Tundu Lissu: Hamas Siyo Magaidi ila Wale waliopora Ardhi yao. Unayemuona Gaidi Wewe kwa Wenzako ni Mpigania Uhuru mfano Mandela!

Israel kama nchi ilitambulika rasmi na Umoja wa mataifa mwaka 1948. Lakini hiyo haimaanishi kabla yake haikuwepo.

Tanganyika ilitambulika na Umoja wa Mataifa lini? Je, inamaanisha nchi ya Tanganyika au ardhi ambayo sasa inaitwa Tanganyika, kabla ya 1961, haikuwepo?

Na kabla ya kuanzishwa Umoja wa mataifa ina maana hakukuwepo na nchi hata moja?

Canaan ilikuwepo tangu enzi kabla ya Yesu. Na ni kutoka kwenye hiyo ardhi ya Canaan, kumepatikana Jordan, Lebanon, Israel, na eneo jingine lilitengeneza sehemu ya Misri, Iraq, na Syria.
Alafu hakuna mfalme yeyote wa palestina kwenye historia
 
Kama uliyoyaandika ni kweli basi nimejua kwa nini Lisu afanikiwi kwenye siasa licha ya kutapatapa hapa na pale.

“nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani;…….” Maneno ya Mungu muumba kwa Israel.
Wana wa Israeli ambao hawamuamini Yesu na wanamdhihaki na kumtukana. Je mola atakuwaje nao?
Hawa waliisha muasi Mwenyezi Mungu na akawaahidi hawataishi kwa amani tena mpaka siku ya mwisho.
Hata wakatoliki waliwauwa sana huko Ulaya na wakakimbilia kwenye nchi za waislamu ndipo walikua wakiishi kwa amani.
Kwa hiyo haya yote ni maamuzi ya baba wa mbinguni.
 
Wewe ndiye hauelewi, katika vitabu vya historia neno nchi halikutumika badala yake walitumia maneno kama ardhi hii itaitwa.... au mahali hapa pataitwa.... Na wakati mwingine jina la mtu maarufu wa kabila liliendelezwa na kuwa jina la mahali na kuwa jina la nchi.
Mimi nazungumzia Azimio la Umoja wa Mataifa namba 181 la 1947

Hiyo Biblia Siyo wote wanaiamini
 
Nitawashangaa Kama mtaamini alichoandika John the Baptist kinatoka kwa Lissu. Sijui kwanini mnaingia kwenye mtego wake kirais.
Nenda Youtube

Wewe kila siku uko nyuma ya Wakati kila kitu hadi utafuniwe na akina BoniYai 😂😂

Wachangiaji kadhaa wamemsikiliza na wameongeza na mengine ambayo aliyaongea maana ilikuwa mahojiano ya Zaidi ya dakika 100
 
Kama uliyoyaandika ni kweli basi nimejua kwa nini Lisu afanikiwi kwenye siasa licha ya kutapatapa hapa na pale.

“nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani;…….” Maneno ya Mungu muumba kwa Israel.
Nyerere mbona aliwapinga akafanikiwa, same to Mandela aliwapinga na akafanikiwa.

Kingine Abraham ana watoto wengi zaidi ya 5 n wajukuu maelfu sasa kwani Israel tu ndio wakilaaniwa mtu atalaaniwa wakati huo mstari ni wa Abraham.

Saudi Arabia, Qatar etc zinapinga wayahudi mbona zina uchumi mkubwa kuliko sisi tunaowalamba miguu??

Typical African mindset
 
Tundu Antipas Lissu ameuchambua kwa kina mgogoro wa Gaza na kusema Palestine ipo tangu Enzi za Torati lakini Israel ilianzishwa mwaka 1947 kwa Azimio la Umoja wa Mataifa.

Lisu anasema mwaka 1916 Uingereza ilijitwalia eneo la Mashariki ya Kati na kulitawala ikiwemo Palestine, Jordan, Syria, Saudi Arabia nk

Lissu anazidi kufafanua baada ya Vita Kuu ya kwanza palizuka Makundi ya Kigaidi mawili ya Wayahudi ambayo yalikuwa yanauwa Waarabu hasa Wapalestina na waliwahi kuchoma moto Kijiji kizima cha Wapalestina na kuuwa Wanawake na Watoto Zaidi ya 100 pia walilipua Hotel ya King David

Baada ya kuona hatari ya Wayahudi na hasa baada ya kufyekwa na Hitler na kubakia wachache Uingereza ilipelekea pendekezo UN ili sehemu ya koloni lake la Palestine wapelekwe Wayahudi. Ndipo Azimio la Umoja wa Mataifa namba 181 la mwaka 1947 likapitishwa huku Wayahudi takribani 650,000 wakipewa 56% ya Ardhi ya Palestine na Wenyeji Palestine waliokuwa takribani 1,350,000 wakiachiwa 44% ya Ardhi yao

Lisu anasema baadae Wayahudi wakajiongezea eneo na kufikisha 80% huku Wapalestina wakisongamanishwa kwenye 20% ya Ardhi yao

Na kama haitoshi 1967 baada ya kushinda Vita na Misri na Syria Wayahudi walijimilikisha 100% ya Ardhi ya Wapalestina na kuchukua pia maeneo ya Sinai na Golani

Lisu anasema Hamas ilianzishwa miaka ya 1982 na awali Wayahudi waliwatumia Hamas kuidhoofisha PLO lakini baadae Hamas walijitambua ndipo Wayahudi wakaanza kuwarubuni Fatah wawe ndio Chawa wap

Hamas walijiimarisha na Kwenye Uchaguzi Huru mwaka 2006 Hamas ilishinda viti Vya Ubunge 78 Kati ya viti 132

Lisu anasema Azimio la Umoja wa Mataifa namba 242 la mwaka 1967 linatambua uwepo wa Mataifa Mawili ya Israel na Palestine hivyo Hamas Wana Haki zote kuitetea Ardhi ya Babu zao na Watoto wao

Wewe ukiwaita Hamas ni Magaidi Wenzako Wapenda Haki na Waarabu wote wanawaita ni Wapigania Uhuru

Hata Mandela na ANC waliitwa ni Magaidi na Condolesa Rice alipokuwa Waziri wa Foreign wa USA alisema anapata tabu Wakati anapomualika Waziri mwenzake wa Foreign Affairs wa SA Kwani inabidi kwanza atengue ile kanuni ya Ugaidi wa ANC ndipo apewe visa, amesema Lisu

Lisu anasema Wayahudi kama wanaamini wataifuta Hamas.basi wanajidanganya sana

Lisu anamalizia kwa kusema kichekesho kilichopo ni Kuwa Waisrael karibia milioni 20 Wako New York Marekani Wakati pale Israel Wako milioni 7 na ushee tu na Zaidi ya nusu ya raia wote wa Jordan ni Wapalestina

Nawatakia Dominica Njema
Lisu ameongea vizuri kabisa wale wafia dini .. wa taifa teule wamepewa makavu kaawambia ukweli kabisa
 
"Palestina ipo tangu enzi za Torati lakini Israeli ilianzishwa mwaka 1947 kwa Azimio la Umoja wa Mataifa" - Tundu Lissu

Labda kama mtoa taarifa amemnukuu Lissu vibaya, pengine alikuwa na maana Israeli ya sasa, na wala siyo ile ya kihistoria. Kwa kuwa ukivisoma vitabu vyote vitano viundavyo Torati ndivyo hasa vyenye kuelezea historia ya Israeli na uhalali wao wa kumiliki nchi yao.

Kitabu cha Mwanzo kinaelezea kwa kina asili ya taifa hili na ahadi ya kumiliki eneo hili, Kitabu cha Kutoka kinaonyesha historia yao kuanza kuwa taifa lenye kuhesabika kwa muundo wao wa makabila 12, kitabu cha Walawi kikionyesha uongozi wao wa kiroho kupitia mamlaka ya kikuhani chini ya Mungu wao mkuu YHWH.

Kitabu cha Hesabu ni mpango mkakati wa kuvita ili kuiendea na kuitwaa nchi ya ahadi, yaani Kaanani na kuitambua hata mipaka ya nchi yao ya ahadi, na kitabu cha Kumbukumbu la Torati kimesheheni amri mbalimbali za kimwili ambazo ziliwekwa ili wapate utakaso na kibali mbele ya Mungu wao mkuu, YHWH.

Ni kweli Palestina ilikuwepo na inatajwa wakati wa enzi za Torati, lakini si kweli ya kwamba Israeli haikuwepo. Israeli ilikuwapo, ilikuwapo, kwa nyakati kadhaa haikuwepo, sasa ipo, na siku zote itakuwepo. Ni vyema tukachunga ndimi zetu kwa ajili tu ya kutaka kupata kiki na umaarufu wa kisiasa.

Ni lazima tutambue na tuelewe, tupende tusipende, Israeli ina uhalali wa kumiliki eneo lake ambalo walikabidhiwa na Mungu mwenyewe, na eneo hilo walionyeshwa mpaka mipaka yake yote na majirani zake. Mungu si kama mwanadamu hata tupate kumtilia mashaka ya kile alichokiamuru, kwa hakika kwa kufanya hivyo ni kumtii Ibilisi.

Pengine ni vyema tukatafakari kwa pamoja maudhui yaliyopo nyuma ya kipande kifuatacho kutoka katika maandiko matakatifu.

WARUMI 11
33 Jinsi utajiri wa Mungu ulivyo mkuu! Hekima yake na maarifa yake hayana mwisho. Njia zake na maamuzi yake hayachunguziki!

34 Kwa maana ni nani amepata kufahamu mawazo ya Mungu au kuwa mshauri wake?

35 Au ni nani amewahi kumpa cho chote ili arudishiwe?

36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa ajili yake na vyote vinadumu kwake. Utukufu ni wake milele. Amina.
 
Tundu Antipas Lissu ameuchambua kwa kina mgogoro wa Gaza na kusema Palestine ipo tangu Enzi za Torati lakini Israel ilianzishwa mwaka 1947 kwa Azimio la Umoja wa Mataifa.

Lisu anasema mwaka 1916 Uingereza ilijitwalia eneo la Mashariki ya Kati na kulitawala ikiwemo Palestine, Jordan, Syria, Saudi Arabia nk

Lissu anazidi kufafanua baada ya Vita Kuu ya kwanza palizuka Makundi ya Kigaidi mawili ya Wayahudi ambayo yalikuwa yanauwa Waarabu hasa Wapalestina na waliwahi kuchoma moto Kijiji kizima cha Wapalestina na kuuwa Wanawake na Watoto Zaidi ya 100 pia walilipua Hotel ya King David

Baada ya kuona hatari ya Wayahudi na hasa baada ya kufyekwa na Hitler na kubakia wachache Uingereza ilipelekea pendekezo UN ili sehemu ya koloni lake la Palestine wapelekwe Wayahudi. Ndipo Azimio la Umoja wa Mataifa namba 181 la mwaka 1947 likapitishwa huku Wayahudi takribani 650,000 wakipewa 56% ya Ardhi ya Palestine na Wenyeji Palestine waliokuwa takribani 1,350,000 wakiachiwa 44% ya Ardhi yao

Lisu anasema baadae Wayahudi wakajiongezea eneo na kufikisha 80% huku Wapalestina wakisongamanishwa kwenye 20% ya Ardhi yao

Na kama haitoshi 1967 baada ya kushinda Vita na Misri na Syria Wayahudi walijimilikisha 100% ya Ardhi ya Wapalestina na kuchukua pia maeneo ya Sinai na Golani

Lisu anasema Hamas ilianzishwa miaka ya 1982 na awali Wayahudi waliwatumia Hamas kuidhoofisha PLO lakini baadae Hamas walijitambua ndipo Wayahudi wakaanza kuwarubuni Fatah wawe ndio Chawa wap

Hamas walijiimarisha na Kwenye Uchaguzi Huru mwaka 2006 Hamas ilishinda viti Vya Ubunge 78 Kati ya viti 132

Lisu anasema Azimio la Umoja wa Mataifa namba 242 la mwaka 1967 linatambua uwepo wa Mataifa Mawili ya Israel na Palestine hivyo Hamas Wana Haki zote kuitetea Ardhi ya Babu zao na Watoto wao

Wewe ukiwaita Hamas ni Magaidi Wenzako Wapenda Haki na Waarabu wote wanawaita ni Wapigania Uhuru

Hata Mandela na ANC waliitwa ni Magaidi na Condolesa Rice alipokuwa Waziri wa Foreign wa USA alisema anapata tabu Wakati anapomualika Waziri mwenzake wa Foreign Affairs wa SA Kwani inabidi kwanza atengue ile kanuni ya Ugaidi wa ANC ndipo apewe visa, amesema Lisu

Lisu anasema Wayahudi kama wanaamini wataifuta Hamas.basi wanajidanganya sana

Lisu anamalizia kwa kusema kichekesho kilichopo ni Kuwa Waisrael karibia milioni 20 Wako New York Marekani Wakati pale Israel Wako milioni 7 na ushee tu na Zaidi ya nusu ya raia wote wa Jordan ni Wapalestina

Nawatakia Dominica Njema 😀
Mwambie huyo Lissu kama anafikiri atapata kura za upande wa pili bila kusilimu anajidanganya. Lissu anaukana ukweli ulioandikwa mwenye biblia wakati anajiita mkristo! Na urais wa nchi hii haupati ng'o.
Wakati wa torati iliitwa Caanan siyo palestine. Huyo mfalme Daudi alitawala wapi na alikuwa kabila gani?

Lissu mnafiki mkubwa
 
Kwenye historia juu ya Palestine na Israel, hapo Lisu amepata zero.

Palestine na Israel, ilitangulia kuwepo Israel kabla ya Palestine. Neno Palestine linaonekana kwa mara ya kwanza wakati wa utawala wa Warumi, na ilimaanisha pwani ya bahari ya nchi ya Canaan, ambayo wakazi wake wengi walikuwa ni Wayahudi, na wachache walikuwa wafilisti na Waarabu.

Kimsingi hakuna watu wanaoitwa wapalestina. Hawa wanaoitwa wapalestina ni waarabu waliokuwa wakiishi ndani ya nchi ya Canaan.
Hapo unehadithiwa na mchungaji kibwetere na ww ukameza hivyo hivyo bila kutafuna
 
Kwa hiyo Lissu kuwaunga mkono Hamas maana yake anakubali njia wanazotumia kudai uhuru wao?

Hamas wameua mpaka ndugu zetu watanzania, unasema vipi hawa sio magaidi?

Huko Chadema kutoa uhai wa wengine hata wasiohusika kwenye vita yenu, ili kudai uhuru wako ni sawa?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kuna kitu kinaitwa collateral damage vitani, hivyo hao Watanzania waliofia huko Palestine ndio matokeo ya vita

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mwambie huyo Lissu kama anafikiri atapata kura za upande wa pili bila kusilimu anajidanganya. Lissu anaukana ukweli ulioandikwa mwenye biblia wakati anajiita mkristo! Na urais wa nchi hii haupati ng'o.
Wakati wa torati iliitwa Caanan siyo palestine. Huyo mfalme Daudi alitawala wapi na alikuwa kabila gani?

Lissu mnafiki mkubwa
Upuuzi
 
Back
Top Bottom