Tundu Lissu asusia mkutano Dar

Padre Dr.Willbroad Slaa,kwanza niseme nashukuru kwamba Kiongozi wa Ngazi ya juu sana katika Chama cha siasa unakuwepo katika kuchangia mada hapa katika forum za nanmna hii,hivyo kutuliza na kukidhi kiu ya wachangiaji wengi ambao huhitaji majibu na misimamo ya jikoni,nikimaanisha kutoka Chamani,ambako wewe ni mmojawapo ya wawakilishi wa moja kwa moja.
Father,ningependa nitangulize imani yangu kabla sijasema nitakacho sema
NINAAMINI KWAMBA SI MARA ZOTE KILE NINACHOKIAMINI NDIO KIWE CHA KWELI AU SAHIHI
NINAJUA KWAMBA MARA NYINGI BINADAMU TUNACHUKULIA KWAMBA MISIMAMO YETU NDIO ILIYO SAHIHI ZAIDI,NA ILE YA WENZETU SI SAHIHI KWA SABABU TUNAONA KWAMBA SISI NDIO SISI TU
NIAAMINI KWAMBA MARA NYINGI MAMBO KAMA VILE YA DINI,SIASA,NA MAPENZI YANAENDESHWA KI-USHABIKI ZAIDI(i.e 1.shabiki wa Simba hata siku moja hatokiri wazi ama kushawishika kwamba Yanga ni wazuri kuliko wao,hata kama itokee mathalani Yanga anaongoza na Simba anashikilia nafasi ya mwisho ,ama kinyume chake 2.M Protestant ni vigumu sana kumwelewa mkatoliki pale mkatoliki anapomwambia m protestant "Hapana,sisi hatuabudu sanamu,bali tunasujudu",kwa sababu tu Mprotestant hamwelewi vema Mkatoliki)
NINAAMINI KWAMBA WATU WENGI DUNIANI WANAONA WAZAZI WAO NDIO WA MAANA ZAIDI DUNIANI KWA SABABU TU NDIO WATU WA KARIBU ZAIDI NA WAO,NI WATU WANAOWATATULIA MATATIZO YAO,NA NDIO WATU WALIOWAFAHAMU KI UKARIBU ZAIDI TOKA UTOTO WAO....INGAWAJE WAZAZI HAWA KWA WATU WENGINE WATAONEKANA HAWAFAI KABISA(inawezekana ikawa kweli hawafai ama ni mtazamo tu wa hao watu wengine)

Father,kwa kusema hayo juu,si nia yangu ukubaliane nami nitakachokwambia,bali ni nia yangu kukushawishi wewe na wengine kwama tunahitaji kujua kwamba katika nchi hii hakutakuja tokea siku watu wote wakawa na mawazo yaleyale kwa sababu hawa watu wanatoka katika familia tofauti,kabila tofauti,dini tofauti,kanda tofauti,(vyote hivi vinachangia sana mtazamo wa mtu katika kuchanganua jambo lolote maishani)......NINAOMBA TUFIKIE MAHALI PA KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA,hili ni jambo muhimu ili kuleta HESHIMA......JAZBA haitasaidia hasa pale tutakapoona mbona watu wanaonyesha kutokukubaliana na KILE SISI TUNACHOAMINI NDICHO CHA KWELI.....
HIVYO BASI;
NI VEMA UKAWASISITIZIA HAWA WANANCHI WALIO NA MSIMAMO WA UPANDE WA CHADEMA(sijui nimepatia hapa?au niseme msimamo wa mageuzi ya Katiba yanayoridhiwa na Chadema?au na vyama vya Upinzani?au na wana mageuzi ya katiiba?-niko tayari kusahihishwa,yawezekana nimekosea)kuacha KUZOMEA....na yule aliyesema kushangilia haikatazwi,naomba tuelewe kwamba katika saikolojia,Binadamu wote tuna hulka ya kupenda kusifiwa....NDIO maana nadhani tunaweza kubadilisha ujumbe wetu kwa KUWASHANGILIA wale wanaoongea tunachotaka,na kuwasikiliza na kukaa kimya kwa wale wanaoongea kile tusichotaka kukisikia......hili linahitaji UVUMILIVU,kwani saikolojia pia inasema mtu anapoongea kile usichotaka kukisikia,utatamani UMZOMEE,lakini kwa sababu ya kanuni ya KUHESHIMIANA ili kila mtu asikike,basi NI VEMA KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA,i mean kukaa kimya mtu anapoongea kile tusichokipenda ili kutokuonyesha tumemdharau.

Father,mara nyingi kwenye siasa ni viongozi wanaoelewa ki undani zaidi real OBJECTIVES,na wananchi wengi huwa wanaendeshwa na USHABIKI zaidi.
TUPUNGUZE USHABIKI ILI SUALA HILI LA KATIBA LIFIKIE MUAFAKA WA MAJORITY.
TUJUE KWAMBA KILA UPANDE UNAWEZA KUSHINDA KILE INACHOTETEA(WANAMAGEUZI WANAWEZA KUSHINDA,WENYE MSIMAMO MWINGINE WANAWEZA SHINDA)
Nawakilisha.ninajua yawezekana mawazo yangu si sahihi,kwani ninaamini katika kukubaliana kutokukubaliana.
Maoni yako ni mazuri kama ungeondoa iyo repetence ya mara Father,mara Padre,nyie manajidai mnazungumza honestly behind ananymous screen names, lakini mna nia ya kisiasa. Ofcorse mnataka wale wanachama wa CDM ambao si wakristo wajione wanaongozwa na Padre ama kiongozi wa dini ya wakristo.

Ningeomba mwongozo kwenye hili,kiutaratibu kwenye medani za kisiasa,kama mtu aliwahi kuwa Rais,basi hata akistaafu,si ajabu kusikia akiwa referenced as "president",na mara nyingi huelezwa kuwa ni mstaafu.Sasa kwa upande wa Dr Slaa,yeye tayari yuko kwenye siasa na upadre alishaachana nao.Hilo uliheshimu.Ningependa kujua kama mtu ukiachana na upadre kama unaruhusiwa kuitwa padre.Na kama si sahihi,basi ni bora tu umwite Dr Slaa,ama katibu nk.
 
Ni wazi na wewe unanguvu yako ya umma,basi tngeomba ujiweke wazi,naamini wewe ni CCM.

Natamani ungefungua macho yako ukajua hii si struggle ya vyama wala siasa, wala katiba, suala la katiba na vyama ni mapazia tu na upepo unaokuja ni mkali zaidi pazia hizi kuuzuia. Sina haja ya kujitambulisha kwani unajua dhahiri kuwa mawazo yangu yananinieleza zaidi mimi ni nani. Panua uzio wako uone mapambano yanayokuja.
 
Kuna watu huku mambwenkoswe wanauliza muswada ni kitu gani? Kwa nini huko mjini mnavutana? Mawasiliano huku ni tatizo. Naelimisha hawanielewi. Hamwezi kutusubiri?
 
Natamani ungefungua macho yako ukajua hii si struggle ya vyama wala siasa, wala katiba, suala la katiba na vyama ni mapazia tu na upepo unaokuja ni mkali zaidi pazia hizi kuuzuia. Sina haja ya kujitambulisha kwani unajua dhahiri kuwa mawazo yangu yananinieleza zaidi mimi ni nani. Panua uzio wako uone mapambano yanayokuja.
Inawezekana kuna habari amabazo unazo na hutaki kuziweka hapa licha ya kwamba uko annonymous.Ni vizuri ukatueleza huo upepo ambao ni zaidi ya stuggles ya vyama vya siasa na katiba ambao unakuja na pazia haliwezi kuuzia ni upepo gani huo?Vita?Umesema mko tayari kupambana,ninavyoelewa,mapambano ni ya katiba mpya kwa sasa,na ni wazi kuna mivutano baina ya vyma vya siasa kuhusiana na hili.

Ndio maana nikasema mchango wako unaonyesha wazi wewe si mwnanchi wa kawaida kama mimi na wengine wetu humu.
Kama unadhani kuna kitu kinakuja zaidi ya haya madai ya katiba na struggle between the political parties,then are you trying to imply kuwa CDM wana vikosi vya kupigana ie rebels?
 
Inawezekana kuna habari amabazo unazo na hutaki kuziweka hapa licha ya kwamba uko annonymous.Ni vizuri ukatueleza huo upepo ambao ni zaidi ya stuggles ya vyama vya siasa na katiba ambao unakuja na pazia haliwezi kuuzia ni upepe gani huo?

Ndio maana nikasema mchango wako unaonyesha wazi wewe si mwnanchi wa kawaida kama mimi na wengine wetu humu.
Kama unadhani kuna kitu kinakuja zaidi ya haya madai ya katiba na struggle between the political parties,the are trying to imply kuwa CDM wana vikosi vya kupigana ie rebels?

For once unaweza kutanua your horizon and think beyond CHADEMA and CCM?
 
For once unaweza kutanua your horizon and think beyond CHADEMA and CCM?
Jibu,mko tayari kwa mapambano gani kama si haya ya katiba mpya?Ama unataka nirudie rudie vitu ambavyo umebandika wewe.
 
Jibu,mko tayari kwa mapambano gani kama si haya ya katiba mpya?Ama unataka nirudie rudie vitu ambavyo umebandika wewe.

Nimekwisha jibu mwanzo, nasi tupo tayari kutumia nguvu ya umma, just as you know peoples power is not limited to Slaa, Mbowe and Lisu only. Tutapambana kwa lolote watakalo taka, na nakufahamisha tumekwisha anza kupambana.
 
Mkuu nyie mnatumia nguvu ya dola,na sometimes nguvu ya vurugu za watoto kama ilivyojitokeza.
Ndio maana nikajiuliza ulimaanisha nini pale uliposema si struggle za vyama vya siasa wala katiba mpya.Naamini hii ni struggle ya kutaka mabadiliko.
 
Wait and see brother, mshukuru mungu unaishi nyakati za kuzaliwa upya taifa letu.
 
Wait and see brother, mshukuru mungu unaishi nyakati za kuzaliwa upya taifa letu.
Mkuu ukweli ni kwamba upande utakaoshinda ni ule upande wenye passion ya kweli.Si umeona hiyo nguvu ya umma ya kupachika matokeo yake ni usingizi?Nguvu ya umma ya wenzenu ni ya umma kikweli kweli,wao wanachofanya ni kuwa guide tu,na pengine muwashukuru otherwise wananchi hao gadhabu yao ni valid na msipowasikiliza mnategemea nini?
Nguvu ya umma wa kupachika haina nguvu FYI.
 
Mkuu ukweli ni kwamba upande utakaoshinda ni ule upande wenye passion ya kweli..

Nadhani ni mapema zaidi kuongelea upande utakaoshinda kwa sasa, lakini yote heri kwani kila upande utakuwa umetekeleza wajibu wake wa asili(kupigana). Hali ilivyo sasa mnaambiwa nguvu ya upande wenu tu, viongtozi wenu hawajawaambia nguvu ya upande wa pili. Matokeo yoyote yataibadilisha nchi hii na pengine makundi yanayodharauliwa sasa yataheshimiwa hata baada ya mapambano regardless yatakuwa yameshinda au kushindwa. Nashukuru mungu nipo upande unaojua kuwa mapambano haya hayatuhusu sisi na upepo bali na watu wenye dhamira zao. MAPIGANO YAMEANZA NASI TUMESIMAMA.
 
Nguvu ya upande wa pili ni nguvu ya dola hilo halina ubishi.Nguvu ya umma ni tofauti na nguvu ya dola na mobilised gangs planted to instigate unrest ama kuvuruga taratibu kama mlivyowakusanya hao watoto wenye njaa na kuwajaza kwenye mjadala muhimu wa kitaifa,yote hayo kwasababu mnajua mnashindwa,the noose around Tanzania peoples' neck is slowly but surely loosing up.The noose of Mafisadi around our neck is loosing up.We willl be free because we want, trust me on this.Hiyo nguvu yenu si nguvu ya umma.
 
Nguvu ya upande wa pili ni nguvu ya dola hilo halina ubishi.Nguvu ya umma ni tofauti na nguvu ya dola na mobilised gangs planted to instigate unrest.

I wish ningejua unachotaka kumaanisha hapa, lakini haijalishi utaiita kwa jina gani, hakutakuwa na mapambano ya upande mmoja kama mnavyo aminishwa.
 
Haa haaaaa! Uliwauliza juu ya umri wao ndugu? Ukitaka kujua kama Serikali iko serious na utoaji maoni ulio huru katika Muswada huu soma kifungu cha 28 (2) na (3) cha Muswada: "28 (2) For the purposes of subsection (c) paragraph (1) the referendum campaign shall be conducted by the Commission and no political party or affiliate organization to a political party shall participate in a referendum campaign.
(3) A person who contravenes the provisions of subsection (2) commits an offence and on conviction be liable to imprisonment, without fine, to a term not exceeding two years."

Kifungu hiki kina jambo la ajabu sana: Kwamba eti Tume iliyokusanya maoni ndio ifanye Kampeni yenyewe, sasa hapo unategemea nini? Si watafanya kampeni kuvutia kile wanachoamini? Na endapo mtu mwingine anafanya kampeni eti linakuwa kosa la jinai! Sasa hapa ukiambiwa kuwa CCM/Serikali imepeleka watoto ili kukaba nafasi za watu wenye uchungu na uelewa wa mambo ya nchi yao utashangaa?

Imepata nguvu ya Bunge na Rais kuwa sheria kamili?!
 
I wish ningejua unachotaka kumaanisha hapa, lakini haijalishi utaiita kwa jina gani, hakutakuwa na mapambano ya upande mmoja kama mnavyo aminishwa.
Ndio maana nikasema unaandika kwa ushabiki zaidi na inaonekana una hasira kweli kweli na CDM, no wonder you cant comprehend.Ni umma gani huo mnaodai mtatumia nyie ccm?Hamna nguvu ya umma ccm,ni nguvu ya dola ambayo mnaitumia dhidi ya umma,umeelewa sasa?
 
Nafikiri VITA itatua Tanzania hivi karibuni na damu ya watu itamwagika.

Ila akina Gbabo wa Tanzania watajulikana na watawindwa na ICC hata wakijifanya kukimbilia Uarabuni.

Huko Uarabuni kwenyewe mambo yanachemka.

Ujinga wa watu wengine dunia hii ni kuwa wakisikia wengine mambo yanawaka, wanaona wao hayo hayawahusu. Mrusi na Ubabe wake na vyombo vya hali ya juu na vyombo vikali vya ulinzi kama KGB, ALFA, Red Army...... walishindwa na nguvu ya UMMA na wakajifia na Ukomist wao, itakuwa CCM?

Wakati ni UKUTA na mkitaka kupigana nao, mtaangamia.

Kama mkitumia njia za KUUWA watu na hasa waandamanaji, mambo yatakuwa kama Syria. Mkiniuwa mie kama Mkristo, mtashangaa kuwa kumbe familia ya SIKONGE ni kubwa sana na ina waislaam wengi zaidi ya Wakristo na hao wote wataungana kama familia na kuanza kuandamana kuwapinga. Kidogokidogo MOTO utazidi kula nyasi na kuwa mkubwa zaidi na zaidi.

Ingelikuwa ni BUSARA zaidi kwa future ya Taifa letu, mngelifanya haya MABADILIKO kwa amani. Ubaya zaidi ni kuwa kuna watu kama hawa akina Tambwe Hiza mambo yakiharibika, hawatakuwa hata na pa kukimbilia. Akina Kikwete, Rostam, Lowassa, Chenge, Mkapa, Mwinyi nk wanamajumba yao nje ya Tanzania na mapesa ya kutosha kuishi huko.

Tutabaki wenyewe kwa wenyewe TUKIMWAGA damu zetu huku hao waanzilishi wakikimbilia MAJUU.

Ila ukweli unabaki palepale kuwa TANGU ENZI ya AGANO LA KALE, AMANI IMEKUJA KWA DAMU.
 
Nadhani ni mapema zaidi kuongelea upande utakaoshinda kwa sasa, lakini yote heri kwani kila upande utakuwa umetekeleza wajibu wake wa asili(kupigana). Hali ilivyo sasa mnaambiwa nguvu ya upande wenu tu, viongtozi wenu hawajawaambia nguvu ya upande wa pili. Matokeo yoyote yataibadilisha nchi hii na pengine makundi yanayodharauliwa sasa yataheshimiwa hata baada ya mapambano regardless yatakuwa yameshinda au kushindwa. Nashukuru mungu nipo upande unaojua kuwa mapambano haya hayatuhusu sisi na upepo bali na watu wenye dhamira zao. MAPIGANO YAMEANZA NASI TUMESIMAMA.

Ha ha haaa! Nchi hii haiishiwi vibwengo.

Karibu kitimoto hapa Rainbow (Mbezi) leo Jumamosi.
 
Ndio maana nikasema unaandika kwa ushabiki zaidi na inaonekana una hasira kweli kweli na CDM, no wonder you cant comprehend.Ni umma gani huo mnaodai mtatumia nyie ccm?Hamna nguvu ya umma ccm,ni nguvu ya dola ambayo mnaitumia dhidi ya umma,umeelewa sasa?

Kwanza ni lazima ujue mimi sijawahi kuichukia CDM wala sina pango wa kufanya hivyo mbele, ila kama ukiniuliza kama kuna watu nawachukia huko CDM nitakujibu NDIYO. Pili mimi ninapenda tujadili suala hili mbali zaidi ya CDM na CCM a hata kama unadhani ni vyema kulichambua suala hili kiCCM na CDM kwani huji kuwa CCM ina UMMA wake? Hujui wapo waliopewa fursa ya kuichagua CDM na CCM wakaichagua CCM? Hao walioichagua CCM ndio watakaosimama na CCM. Kwa bahati mbaya haitakuwa hivyo kama nilivyokuambia awali hayatakuwa mapambano ya uCCM na uCDM. Usije kuingizwa kenye mapambano usoyajua jaribu kuangalia uliposimama
 
Wliolala wanaonekana ni wengi,kushiriki kwenye mjadala si mbaya,ubaya unakuja pale ambapo walikwenda kwa maelekezo ya kuziba nafasi ya wengine ambao wangeweza kuchangia kuliko wao,huu usingizi ni ishara kwamba huenda ni kweli waliamshwa mapema,hapo walipo wanafidia mda ambao hawakulala!
 
Back
Top Bottom