti yake kuokotwa Coco Beach Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi liko kimya hadi leo.

(iv) Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Dar Es Salaam (DIT), Aquilina Aquiline, aliuawa mchana kweupe na askari polisi maeneo ya Kinondoni. Polisi waliohusika na mauaji hayo wamesafishwa na Jeshi la Polisi na hivyo hakuna taarifa yoyote rasmi juu ya nani hasa ndiye mhusika hadi sasa.

4. Mashambulio ya mabomu (mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa marudio Soweto, Arusha, Kanisa Katoliki Olasiti, Arusha, na ofisi za kampuni ya mawakili ya IMMA Advocates ya Dar Es Salaam, 26 July 2017); na mashambulizi ya risasi dhidi yangu Dodoma, 7 September, 2017, yamenyamaziwa na Jeshi la Polisi hadi sasa.

Katika mazingira haya, IGP Sirro anawezaje kushangaa watu wanapohoji utendaji na uadilifu wa Jeshi la Polisi???

Tunahitaji majibu ya maswali haya, sio vitisho vya wale tunaowalipa mshahara ili wawe na majibu sahihi badala ya propaganda.

Tuna wajibu wa kuhoji. Kuyanyamazia haya ni kuungana na watekaji nyara na wauaji. Tunakataa kunyamaza kimya.

Tundu Lissu.
Baadhi ya maswali ni mazuri ila nikiri Lissu kidogo kuna mahali hayuko sawa. Kuna maswali kwa jinsi alivyo 'mwanasheria msomi' hakupaswa kuuliza maswali ya dizaini hiyo yako cheap sana. Yalitakiwa yaulizwe na mtu asiye na uelewa kabisa.
Mfano swali la 1 (iii), (iv) na (v).

Pia nasikitika mauaji ya Kibiti kwake sio kitu kikubwa.
 
Narudia tena, haya maswali ni magumu sana jamani, ni magumu kwelikweli, "hatujawahi kupata maswali ya ajabu namna hii" in Lisu's voice
 
Hoja za maana sana lakini kwa kuwa kaandika Lissu, basi lazima Kunguru wa Lumumba wataanza kuchangia bila hata ya kujua Lissu kaandika nini!!
Vilaza wa Lumumba wapo nyumbani kwa Le mutuz mda huu wakikariri ujinga toka kwa Le mutuz jiandaeni kuona majibu ya kijuha mda si mrefu kutokana na CCM kusheheni mbumbu wa kutosha mitandaoni.
 
Binafsi nalaumu kutokua na sera ya kuonyesha tunadeal vipi na watekaji/ magaidi. Nchi zisizo za Afrika nyingi zina sera ya kutokuoongea na mtekaji.

Kuna kipindi watoto walitekwa na kupelekwa Uganda kisha mzazi anadaiwa fedha ili mtoto aachiwe. Nilichoshangazwa ni kwamba, wazazi ndiyo walikua wanafanya negotiation na askari walijiweka kando kabisa.

Mtekaji alitaka dola 1000 baada ya kuongea na wazazi akakubali dola 600 mtoto akasafirishwa ila hakukua na askari wa kulifuatilia tukio kinyume mpaka huko Uganda. Wote tukasema mradi karudi salama basi haina shida.

Kama Mo alitekwa ni muendelezo wa tatizo la kukosa sera. Ninachoona ni kwamba jamaa walilipwa pesa ndiyo maana kaachiwa na nina asilimia za kuamini kua wazazi wa Mo ndiyo walioendesha negotiation mpaka drop point ikapangwa.

Hivyo Mo hajapatikana ila ameachiliwa.
MO HAJAPATIKANA KWA MSAKO ILA AMEACHILIWA BAADA YA KUMALIZANA PIA MAOMBI YA GWAJIMA
 
Back
Top Bottom