Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

Lisu anapoteza mwelekeo japo mkulu kapotea zaidi
Tulia tu kidogo, utamwelewa Tundu. Soma ukiwa umeweka jazba pembeni.
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Khaaa, hivi waliokua wakiomba mikataba na wawekezaji iwe inajadiriwa bungeni ni kina nani? Unalikumbuka sakata la Buzwagi lililompa umaarufu Zitto? Tundu alikua mwana harakati tu mtaani wakati ule but one day akiwa ch 10 nilimwona akiuonesha mkataba ule, sijui aliuiba sehemu, don't know.
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Umemsikia mkulu wakati anazindua fly over ya Ubungo wewe? Siku ambayo Nape alikua anaunda tume ya kumchunguza Makonda, irudie tu ile hotuba and then sijui kama utasema tena hiki ulicho kisema.
 
Hivi kwa nn watu mnatoa povu sana kuwatetea hawa jamaaa????? hv watanzania tutaendeshwa sana na hawa wanasiasa maana ndo hao walikua wanapiga kelele kua mikataba ya madini ni mibovu leo wanawatetea !!!!hapo mm ndo hua nachoka na tz jamaan wanatuachia mashimo tu hao mm naona rais kaanza vizuri na hilo ili wasione tz ni shamba la bibi yao
uzuri rais wetu yupo makini hatishwi na mavuvuzera kila baya lao haya jems delishas huyo kamteteeni
 
Watu wanaochangia hapa wengi wana uelewa mdogo au siasa zimebeba akili zao.

Lissu hajatetea wawekezaji ila katoa maoni tu kwamba kuuzuia huo mchanga kutapelekea kuwalipa hao jamaa anachotakiwa kukifanya Magu ni kuita watu wenye dhamana ya sheria na mikataba wajue nini cha kufanya tujitoe huko kwenye pingu za kimataifa ndyo tuje kuwabana huku ndani.
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Amuandikie kumshauri kwani alimsindikiza kuchukua fomu?
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Huwa unasikilizaga bajeti mbadala zinazowasilishwa na upinzani bungeni? Yote yanayojadiliwa kwa manufaa ya nchi yankuwa humo. Kwa kuwa chama tawala wanaringia wingi wao, wapinzani huwa hawasikilizwi
 
Lisu acha siasa za unaharakati. hacha kupinga kila kitu toa way forward siyo kila kitu kupinga. tunakukubali but siyo kila kitu ni kibaya bwana
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Una IQ kubwa sana
 
Lisu acha siasa za unaharakati. hacha kupinga kila kitu toa way forward siyo kila kitu kupinga. tunakukubali but siyo kila kitu ni kibaya bwana
Watu wanaochangia hapa wengi wana uelewa mdogo au siasa zimebeba akili zao.

Lissu hajatetea wawekezaji ila katoa maoni tu kwamba kuuzuia huo mchanga kutapelekea kuwalipa hao jamaa anachotakiwa kukifanya Magu ni kuita watu wenye dhamana ya sheria na mikataba wajue nini cha kufanya tujitoe huko kwenye pingu za kimataifa ndyo tuje kuwabana huku ndani.
Asante sana mkuu mwingine huyo ameandika hapo ndo wale wale.
 
Huoni aibu kuandika hayo uliyoyaandika kwenye nyekundu hapo?
Tatizo siyo nyie "tatizo ni akili zenu "muwe mnasoma na kuelewa kabla kukurupuka kuandika pumba!
Hivi kwa nn watu mnatoa povu sana kuwatetea hawa jamaaa????? hv watanzania tutaendeshwa sana na hawa wanasiasa maana ndo hao walikua wanapiga kelele kua mikataba ya madini ni mibovu leo wanawatetea !!!!hapo mm ndo hua nachoka na tz jamaan wanatuachia mashimo tu hao mm naona rais kaanza vizuri na hilo ili wasione tz ni shamba la bibi yao
Acha kushindana na kila kitu raisi anachotolea maamuzi. Tumekuchoka. Acha kutafuta sifa za kitoto. U r too radical.
sikuhizi wameacha kuimba reggae wanaimba ndombolooo
 
Sera ipo toka 2009 kuwa hawa wawekezaji wakishirikiana na serikali wajenge hizo smelt hapa nchini. Miaka saba sasa hakuna dalili. Sasa unafanyaje ili wajue kuwa tunataka smelt hapa nchini?
 
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
Huna msaada katika nchi hii. Sijui na familia yako wanakuchukulia vipi.

Naamini wanavumilia tu coz hawawezi pata baba mwingine.

Lini utasaidia serikali lini utanusulu mawazo yako yakajenga, lini utaacha kejeli katika nchi inayo kupa kulala na kubwabwaja hivyo.

unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Jamaa huwa yuko ivo...rais angeruhusu usafirishwe angepinga mchanga wetu unaibiwa. ..siku zote yeye ni anti-gvmnt, ndo kazi yake
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Aliye kwambia magu anashaurika ni nani?
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Nyie si ndio mpo wengi?
Na tangu lini fisiem ikachukua ushauri wa wapinzani.
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Ushasahau kasema yeye ndo anaamua na hapangiwi cha kufanya??
 
BADO NAAMINI SERIKALI YA AWAMU YA TATU HAIKIWA NA NIA NJEMA KWA TAIFA LETU KATIKA HILI NA PIA LIKAENDELEZWA NA AWAMU YA NNE. NAAMINI PIA RAIS JPM ANA NIA NJEMA TUONDOKE HAPA NA NDICHO TUNDU LISSU ANACHOELEZA VIZURI KISHERIA KWAMBA UTARATIBU WA KUZUIA MCHANGA ANAOFANYA RAIS SIO NJIA SAHIHI NA KWAMBA WAWEZA KUWA HASARA KUBWA ZAIDI KWETU KWA KUJUA MIKATABA ILIVYOINGIWA NA HUO NDIO UKWELI MCHUNGU. SWALA SIO KWAMBA TUNDU LISSU ANAPINGA KILA KITU HAPANA, NI UKWELI KWAMBA WALIOKO CCM HAWATHUBUTHU KUMWAMBIA RAIS UKWELI KUHOFIA KUPATA KADHIA KAMA YA NAPE, MSUKUMA,BASHE NA MALIMA KAMA MIFANO. NADHANI WAKATI UMEFIKA KWA RAIS KUJARIBU KUJISHUSHA NA KUKUBALI KUSHAURIWA NA IKIWEZEKANA KUFANYA KAZI HATA NA UPINZANI KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI. MWALIMU NYERERE ALITAKA TUSICHIMBE MADINI MPAKA TUWE NA WATAALAM WA KUTOSHA NA MZEE MWINYI ALILIONA HILI PIA. WALIOFUATA WAKAONA NI UPUUZI. SASA TUNALIA. NAMSIFIA DR. KAFUMU KUONYESHA MSIMAMO KAMA WA LISSU, JAPO KWA LUGHA YA KUJIHADHARI MGONGANO NA RAIS MOJA KWA MOJA - NA HAPA NDIO FAIDA YA UPINZANI DUNIANI. WAO HUSEMA STRAIGHT. WA NDANI MARA NYINGI NI KUNUNGUNIKA NA KUTOKUWA WAKWELI NA KUSIFIA KILA KITU CHA KIONGOZI MKUU. TUANGALIE FACTS SIO LAZIMA NANI KASEMA.
 
Kwa taarifa yako, big brand ijulikanayo kama "TUNDU LISSU" leo hii ilipatikana kwenye madini; enzi hizo, tena akiwa kijana mdogo sana, akitetea wachimbaji wadogo waliofukiwa kama panya kupisha wawekezaji kwenye migodi/maeneo kadhaa enzi za Mkapa; 1996 to 2000's kama sijakosea. Homework hiyo; nenda library kaongeze maarifa. Wewe na uzee wako hapo ulipo una faida gani kwa taifa?
 
Back
Top Bottom