Dunia imeshindwa kuwalinda Watoto wa Palestine?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,075
Wayahudi wamepitia magumu mengi tangu enzi za kabla ya Yesu, ikiwemo kuuawa na kisha kutiwa utumwani Misri na Babylon (Iraq), kunyang'anywa ardhi yao iliyomilikiwa na babu zao, ardhi iliyokuwa ikianzia Misri, hadi baadhi ya maeneo ya Jordan, Lebanon, na Iraq. Kama hiyo haitoshi, Hitler aliamua kuwamaliza Wayahudi wote. Akafanikiwa kuwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6. Hata walipoamua kurudi kwenye ardhi ya babu zao, wakitokea Ulaya walikokuwa wakiuawa kwa njia mbalimbali za mateso na maanagamizi, wakafika kwenye ardhi yao ya Canaan, wakawakuta Waarabu wamejimilikisha ardhi yote.

Pamoja na Waisrael kukubali kuchukua eneo dogo waliyogawiwa na Wakoloni Waingereza, wakiacha eneo kubwa kwa Waarabu waliojimilikisha ardhi yao, pamoja na UN kupitisha azimio kuwa eneo hilo dogo walilogawiwa litambulike kuwa ni ardhi ya Taifa la Israel, bado haikuwasaidia Wayahudi kupata amani wala uhakika wa kuishi. Mwanzoni kabisa, mwaka huo huo 1948 ambapo Taifa la Israel lilitambuliwa rasmi na umoja wa Mataifa, mataifa 6 ya kiarabu yalipitisha azimio la kuwamaliza Wayahudi wote, na kulifuta Taifa la Israel.

Wakaanzisha vita ya kuwaangamiza wayahudi, lakini Mungu akawa upande wa Wayahudi, dhamira ya mataifa ya Kiarabu ikashindwa. Vita hivyo vya mwaka 1948, vilifuatiwa na vita vingine vya mwaka 1956, 1967, 1973 na 1982. Katika vita hivyo, mataifa ya kiarabu, na mara moja Taifa la Urusi (USSR) yaliingia vitani moja kwa moja. Lakini kuna vita vingine nane ambavyo Hamas, Hizbollah na makundi mengine yalishiriki pekee yao. Kwa hiyo, mpaka leo, vita hii ya sasa ni ya 18, Israel inapambana na watu wanaotamani Israel isiwepo katika ramani ya Dunia.

Baadhi ya mataifa, kama vile Misri, baadaye yaliamua kuachana na msimamo wao wa awali, na hivyo kuamua kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel. Na baadaye mataifa mengine mengi ya kiarabu yaliamua kufuata msimamo wa Misri. Lakini Taifa la Iran, tangu wakati huo mpaka leo limeendelea kushikilia msimamo wake kuwa Wayahudi hawastahili kuwepo Duniani, wala Taifa la Israel, na huo ndiyo umekuwa msimamo wa makundi ya kigaidi ya Hamas na Hizbollah, yaliyoanzishwa na yanaendelea kufadhiliwa na Iran.

Makundi haya ya kigaidi ya Hamas na Hizbolah yamekuwa hatari kwa Israel, Wapalestina na mwingine yeyote aliye kinyume nayo. Kundi la kigaidi la Hamas, mara moja liliamua kuanzisha vita dhidi ya ya serikali ya Abbas likipinga Wapelestina kufanya makubaliano yoyote na Waisrael. Wao msimamo wao ni Wayahudi wamalizwe, wasiwepo Duniani.

Katika vita hivyo, Hamas walifanikiwa kuiondoa Serikali ya PLO kwenye eneo la Gaza, na kisha wao Hamas wakaanzisha utawala wao. Hata ulipofanyika usuluhishi, Hamas hawakukubali kuiachia Gaza iwe chini ya mamlaka ya Ramallah. Wakati wa uchaguzi, Hamas wakajigeuza kuwa chama cha siasa, na kushinda uchaguzi eneo la Gaza.

Japo, hakuna uhakika kama Wapalestina wa Gaza waliwachagua Hamas kwa hiari au kwa woga. Kwa itikadi ya Hamas, yeyote anayeshindwa kuendana na matakwa yao, anastahili kifo. Hata sasa wakati mashambulio ya Wayahudi yanaendelea, raia wameombwa kuondoka maeneo ya Gaza Kaskazini ambako Hamas wamechimba mahandaki mengi ambayo milango yake inatokea kwenye majengo mbalimbali ikiwemo hospitali, nyumba za makazi, shule na hata misikitini, Hamas wanawazuia watu wasiondoke, kwa sababu kwao raia wasio wapiganaji ndiyo ngao ya kuwakinga na mashambulio ya Israel.

LAKINI Masikitiko makubwa ni juu ya vifo vya watoto, watu wasio na hatia wala hawana utashi wa kuamua chochote. Kila ukiona picha za miili ya watoto hawa, inahuzunisha sana. Lakini pamoja na watoto hawa, wapo pia watu wazima ambao kwao kilicho muhimu ni uhai wao, hawana ambitions za madaraka, wala utajiri, wala ardhi, wala siyo wafuasi wa itikadi za Hamas. Wanalazimika kutofanya chochote dhidi ya Hamas ili angalao waishi.

Hawa kwa mazingira yalivyo sasa, wamekuwa mateka wa Hamas, na hivyo kuibeba adhabu ya Hamas. Hawa ndio tunaowaonea huruma.

Wangepatikana viongozi wenye hekima, wangeweza kuokoa maisha ya watoto hawa na watu hawa wazima ambao mioyo yao haina uovu.

Kwa nini viongozi wenye hekima, wasifanye utaratibu wa kuwatengea eneo salama watoto hawa pamoja na mama zao, ikiwezekana hata ndani ya Israel? Nina imani Israel haiwezi kulikataa hilo, maana hata kabla ya vita kulikuwa na Wapalestina wa Gaza waliokuwa wanafanya kazi Israel, kila siku wakienda Israel na kurudi Gaza.

Lakini pia, ndani ya Israel, kuna Wapelestina na Waarabu ambao ni raia wa Israel, wanaishi ndani ya Israel. Israel imekuwa ikiwapa umeme, maji na misaada ya chakula Wapalestina wa Gaza, haiwezi kushindwa kuwahifadhi watu hawa wasio maadui kwao.

Nina hakika, bila ya Hamas, Hizbollah, na zaidi bila ya Iran, Wapalestina na Wayahudi, wote wanaweza kuishi kwa amani. Amani ya Israel na Palestine, inauawa na Iran.

Je, Dunia imeshindwa kuidhibiti Iran ili kuokoa maisha ya Wapalestina na Wayahudi? Wapalestina ni dhaifu sana kuweza kupambana na makundi ya kigaidi ya Iran kama vile Hamas na Hizbollah, inahitajika nguvu ya kimataifa, hasa mataifa ya Kiarabu.
 
WAarab hawajawahi kuwa na akili umfute mwenzako ili iweje?
Kusema hivi simaanishi na mimi ni mbumbumbu wa kuamini israel ni taifa teule. anayewaita hao taifa teule ni taahira kama taahira yoyote aliyethibitishwa na dokta.
 
Umeandika mambo mengi lakini umeandika uharo tu unasema Iran haitaki wayahudi wawepo duniani hali ya kuwa ndani ya nchi yake ana raia kibao wenye asili ya kiyahudi tena wengine wako ndani ya taasisi nyeti ndani ya nchi hiyo mbona hajaanza kuwauwa hao?

Unasema Iran ndo mvuruga amani kati ya Israel na palestina kwani Iran ndo huwa anawatuma akina Netanyau kupora ardhi na kuuwa wapalestina kila mwaka?

Mgogoro kati ya Israel na palestina upo kwa zaidi ya miaka 75 hata kabla ya Hamas kuanzishwa na kabla ya serikali ya sasa haijaingia mamrakani nchi Iran.

Tangu kuanza kwa kwaka 2023 takwimu zinaonesha wapalestina zaidi ya 600 wakiwemo watoto zaidi ya 100 wamesha uawa na vikosi vya Israel huko west bank vipi na huko kuna hamas?
 
mungu wa wagalatia alishindwa kumlinda katoto kake dhidi ya waisraeli waka kapasua msalabani , ndiyo dunia itaweza kulinda watoto wa palestina
 
Radicals ndio msingi wa huu mgogoro. Imani bila akili ni disaster kubwa hasa kwa kiumbe muarabu akisaidiwa na mshirika wake kiumbe mweusi
Duuuuh, WAKRISTO mnajikutaga mna akili Sana

Chuki ya WAKRISTO dhidi ya waislamu ni kubwa mno
 
Wayahudi wamepitia magumu mengi tangu enzi za kabla ya Yesu, ikiwemo kuuawa na kisha kutiwa utumwani Misri na Babylon (Iraq), kunyang'anywa ardhi yao iliyomilikiwa na babu zao, ardhi iliyokuwa ikianzia Misri, hadi baadhi ya maeneo ya Jordan, Lebanon, na Iraq. Kama hiyo haitoshi, Hitler aliamua kuwamaliza Wayahudi wote. Akafanikiwa kuwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6. Hata walipoamua kurudi kwenye ardhi ya babu zao, wakitokea Ulaya walikokuwa wakiuawa kwa njia mbalimbali za mateso na maanagamizi, wakafika kwenye ardhi yao ya Canaan, wakawakuta Waarabu wamejimilikisha ardhi yote.

Pamoja na Waisrael kukubali kuchukua eneo dogo waliyogawiwa na Wakoloni Waingereza, wakiacha eneo kubwa kwa Waarabu waliojimilikisha ardhi yao, pamoja na UN kupitisha azimio kuwa eneo hilo dogo walilogawiwa litambulike kuwa ni ardhi ya Taifa la Israel, bado haikuwasaidia Wayahudi kupata amani wala uhakika wa kuishi. Mwanzoni kabisa, mwaka huo huo 1948 ambapo Taifa la Israel lilitambuliwa rasmi na umoja wa Mataifa, mataifa 6 ya kiarabu yalipitisha azimio la kuwamaliza Wayahudi wote, na kulifuta Taifa la Israel.

Wakaanzisha vita ya kuwaangamiza wayahudi, lakini Mungu akawa upande wa Wayahudi, dhamira ya mataifa ya Kiarabu ikashindwa. Vita hivyo vya mwaka 1948, vilifuatiwa na vita vingine vya mwaka 1956, 1967, 1973 na 1982. Katika vita hivyo, mataifa ya kiarabu, na mara moja Taifa la Urusi (USSR) yaliingia vitani moja kwa moja. Lakini kuna vita vingine nane ambavyo Hamas, Hizbollah na makundi mengine yalishiriki pekee yao. Kwa hiyo, mpaka leo, vita hii ya sasa ni ya 18, Israel inapambana na watu wanaotamani Israel isiwepo katika ramani ya Dunia.

Baadhi ya mataifa, kama vile Misri, baadaye yaliamua kuachana na msimamo wao wa awali, na hivyo kuamua kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Israel. Na baadaye mataifa mengine mengi ya kiarabu yaliamua kufuata msimamo wa Misri. Lakini Taifa la Iran, tangu wakati huo mpaka leo limeendelea kushikilia msimamo wake kuwa Wayahudi hawastahili kuwepo Duniani, wala Taifa la Israel, na huo ndiyo umekuwa msimamo wa makundi ya kigaidi ya Hamas na Hizbollah, yaliyoanzishwa na yanaendelea kufadhiliwa na Iran.

Makundi haya ya kigaidi ya Hamas na Hizbolah yamekuwa hatari kwa Israel, Wapalestina na mwingine yeyote aliye kinyume nayo. Kundi la kigaidi la Hamas, mara moja liliamua kuanzisha vita dhidi ya ya serikali ya Abbas likipinga Wapelestina kufanya makubaliano yoyote na Waisrael. Wao msimamo wao ni Wayahudi wamalizwe, wasiwepo Duniani.

Katika vita hivyo, Hamas walifanikiwa kuiondoa Serikali ya PLO kwenye eneo la Gaza, na kisha wao Hamas wakaanzisha utawala wao. Hata ulipofanyika usuluhishi, Hamas hawakukubali kuiachia Gaza iwe chini ya mamlaka ya Ramallah. Wakati wa uchaguzi, Hamas wakajigeuza kuwa chama cha siasa, na kushinda uchaguzi eneo la Gaza.

Japo, hakuna uhakika kama Wapalestina wa Gaza waliwachagua Hamas kwa hiari au kwa woga. Kwa itikadi ya Hamas, yeyote anayeshindwa kuendana na matakwa yao, anastahili kifo. Hata sasa wakati mashambulio ya Wayahudi yanaendelea, raia wameombwa kuondoka maeneo ya Gaza Kaskazini ambako Hamas wamechimba mahandaki mengi ambayo milango yake inatokea kwenye majengo mbalimbali ikiwemo hospitali, nyumba za makazi, shule na hata misikitini, Hamas wanawazuia watu wasiondoke, kwa sababu kwao raia wasio wapiganaji ndiyo ngao ya kuwakinga na mashambulio ya Israel.

LAKINI Masikitiko makubwa ni juu ya vifo vya watoto, watu wasio na hatia wala hawana utashi wa kuamua chochote. Kila ukiona picha za miili ya watoto hawa, inahuzunisha sana. Lakini pamoja na watoto hawa, wapo pia watu wazima ambao kwao kilicho muhimu ni uhai wao, hawana ambitions za madaraka, wala utajiri, wala ardhi, wala siyo wafuasi wa itikadi za Hamas. Wanalazimika kutofanya chochote dhidi ya Hamas ili angalao waishi.

Hawa kwa mazingira yalivyo sasa, wamekuwa mateka wa Hamas, na hivyo kuibeba adhabu ya Hamas. Hawa ndio tunaowaonea huruma.

Wangepatikana viongozi wenye hekima, wangeweza kuokoa maisha ya watoto hawa na watu hawa wazima ambao mioyo yao haina uovu.

Kwa nini viongozi wenye hekima, wasifanye utaratibu wa kuwatengea eneo salama watoto hawa pamoja na mama zao, ikiwezekana hata ndani ya Israel? Nina imani Israel haiwezi kulikataa hilo, maana hata kabla ya vita kulikuwa na Wapalestina wa Gaza waliokuwa wanafanya kazi Israel, kila siku wakienda Israel na kurudi Gaza.

Lakini pia, ndani ya Israel, kuna Wapelestina na Waarabu ambao ni raia wa Israel, wanaishi ndani ya Israel. Israel imekuwa ikiwapa umeme, maji na misaada ya chakula Wapalestina wa Gaza, haiwezi kushindwa kuwahifadhi watu hawa wasio maadui kwao.

Nina hakika, bila ya Hamas, Hizbollah, na zaidi bila ya Iran, Wapalestina na Wayahudi, wote wanaweza kuishi kwa amani. Amani ya Israel na Palestine, inauawa na Iran.

Je, Dunia imeshindwa kuidhibiti Iran ili kuokoa maisha ya Wapalestina na Wayahudi? Wapalestina ni dhaifu sana kuweza kupambana na makundi ya kigaidi ya Iran kama vile Hamas na Hizbollah, inahitajika nguvu ya kimataifa, hasa mataifa ya Kiarabu.
Umeshindwa kusema naiunga mkono Israel kuua wapalestine kila mwaka, sema tu hakuna anaye kuzuia upo huru.
 
Hivi labda na mimi niulize israeli kila siku anavunja makazi ya wapalestina na kupanua makaazi ya walowezi wapya wa kiyahudi hawa wapalestina waende wakaishi wapi?
 
Hata walipoamua kurudi kwenye ardhi ya babu zao
Kina nani mkuu? Maana makabila yalikua 12 yaliyorudi Israel ni makabila mangapi?

Kingine kusema ni ardhi ya mababu hivi leo Kagame akaidai Kivu sababu historically ilitawaliwa na machifu wa kitutsi mbona anapingwa? Historically Kagera ilikua chini ya Hema empire ya Uganda mbona Idd Amin alipotaka kuirejesha tulimzuia? Oooh leo hii Oman warudi kudai zanzibar sababu tu mababu zao waliishi huko tutakubali?

Mind you Israel alikuta canaan kuna makabila yanaishi, akafanya massacre ndio akatawala so its not like it was an empty plain.
 
Back
Top Bottom