Tundu Lissu awataja Majaji wa Kikwete wasio na Sifa (Kazi ndio inaanza)

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Lissu amkomalia JK

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ameendelea kumwandama Rais Jakaya Kikwete, akisema baadhi ya majaji aliowateua hawana sifa, na kwamba viongozi wa serikali waliojitokeza kumpinga wameshindwa kujibu hoja.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana katika ofisi ndogo ya Bunge, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), alisema kuwa alishatoa maelezo hayo hata katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi.

"Nilieleza jinsi rais alivyofanya uteuzi wa baadhi ya majaji pasipo kupata ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wamekuwa wakijibu kiujumla, mimi niliwataja kwa majina yao na hata hili nilieleza katika Kamati ya Ngwilizi ambayo taarifa yake haikuwekwa hadharani pasipo sababu za kueleweka," alisema.

Alisema wanaotaka kujibu hoja zake wanapaswa kuweka hadharani orodha ya majina ya majaji waliopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama kuanzia mwaka 2005 wakati Rais Kikwete alipoingia madarakani.

Lissu aliwataja baadhi ya watu waliowahi kujitokeza kumjibu kuwa ni Naibu wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, ambaye alisema kuwa serikali ina taarifa hizo na itazifanyia kazi.

Alisema kuwa msimamo huo ulikubaliwa na waziri wake, Mathias Chikawe na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambao kwa nyakati tofauti walisema kuwa, endapo serikali itachukua hatua ambazo alipendekeza watakuwa wanaingilia uhuru wa mahakama.

Wengine waliojitokeza kujibu hoja yake ni Jaji Mkuu, Othman Chande na Jaji Kiongozi, Faki Jundu ambao walisema kuwa tuhuma zilizotolewa bungeni si za kweli.

Pia Rais Kikwete naye alikaririwa hivi karibuni akiwa jijini Arusha ambapo bila kumtaja Lissu kwa jina, alisema kuwa majaji wanateuliwa kwa kufuata utaratibu na wana sifa zinazostahili.

Ni kutokana na kauli hizo, Lissu alifafanua kuwa, katika hoja zake alisema kuna baadhi ya majaji waliteuliwa bila kuwa na sifa maalumu kama zilivyobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 109, kipengele cha 6, 7 na 8.

"Ibara hiyo ya 109 kipengele cha 6-8 kinasema; mtu anaweza kuwa Jaji iwapo tu ana shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambuliwa kisheria, awe ameshakuwa hakimu, awe ameshakuwa wakili na kusajiliwa na sifa zote hizo ziambatane na utumishi wa miaka kumi mfululizo.

"Lakini sifa zote hizo lazima mtu anayeteuliwa kuwa Jaji awe nazo kwa miaka kumi mfululizo. Sasa badala ya kuzungumzia masuala hayo kwa ujumla jumla, ningependa wanaonijibu watamke wazi wazi Jaji Mbaruku Salumu Mbaruku alisoma chuo kipi na akapata shahada ya sheria iliyompa sifa ya kuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar kabla ya kuteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa hadi sasa," alisema.

Alishangaa viongozi wanaojitokeza kumjibu akisema hata Katiba ya Zanzibar 94 (3) inasema; ili mtu achaguliwe kuwa jaji, ni lazima awe na shahada ya Chuo Kikuu.

"Huyu jaji ambaye anasoma sasa alipataje kuwa jaji kabla ya kuwa na shahada ambayo ndiyo sifa ya msingi?" alihoji.

Lissu aliwataja majaji wengine ambao wameteuliwa bila kuwa na sifa kuwa ni Fatuma Masengi, ambaye kwa mujibu wa Lissu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Singida na baadaye akawa Hakimu Mkazi kisha akaanza kujisomea Chuo Kikuu Huria na kuhitimu mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa jaji mwaka 2006.

Alihoji kuwa kama katiba inaelekeza mtu awe jaji ni mpaka awe amekuwa hakimu kwa miaka 10, huyu alipataje kuwa jaji?

Majaji wengine waliotajwa ni Latifa Mansoor, ambaye pamoja na kuwa na shahada ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyotunukiwa 1993, lakini alifukuzwa kwa udanganyifu na ubadhirifu akiwa mfanyakazi katika Manispaa ya Ilala.

Kwamba baadaye alipoibuka mwaka 2008 aliteuliwa kuwa jaji wakati hajawahi kuwa wakili, na kwa kuwa alifukuzwa katika utumishi wa umma.

Lissu pia alimlalamikia Rais Kikwete kwa kutumia vibaya madaraka yake kwani anateua majaji wa mikataba, ambao wameshastaafu na kulipwa mafao yao.

Aliongeza kuwa, majaji wengine waliteuliwa na Rais wakiwa wagonjwa ili waweze kupata fursa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi, ambapo alimtolea mfano Jaji Mwendwa Malecela kuwa tangu ateuliwe mwaka 2006 hajawahi kusikiliza kesi hata moja. Badala yake Lissu alidai kuwa jaji huyo huenda matibabu India tu.

Kufuatia utata huo, Lissu emeendelea kushikilia msimamo wake kuwa anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili Bunge liweze kuchunguza utendaji wa rais kuhusu uteuzi wa majaji.

Lissu alisema Bunge litaangalia kama rais ameteua majaji kwa mujibu wa katiba au ameikiuka, na kwamba yeye ana uhakika kuwa rais amekiuka katiba.

Chanzo: Tanzania Daima | Nov 29, 2012
 

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,296
0
Si ajabu hao ni ndugu zake au waliwahi kuwa washikaji zamani Raisi wetu ni zaidi ya umjuavyo yeye kufuata katiba kuendesha nchi kwake ni tusi ,ashukuru watanzania wapole kama kondoo nchi zingine angekiona
 

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
Si ajabu hao ni ndugu zake au waliwahi kuwa washikaji zamani Raisi wetu ni zaidi ya umjuavyo yeye kufuata katiba kuendesha nchi kwake ni tusi ,ashukuru watanzania wapole kama kondoo nchi zingine angekiona
Halafu wote ni maswahiba . Ni wazi Kikwete ni janga la Taifa na mbaya sana amekwisha haribu system zote za serikali na uswahiba.
 

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,431
2,000
Bilisikiliza hotuba ya Arusha, JK alikuwa anaongea kama mtu asiye na uhakika na akisemacho kuhusu suala hili. Pia alikuwa anaongea kisiasa kuliko uhalisia.


Aweke ushahidi hadharani mfano LISSU amewataja baadhi ya majina, Sasa kama si kweli basi waweke hadharani vielelezo vya majaji hawa. Au wenyewe wajitokeze kukanusha kutokana na vigezo.

ACHENI BLABLABLa​


MIZAMBWA
nabii mtarajiwa!!!
 

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,129
2,000
Kwa jinsi hawa wote wanavyojibu hoja ya Lisu utadhani wameishia darasa la saba!
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,660
2,000
Tuache kando dhamira ya Tundu Lissu, ambayo watu wanauhuru wa kuitafsiri wanavyoona kama vile, anapiga debe kwa wivu ajili yeye hajateuliwa, ama ana kiherehere cha kutaka aonekane yeye anajua zaidi taaluma ya shieria, ama jamaa ana ubishi wa asili yake, ama ana uchungu wa dhat na wananchi wa Tanzania.

Lakini, tuone umuhimu na uzito wa hoja yake. Ni nin maslahi na nia ya kiongozi mkuu wa nchi, kufanya uteuzi wa nafasi kwa watu wasio na sifa wakati tasnia ina wataalam wenye sifa kibao?

Raisi anapoingia madarakani kwa kura za kuchakachua, na hatimaye ameendeleza wimbi la kuvunja sheria na kukiuka katiba ya nchi, huyu anapata wapi kiburi na dharau kubwa ya kiwango hiki?

Ni kwamba raisi huyu ni mbumbumbu kiasi kwamba haelewi kiwango cha madhara anayolisababishia taifa kwa uteuzi wake wa mawaziri na viongozi usiozingatia sifa na uwezo, na badala yake anazingatia mambo ya ovyo ovyo tu na unasaba na uswahiba?

Ni nini haki ya Watanzania kumdhibiti kiongozi kama huyu? Haki hizo ili wazipate wanahitaji kufuata taratibu zipi? Naona jamaa alishajua ni kelele za chura ndiyo maana ana kiburi na uziwi huku akiendelea kuibomoa nchi pasipo hofu wala aibu.

Najua tumechelewa lakini we can still do something rather than letting this guy to peacefully complete his evil mission. Tuelewe kwamba, usipoziba ufa utajenga ukuta na ukicheka na nyani lazima uvune mabua. Huyu jamaa na hawa washikaji wake, anatumaliza ndugu zangu.

Nawasilisha.
 

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Sasa kazi imekuwa safi, majaji wenye sifa tayari tunawajua, JK alisema yeye huwa analetewa tu majina, ila Jaji mkuu alisema wanasifa sasa ni kazi ya waandishi wa habari na watanzania wenye mapenzi mema na utawala wa sheria kuwahoji hawa majaji JK, Jaji mkuu nk kama wanasifa hawa majaji kama katiba inavyosema kutokana na uteuzi wao. Na kama hawana na waliteuliwa lazima watu kadhaa wawajibike na hukumu za kesi zao zote zitenguliwe na wote waliotiwa hatiani kuachiwa huru mara moja kwani walihukumiwa na watu wasio na sifa za kimahakama na uwezo unaotakiwa kwa kesi husika.

Sasa hii ni mahakani kwenye haki je huku kwetu namtombo kukoje??

Baba Kikwete tuhurumie sasa wanafunga kwa kukosa elimu na sifa za kazi. Kesho watamfunga Riz sijui ndio utujua ?? Ndio maana ndio mzee ni nyingi sana .
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Kikwete anadai anapelekewa majina na kamati ya mahakama. Anachorekebisha yeye ni kuangalia usawa wa kijinsia( na wa KIDINI kwa siri sana). KATIBA yetu ya JMT kwa sasa inatutesa sana kwenye teuzi hizi za Rais.

Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka.

Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.
 

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Mimi ningependa hao watumishi wa serikali kuanzia naibu waziri wa katiba na sheria pamoja na waziri wake, katibu mkuu kiongozi, jaji kiongozi na jaji mkuu na hata raisi kikwete mwenyewe wajitokeze na utetezi wenye kueleweka.

Kwakuwa Lissu amewataja kwa majina majaji wasio na sifa ya kuwa majaji basi nao wawataje kwa majina na kuthibitisha kwamba wana sifa za kuwastahili kuwa majaji.

Hapa ni kulazimisha CV zao ziwekwe wazi na sheria za teuzi ziwekwe wazi ili tumkome nyani giladi mchana na waache kelele na kejeli zao.
 

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,975
2,000
Kamanda Lissu anasimamia katiba aliyoahidi kuilinda kwenye kiapo cha ubunge sasa akipeleka hoja ya kumchunguza rais mibunge mingi ya ccm itakwamisha hoja na pia mkwamo mwingine utaanza kwa Bi Kiroboto!
 

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,698
2,000
Huyu JK Sijui atatufikisha wapi? Tuchukue hatua haraka iwezekanavyo.Tundu Lissu kaza uzi ili watu wengine wajue Urais si lelemama.

"Ukipewa kazi ya nchi lazima ujiheshimu"-Mwl Nyerere.
 

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,129
2,000
ungefafanua ingeonyesha nguvu ya hoja yako ila hapa wewe unaonekana ni chekechea
Acha uvivu wa kusoma,usiwe unachangia bila kusoma mada husika,ukisoma majibu ya jumlajumla yaliyotolewa na hao waheshimiwa kuanzia Rais,majaji wakuu wote na wengine hayaakisi hoja ya Lisu,ulitakiwa kurudi kwenye thread na kusoma majibu ya viongozi wako pasipo kutarajia mie niyarudie,acha kukurupuka jomba!
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,512
2,000
Tuwe na TUME safi za KITAALUMA. Watu waombe kazi hizi. Ifanyike vetting ya hali ya juu. Interview ziwe wazi kabisa. Wenzetu hapa Kenya sasa hata JAjiMkuu anaomba kazi kwa uwazi kabisa hadi TV zinaonyesha "live" mahojiano. Kenya wanatuacha sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom