Tundu Lissu bila Team Lowasa ni bure!

Tundu Lissu bila Team Lowasa ni bure!

Barbarosa unahangaika na Lisu sana. Mtaji wa Lisu ni ujasiri, msimamo na uwezo wa kipekee wa kujenga hoja. Hicho kichwa chake ni cha pekee Tanzania ukubali usikubali

Haaaswa uwezo wa kutafuta kiki. Ila hii ya mwisho karibu ingemtoa roho. Kiki ya kushambulia gari na yeye asiumie ikawa kupigwa risasi kabisa. Wenzake walimgeuka. Angefanya kama Nassari bila kuwashirikisha wanzake.
 
Tundu Lissu ni moja ya watu wenye akili sana kuwahi kutokea Tanzania.

Uwezo wake binafsi wa kiakili, ujasiri, uthubutu ndivyo vilivyomfikisha hapo..

Lowassa hawezi kuwa jeshi la mtu mmoja hata siku moja, Lowassa bila hela is nothing... Uwezo wa kifedha na kundi la mtandano ndivyo vilivyomjenga akiwa CCM na mtandano haukumtegemea yeye bali yeye ndiye aliutegemea mtandao aende ikulu, Mtandao ulisambaratishwa na JK na mwisho wa siku ukaja kumalizikia CDM..


Sasa kwa nini Tundu Lisu hana Hela? Au Lowasa alizaliwa nazo? Unamuona Tundu Lisu ana akili kwa sababu na wewe ni low IQ pia labda kakuzidi kidogo!

Mtu yoyote mwenye Intelligence ya kawaida kwanza hata mtoto wa Sekondari anapangua hoja za kitoto zote za Tundu Lisu!
 
Lowassa atawatoa roho ccm hivi si mumchukue tu lissu atabaki kuwa lissu
 
Lowassa ni Mlima Kilimanjaro
Na Lissu ni Kama Kilimanyege cha pale Morogoro store
Siasa ya Tanzania sio kupiga Kelele na Kama ingekuwa ni uwezo wa kupiga Kelele Lowassa na Kikwete wasingekuwa na Mafanikio ya Kisiasa kiasi kile
Risasi za nini sasa? Kama Lissu sichochote ?
 
Kamwe kabatini usilinganishe kazi ya sufuria Na umma kwa sababu vyote vimo kabatini.
LOWASSA ni kama umma uswahilini, tusipopika chips hauna kazi.
Kazi ya LOWASSA ilikuwa ni siku tulipopika chips 2015, Siku ya uchaguzi Na kazi yake iliishia hapo
Mbona kama kweli hivi ngoja nifanye hesabu zangu na mimi
 
Sasa kwa nini Tundu Lisu hana Hela? Au Lowasa alizaliwa nazo? Unamuona Tundu Lisu ana akili kwa sababu na wewe ni low IQ pia labda kakuzidi kidogo!

Mtu yoyote mwenye Intelligence ya kawaida kwanza hata mtoto wa Sekondari anapangua hoja za kitoto zote za Tundu Lisu!

Nani kakudanganya IQ kubwa ndio inaleta utajiri, namna ambayo Lowassa alizipata hela ukiondoa urithi wa ng'ombe kila mtanzania anajua na ndio namna pia wanaCCM wengine huzipata hela..

Hakuna aliyewahi kupangua hoja za TL zaidi yakumfungulia kesi alizoshinda kila siku, kama una akili ungepambana na jeshi la polisi lituambie nani alimpiga risasi TL ndani ya makazi yenye ulinzi na karibu kabisa na makazi ya naibu spika..
 
Back
Top Bottom