Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

Binafsi sioni kosa la Lissu, ameeleza ni nini Rais alipaswa kufanya kabla ya kuzuia mchanga kusafirishwa.. Magufuli ana nia nzuri lakini njia anazotumia zinaweza zikaliingizia taifa hasara zaidi badala ya faida kwa sababu ya mikataba iliyoingiwa na serikali zilizopita na wawekezaji hawa..
Tusiwe mashabiki wa watu, tuwe mashabiki wa ukweli.. Tanzania ni yetu sote
Tatizo kuna watu wanashida ktk kufikiri. Huyo anaye mchimbaji Tundu anamtambua jamaa akishaapishwa kusema hawezi kuchaguliwa wala kuelekezwa cha kufanya. Angemsikiliza Tundu?
 
Kwa jinsi hiyo mikataba ilivyoandaliwa na inavoikaba Serikali zoezi la kuijadili upya ni kizungumkuti. Labda wanasheria wangeshauri kitaalam nchi itajiondoa vipi kwenye shimo hilo la mikataba mibovu bila kukiuka haki za wahusika kama zilivyoainishwa ndani ya mikataba hiyo.
Nadhani Lissu kaeleza vizuri tu kwa kutumia mfano wa Ivo Morales. Tulitakiwa kufanya hivyo na siyo kuvunja taratibu halafu utafute namna ya kujitoa.
 
Acheni kucheza na akili za watanzania nyie ndio mmetufikisha hapa tulipo inabidi muwajibike maana mnatuingiza kwenye mikataba mibovu afu mwisho wa siku bado tunaishia kuburuzwa mahakamani na kulipishwa mabilioni aaaaaarrrgghhhh !!!

Unajua ripoti ya jana umenaswa, sasa ubizi gani huu jana kushinda unaniquote na leo umeniamkia eeeh

Maisha ya mkato mabaya atiiii...eeeeh
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Kwani leo ndo umeyasikia hayo? Si huwa mnapiga tu makofi yakiwafika mnasema hamkushauriwa?

Sema ni yepi wapinzani waliishauri serikali ikayachukua? Ina maana na mwanasheria mkuu wa serikali hayajui hayo? Mnaiingiza nchi matatizoni halafu mnatoa lawama kambale nyie.
 
Jamani wapinzani wamesema sana kuhusu mikataba mibovu na kwenye hili sasa Ccm tuwainge mkono kwa kuidai ifumuliwe na kuangaliwa upya lissu nimekuelewa, Rais wetu lazimisha hilo na ninaamini hilo litakuja soon maana tume ya pili inafuatilia hilo pia
 
Unajua ripoti ya jana umenaswa, sasa ubizi gani huu jana kushinda unaniquote na leo umeniamkia eeeh

Maisha ya mkato mabaya atiiii...eeeeh
Mimi naongelea kuhusu uwajibikaji wa ccm kwa kutuingiza kwenye mikataba mibovu ssa nimenaswaje na ripoti?? Nipo acacia au nina undugu na fisadi muhongo ???

Nmekuqoute maana unapotosha umma so watu tunaojielewa hatuwezi kukubali upuuzi wako
 
Unajua ripoti ya jana umenaswa, sasa ubizi gani huu jana kushinda unaniquote na leo umeniamkia eeeh

Maisha ya mkato mabaya atiiii...eeeeh
Halafu ukiwa unatumia fake ID JF,usichukulie jambo lolote personal!Hakuna anayekujua so jibu hoja au mpotezee aliyekuquote!

Sakata hili la mchanga kuna tatizo kwenye report ya Tume,mark my words,tutaumbuka na Rais wetu kwa kukurupuka!Kwa taarifa ya report ni kuwa mchanga unaotoka nje ni zaidi ya thamani ya 18 Trilion kwa mwaka!Hii sio kweli,kwa mwaka mchanga huingiza around Trilion 1.0-1.8!
Natabiri hili suala litakuja kuisha kimya kimya ukweli ukibainika!
 
Nimesikitishwa sn na maoni ya Lisu, kwanafasi yako kama mbunge na ubobezi wa kisheria nashindwa kuelewa unatoa maoni haya sasa. Unaouwezo wa kuzungumza na mwanasheria mkuu wa serikali, mawaziri na wote wenye mamlaka katika hili ili kututoa hapa tulipo. Tulikuwa tunalalama sn na JK kwamba alikumbatia wezi. Kwa JPM hili sidhani kama linawezekana na siku zote mnaimba wimbo wa maslahi ya nchi kwanza. Sasa kwanini usitumie nafasi yako kutoa huu ushauri kwa wahusika na badala yake unauleta kwenye mitandao ya kijamii? au tuseme na wewe unahisa humo?
Ulitaka asemee wapi? Aliomba Kama Raisi wa TLS kukutana na Raisi wa Nchi hakujibiwa mpaka Leo, huo ushauri angempa Vipi? Tatizo Raisi wetu anachofanya yeye ndio Sheria, asikilizi watu wala kusoma ya watangulizi wake walipokosea arekebishe, anaona Kama kapata Uhuru Jana na anatakiwa kujenga misingi ya Nchi, kumbe misingi ilishajengwa na watangulizi wake na Dunia nzima inajua, haangali tulipojikwaa, anagombana na tulipodondokea, Sasa CCM huu ni Mzigo wenu hasa Wabunge.

Wabunge wa CCM wanajiona wao ni Serikali bila kujua kwamba wao ni washauri wa Serikali, wakosowaji, Watunga Sheria za kuonyesha Serikali njia ya kufata, Wabunge wa CCM wamekuwa wa Ndiooooooo kila kinacholetwa na Serikali, Sasa hapa ndio muda wa kuona wenye akili ni akinanani.
 
Halafu ukiwa unatumia fake ID JF,usichukulie jambo lolote personal!Hakuna anayekujua so jibu hoja au mpotezee aliyekuquote!

Sakata hili la mchanga kuna tatizo kwenye report ya Tume,mark my words,tutaumbuka na Rais wetu kwa kukurupuka!Kwa taarifa ya report ni kuwa mchanga unaotoka nje ni zaidi ya thamani ya 18 Trilion kwa mwaka!Hii sio kweli,kwa mwaka mchanga huingiza around Trilion 1.0-1.8!
Natabiri hili suala litakuja kuisha kimya kimya ukweli ukibainika!


Wewe naye unajua huyo na mimi humu tunakutanaje kwa posts? La ID linahusu nini...au ulitaka niandike maneno machafu kama nyie wa upinzani...kisa ananiboa na najua ni walewale kisa RC wananiandikia visivyo niongezea maarifa..

Wewe makujua mpinzani, haupendi pia kuona mazuri ya awamu hii

Mtanyooka tu

Sageni meno
 
Wewe naye unajua huyo na mimi humu tunakutanaje kwa posts? La ID linahusu nini...au ulitaka niandike maneno machafu kama nyie wa upinzani...kisa ananiboa na najua ni walewale kisa RC wananiandikia visivyo niongezea maarifa..

Wewe makujua mpinzani, haupendi pia kuona mazuri ya awamu hii

Mtanyooka tu

Sageni meno
Nimekwambia hivyo sababu hata mimi ulishawahi kuniambia maneno kama hayo nikapuuzia!Nilipoona umeandik tena ikabidi tu nikukumbushe!

Mark my words,kuficha aibu atakayoipata Rais hili jambo litaisha kimya kimya!Kwa data zile za Rais ni kuwa Buly ni the largest Gold mine in the world!
 
Wayaseme mara ngapi?? Aliwahu kuyasema haya lisu huko nyamongo mkaishua kumpiga vurungu afu leo hii mnataka mseme ndio mmegundua tulikuwa tunaibiwa??? Kwamba miaka yote mlikuwa hamjui??? Shame on u ccm
Hao enzi hizo walikhwa wanachunga mbuzi huko bushi watayajua haya?
 
Kwa bandiko hili SINA imani tena na wewe Lissu. Ni msomi usiye na faida kwa Taifa hili. Wawekezaji wana faida gani kama tunaibiwa hivi? Si bora hata Madini yenyewe yasichimbwe kuliko ujinga tunaofanyiwa?? Naanza kuona kuwa wewe ni miongoni kwa wasomi wabinafsi sana katika Taifa hili kiasi cha kutia aibu!!
Akili zako ni za kuchangia mijadala ya udaku huku hauwezi kamwe. Haoa unaona nyota tu
 
Nimekwambia hivyo sababu hata mimi ulishawahi kuniambia maneno kama hayo nikapuuzia!Nilipoona umeandik tena ikabidi tu nikukumbushe!

Mark my words,kuficha aibu atakayoipata Rais hili jambo litaisha kimya kimya!Kwa data zile za Rais ni kuwa Buly ni the largest Gold mine in the world!

Oooh

Basi ni kwasababu mnapenda kurudia rudia mnayoniandikia...hivyo tu...

Acha kuniambia tutashindwa..napenda kuwa positive na kusukuma kufika...na ndivyo JPM alivyo now.

Endelea kunyooka, nchi ni yetu sote
 
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
Yaani nikifikaga hapa ndo huwa nachanganyikiwa kabisa kumjua mpinzani wa kweli na mpinzani uchwara
Tundu Lissu aliyoyasema yote ni unafiki mtupu na uzandiki
Hivi taaruma yake imeisaidiaje nchi?
Akiwa kama mtu mwenye uelewa na haya mambo ya kisheria tokea ameingia madarakani raisi wetu ameshauri nini kwa manufaa ya nchi yetu?
Lissu ushauri wako waweza kuwa mzuri lakini hebu unganisha nguvu kinchi zaidi ili tujiondoe kwenye wizi huu wa lasilimali zetu
Afadhali basi raisi amefanya maamuzi magumu kuliko wewe unayejua kukosoa tu bila kutoa suluhu mbadala ya tatizo
Kama kweli unauchungu na wizi tuliofanyiwa kwa miaka yote hiyo hebu nenda kamwone Mwanasheria Mkuu wa serikali mshauliane kiutu uzima mweleze kona zote za kisheria zitakazotusaidia kujitoa kwenye giza hili
Jiepushe usiwe sehemu ya kulaumu jipe nafasi ya kuwa sehemu ya ufumbuzi
USHAURI WANGU KWAKO
 
Alioutuo Tundu Lissu ni ushauri tosha.Wewe ulitaka aende Ikulu akamshauri?.
Ni ushauri uliopaswa kutolewa jana na sio leo.
Lakinipia lugha za kashfa na dharau kwa Rais ambaye kiukweli ana dhamira na uchungu usiotia shaka juu ya rasilimali zetu sio USTAARABU.
 
Kwa hili Mkapa alituingiza ktk mikataba mibovu. Lakini huwa historia hujirudia kwa uzuri au kwa ubaya akukumbuke Mungu hakuwaleta Watanzania ktk nchi hii wapate wanayoyapata kutokana na mambo yake

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom