Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

JK alikosa Waislam wenye sifa za kuwa majaji kwa hiyo akaamua kuwateua hata wasio na sifa ili ku-balance dini za majaji. JK ni mdini sana.
 
Kamanda Lissu anasimamia katiba aliyoahidi kuilinda kwenye kiapo cha ubunge sasa akipeleka hoja ya kumchunguza rais mibunge mingi ya ccm itakwamisha hoja na pia mkwamo mwingine utaanza kwa Bi Kiroboto!

mkuu umenena. Tunao viongozi wachache kama Lissu hapa TZ wanaoweza kusimama na kutetea haki kama anavyofanya huyu ndugu. Wabunge wetu wengi ni bendera fuata upepo' hata hawajui kilichowapeleka bungeni.
 
Lissu amkomalia JK

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012

Aisee......huyu sio dada wa lile lijamaa?......Tanzania hii bana........lazima kutoka kwa kisiasa ndio ufanikiwe
 
Lissu amkomalia JK

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ameendelea kumwandama Rais Jakaya Kikwete, akisema baadhi ya majaji aliowateua hawana sifa, na kwamba viongozi wa serikali waliojitokeza kumpinga wameshindwa kujibu hoja.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana katika ofisi ndogo ya Bunge, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisema kuwa alishatoa maelezo hayo hata katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi.

“Nilieleza jinsi rais alivyofanya uteuzi wa baadhi ya majaji pasipo kupata ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wamekuwa wakijibu kiujumla, mimi niliwataja kwa majina yao na hata hili nilieleza katika Kamati ya Ngwilizi ambayo taarifa yake haikuwekwa hadharani pasipo sababu za kueleweka,” alisema.

Alisema wanaotaka kujibu hoja zake wanapaswa kuweka hadharani orodha ya majina ya majaji waliopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama kuanzia mwaka 2005 wakati Rais Kikwete alipoingia madarakani.

Lissu aliwataja baadhi ya watu waliowahi kujitokeza kumjibu kuwa ni Naibu wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, ambaye alisema kuwa serikali ina taarifa hizo na itazifanyia kazi.

Alisema kuwa msimamo huo ulikubaliwa na waziri wake, Mathias Chikawe na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, endapo serikali itachukua hatua ambazo alipendekeza watakuwa wanaingilia uhuru wa mahakama.

Wengine waliojitokeza kujibu hoja yake ni Jaji Mkuu, Othman Chande na Jaji Kiongozi, Faki Jundu ambao walisema kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni si za kweli.

Pia Rais Kikwete naye alikaririwa hivi karibuni akiwa jijini Arusha ambapo bila kumtaja Lissu kwa jina, alisema kuwa majaji wanateuliwa kwa kufuata utaratibu na wana sifa zinazostahili.

Ni kutokana na kauli hizo, Lissu alifafanua kuwa, katika hoja zake alisema kuna baadhi ya majaji waliteuliwa bila kuwa na sifa maalumu kama zilivyobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 109, kipengele cha 6, 7 na 8.

“Ibara hiyo ya 109 kipengele cha 6-8 kinasema; mtu anaweza kuwa Jaji iwapo tu ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kisheria, awe ameshakuwa hakimu, awe ameshakuwa wakili na kusajiliwa na sifa zote hizo ziambatane na utumishi wa miaka kumi mfululizo.

“Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa,” alisema.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

“Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?” alihoji.

Lissu aliwataja majaji wengine ambao wameteuliwa bila kuwa na sifa kuwa ni Fatuma Masengi, ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

Majaji wengine waliotajwa ni Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.

Lissu pia alimlalamikia Rais Kikwete kwa kutumia vibaya madaraka yake kwani anateua majaji wa mikataba, ambao wameshastaafu na kulipwa mafao yao.

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Kufuatia utata huo, Lissu emeendelea kushikilia msimamo wake kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili Bunge liweze kuchunguza utendaji wa rais kuhusu uteuzi wa majaji.

Lissu alisema Bunge litaangalia kama rais ameteua majaji kwa mujibu wa katiba au ameikiuka, na kwamba yeye ana uhakika kuwa rais amekiuka katiba.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012

Daah aiseeeeeee kumbe ni hivo wanfanyaga mhm
 
JK alikosa Waislam wenye sifa za kuwa majaji kwa hiyo akaamua kuwateua hata wasio na sifa ili ku-balance dini za majaji. JK ni mdini sana.

Sikubaliani nawe kwamba hapa alitumia udini,mimi nadhani kwa hawa majaji Fatuma Msengi na Latifa Mansoor alitumia uswahiba. Kuna waislamu wengi tu wenye sifa za kuteuliwa kuwa majaji lakini hawajateuliwa. Yule toka Zanzibar nimewahi eleza hapa kashfa ya uteuzi wa majaji iliyosababisha chama cha mawakili wa Zanzibar(ZLS) kuandika barua kwa rais Shein kupinga teuzi hizo.
 
mh.lissu naunga mkono hoja yako kabla ya kuwasilisha muswada binafsi bungeni kuhusu teuzi hizi ,kuna key persons . hawa wamekuwa wakizunguka na mafaili na kujenga hoja huyu anafaa huyu hafai wapo tumbane mh.ombeni sefue atoe majina yao na waeleze kwa nini walimshauri mh.rais vibaya .na kwa maslahi ya nani .vitumbua vyao tuviweke mchanga ili iwe funzo kwa wengine .kipindi fulani msafara wa rais mwinyi ulipotea njia kule tanga maeneo ya amani mhusika alijuta kwa alichofanya ....
 
[“Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa,” alisema.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

“Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?” alihoji.

Lissu aliwataja majaji wengine ambao wameteuliwa bila kuwa na sifa kuwa ni Fatuma Masengi, ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

Majaji wengine waliotajwa ni Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.
]

Ina maana tuna Jaji wa mahakama ya rufaa mwenye elimu ya diploma au cheti? Mbona vihoja!
Na mbona hili halijibiwi na hao majaji kwa kupinga kwamba elimu zao ni degree kamili na sio chini ya hapo badala yake wanapiga piga pembeni tu!
 
mkuu umenena. Tunao viongozi wachache kama Lissu hapa TZ wanaoweza kusimama na kutetea haki kama anavyofanya huyu ndugu. Wabunge wetu wengi ni bendera fuata upepo' hata hawajui kilichowapeleka bungeni.

mkuu wanajua kilichowapeleka ":tumbo zao na familia zao;"
 
Kwa wale wanaofuatilia mambo,inamaana tundu lisu ndie anaejua sheria kuliko watz wote?kama jibu ni hapana kwanini kama kuna ukweli na hao wengine mbona hawatoi ufafanuzi?tundu atakuwa ana wivu tu hana jipya.
 
Anyway' hii ndiyo tanzania tunayoitaka viongozi wetu hawana uwezo wa kuelewa hali halisi ikoje wanajidanganya na wanadanganyana. Janga la kitaifa tulilonalo sasa hivi ni kikwete na wenzake tusipolivalia njuga tukaliteketeza basi inawezekana mwisho wetu ndo sasa umefika. Namkumbuka kweli marehemu ebbo aliposema tanzania yote iuzwe na kila mtu apewe chake akatafute pa kuishi
 
Tundu, utapeleka bungeni sawa! Kumbuka kuna kisiki cha mama Makinda1 Haipiti ng'o!!!!!
 
Hata jaji mkuu othman Chande naye sifa zake zinautata sana, kwa mfano
1/Ushahidi wa kuchakachua umri(Kimahesabu inaonekana alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 4)
2/Uteuzi wake ulikuwa na mgongano wa kimaslahi na mkurugenzi wa TISS
 
Tundu na zito hawatofautiani kitu katika kujitafutia umaarufu binafsi,tofauti yao ni kuwa tundu anabebwa na dini yake mbele ya pro chadema,wanampenda na ujinga wake
 
Kikwete anadai anapelekewa majina na kamati ya mahakama. Anachorekebisha yeye ni kuangalia usawa wa kijinsia( na wa KIDINI kwa siri sana). KATIBA yetu ya JMT kwa sasa inatutesa sana kwenye teuzi hizi za Rais.

Kama alipelekewa tuu majina na kuchagua anayoona yanafaa, mtu unaweza kuchomekeza jina Mkenya na JK akiona linafaa basi atamteua kuwa jaji. Si anasema yeye anapelekwa majina tuu?
 
Tundu na zito hawatofautiani kitu katika kujitafutia umaarufu binafsi,tofauti yao ni kuwa tundu anabebwa na dini yake mbele ya pro chadema,wanampenda na ujinga wake

Hakuna cha kutafuta umaarufu hapa.

It is a naked fact kuwa Tanzania ina jaji kwenye mahakama ya rufaa ambaye hana shahada ya sheria kwa mujibu wa sheria mama ya Tanzania.

Inaonekana kuwa hii tabia ya kuengua vipengele vya sheria huwa haifanywi na mawaziri kama Kagasheki tuu, bali pia bosi wao.

Hata kama alipelekewa majina yeye ndiye appointee and he is responsible for the appointment.

Ili kuwaziba wapinzani kujitafutia umaarufu wa bei chee, basi serikali iache kufanya mambo ya kijingajinga kama haya.
 
Wana JF,

The list of incompetent judges is long. I am compiling the list with the supporting documents. To put the pants down of those who have replied to what Tundu Lissu said, soon it (the list of cincopetent judges) will be downloaded in this forum. Sioni mantiki ya kuteua majaji wengi (bila kufuata taratibu zilizopo) kama wanaoteuliwa wenyewe hawawezi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria. I am informed by a friend that a High Court judge delivered a ruling which contained no provision of the law to support his decision. Worse enough, where he was supposed to write the provision of the law to support his decision, this judge just left some blanks, but yet he signed the ruling and upon the same being requested by the aggrieved party, the same was issued to that party as it is (containing blanks in the places where the provisions of the law ought to have been sited).

Tatizo lipo kwenye mteuzi (appointing authority). He is taking our country to a deep grave as far as the administration of justice in Tanzania is concerned
 
Back
Top Bottom