Tundu Lissu: Hotuba ya Rais Magufuli kuhusu Makontena ya Mchanga, inatia shaka ya rule of state

....haya aliyoyasema Lissu ni sehemu ya huo ushauri. Ubaya wa wana CCM wengi na viongozi wao HAWAONI zuri lolote wanaloshauriwa na Upande wa kina Lissu. Kumbuka maoni/ushauri wa Mnyika, Kabwe, Lema na wengine wengi tu. Wanachofanya CCM mara nyingi ni kusema: Ondoa hayo maneno kwenye Hotba...."Kuhusu utaratibu", Mwongozo wa Spika..nk. AnavyoLIA na kusikitika raisi wetu leo, ni kuhusu mambo ambayoSerkali "ILISHASHAURIWA" miaka ya nyuma ila wakaweka pamba masikioni...Leo wanashtuka, hawafati utaratibu wa kuviondoa kwanza vitanzi walivyojifunga.....
Youtube zipo hizo mkuu
 
Nadhani ameonyesha kuwa smart kwenye hili,kwa sababu amepata sababu ya kuzuia mchanga,kwani wawekezaji wamedanganya na hivyo itabidi isimame mpaka smelting ipatikane,mwanzo wangeweza kushitaki kwa kuwa serikali haikuwa na ushahidi,leo ni picha tofauti hatakama unamkataba lakini unaiba.
We ongea tu siku mambo yakibadilika tutatafutana humu
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Halafu linasubiri hadi aongee ndio litafte kiki kuponda kinafiki, yaani hayana ajenda mpya kabisa menyewe ni kuponda tu. Kwa taarifa yao 2020 tunamchagua Tena, yavimbe yapasuke kama vp
 
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
Hayo Yote Unayosema KUHUSU BITS TUNAYAJUA NA USIDHANI WEWE PEKE YAKO NDIO ULISOMA SHERIA: UDANGANYIFU NA UKWEPAJI WA KODI ON A GRAND SCALE LIKE THAT IS ENOUGH TO TRIGGER TERMINATION OF SUCH CONTRACTS: Udanganyifu na Ukwepaji wa Kodi Mkubwa Wanaofanya ni Sababu Tosha za Kuuvunja Mkataba Huo Maana Makosa Yako Kwa Mwekezaji. HAKUNA MKATABA AMBAO UNA UMILELE - HILI HATA MWANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA SHERIA ANATAMBUA. Ukwepaji Kodi ni CRIME. WEWE LISSU Ukosoaji Wako Si wa Kizalendo Bali ni wa Kizandiki na NI UHAINI KWA WATANZANIA: TUTAPAMBANA HADI TONE LA MWISHO - WE WILL NOT GIVE IN. Wadanganye na Wakatishe Tamaa Wasiojua Masharti ya Kisheria ya Mikataba
 
unafiki na kujitafutia mtaji kwa wananchi kama unaipenda nchi yetu si ungemuandikia waraka kwake ukamshauri wewe ni kumponda hauna lengo la kuikuza nchi kiuchumi. wewe huo mfano wa bolivia ungemwambia. ila kila kukicha ni kumkosoa na sio kushauri, mpe way forward
Kumshauri Mtu anayesema Kufanya kazi na wewe ni over his Dead body!
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Hata wakipendekeza nani anawaelewa na kuwasikiliza?
Wabunge wa CCM kazi yao kusema ndio hata km hiki kitu ni kwa faida ya Taifa,mikataba mibovu na sheria zote mbovu zilipigiwa kura za ndiooooo na Wabunge wa CCM na JPM akiwa mmojawapo Bungeni huku wakiwacheka wapinzani.halafu leo mtu anajifanya ana uchungu sana mi Naona maigizo tuu.
kinachotakiwa ni kungalia wapi tumejikwaa sio tulipoangukia
 
Hawa wa upinzani si walipiga kelele kabla nchi inapoteza pesa, sasa haya wanayoyaongelea now je waliwahi kupendekeza bungeni kabla!?
Hao ni wanafiki wengine, ndio walewale wasioweza kuridhishwa kila ufanyalo kwao wao baya, ndio maana hii miana siasa mingi ipo kumanipulate akili za watu na si kuwatoa watu walipo, they creat problems even out of solutions, sasa hao ni watu ama devils incernates!
 
Wayaseme mara ngapi?? Aliwahu kuyasema haya lisu huko nyamongo mkaishua kumpiga vurungu afu leo hii mnataka mseme ndio mmegundua tulikuwa tunaibiwa??? Kwamba miaka yote mlikuwa hamjui??? Shame on u ccm
 
Hao ni wanafiki wengine, ndio walewale wasioweza kuridhishwa kila ufanyalo kwao wao baya, ndio maana hii miana siasa mingi ipo kumanipulate akili za watu na si kuwatoa watu walipo, they creat problems even out of solutions, sasa hao ni watu ama devils incernates!
Nani mnafki mkuu?? Haya hta kina zitto na slaa waliyaongea toka enzi za buzwagi ila waliishia kuzomewa tu bungeni afu leo hii unawaita wanafki??? Kwani upinzani ni uadui!!! Magufuli has played his part let opposition play its part too
 
Nazani Tundu Lisu atakana kuwa sio mwandiko wake huu, Leo kama ishu ya Wenje

Sidhani kama katakana,ametoa way forward ya Serikali kuwashinda Acacia, vinginevyo kama Taifa tunaingia kwenye hasira ya kulipa zaidi na kupata hasira zaidi.

Walifanya mikataba hii ni hao hao akina JPM,akiwa waziri miaka 20 iliyopita.Kama angekuwa Mzalendo kweli angajiuzulu kupinga uovu huo,lakini alisema Tumbo lake kwanza.

Hakuna msafi CCM hata hayo ni maigizo tu.

Ameelezwa vyema vunja kwanza mikataba inayotushika,then fanya unayoona ndiyo sahihi.Kwa mikataba CCM iliyoingiza nchi ni mikataba ya akina Mangungo wanaohifanya wanaakili sana kumbe wana asilimia zao hapo.

Hii yote ni danganya Toto.
 
Nani mnafki mkuu?? Haya hta kina zitto na slaa waliyaongea toka enzi za buzwagi ila waliishia kuzomewa tu bungeni afu leo hii unawaita wanafki??? Kwani upinzani ni uadui!!! Magufuli has played his part let opposition play its part too

Sijaona alichofanya zaidi ya kutafuta kick,kwani alikuwa wapi 20yrs ago??Atuambie kwanini hakujiuzulu au kusupport Wapinzani wakati ule wanapiga kelele? Alikuwa mmoja wao siyo?

Ameshakwambia nani yuko nyuma ya zile bilioni nane za kivuko kibovu??Amejengewa hoteli na kandarasi wa Barabara ameshaeleza kama ni kweli au lab?Ndege alizonunua za chini ya kiwango imekuwaje ndiyo Mzalendo??Kununua TT kwa double price je!

Wote ni wale wale subiri ni kama kuna kitakachoendelea hapo.Ameshindwa kutumbua DAB ataweza JK na Mkapa?
 
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
Kwa bandiko hili SINA imani tena na wewe Lissu. Ni msomi usiye na faida kwa Taifa hili. Wawekezaji wana faida gani kama tunaibiwa hivi? Si bora hata Madini yenyewe yasichimbwe kuliko ujinga tunaofanyiwa?? Naanza kuona kuwa wewe ni miongoni kwa wasomi wabinafsi sana katika Taifa hili kiasi cha kutia aibu!!
 
Back
Top Bottom