Tundu Lissu asusia mkutano Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu asusia mkutano Dar

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by nngu007, Apr 9, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 09 April 2011

  MJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Tundu Lisu, jana alitoka ndani ya ukumbi wa mkutano kuhusu mjadala wa maoni wa muswada wa sheria ya mapitio ya katiba, kwa madai kuwa kulikuwa na kundi la watu waliokodiwa kuvuruga mchakato huo.

  Lisu alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutoka nje ya kumbi wa mikutano wa Karimjee, kufuatia kuwapo kwa kundi la watu waliokuwa wakuzomea wachangiaji wa mjadala.

  Akiwa nje ya ukumbi huo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kundi hilo lilikodiwa na CCM kwa lengo la kuvuruga mchakato huo, ili usifanikiwe.


  Tundi pia aliwatupia lawama polisi katika Kanda Maalamu ya Dar es Salaam, kuwa wamekuwa katika katika eneo hilo, kwa lengo la kulinda kikundi hicho kilichokuwa kinafanya kazi ya kuzomea wachangiaji, waliokuwa wakikosoa muswada.

  "Jana (juzi)tulikubaliana kwenye kikao cha kamati kuwa ulinzi katika mkutano wa leo (jana) ungeimarishwa na mtu yeyote atakayebainika kuwa anazomea au kuzuia maoni ya watu wengine kutolewa, polisi wangemtoa nje ya ukumbi, lakini kinchofanyika leo ni tofauti kwa sababu polisi wanawalinda wanaofanya vurugu," alisema.

  Lisu pia alipinga muswada huo kwa maelezo kuwa una mapungufu mengi na kwamba hakuna

  sababu ya kuupeleka bungeni kujadiliwa, kwa utumia hati ya dhararu.

  Kwa mujibu wa Lisu, muswada huo ulipaswa kufuata njia ya kawaida ya kutunga sheria na si kwa hati ya dharura.


  Alisema haiwezekani kwa muswada ambao ni mali ya wananchi na roho ya taifa, kujadiliwa ndani ya siku tatu na kupitishwa.

  Alisema sababu nyingine ya kupinga muswada huo, ni vipengele vilivyopo ndani yake ambavyo alisema kwa maoni yake, vinakandamamiza uhuru wa watu kushiriki katika kutunga katiba.

  Alisema kwa hali ilivyo, mjadala huo ulioandaliwa kwa siku chache hautakuwa na manufaa kwa wananchi na kwamba badala yake, utatengeneza manung'uniko kwa wananchi.


  Alipoulizwa kuhusu hatua ya Lisu kutoka nje ya ukumbi, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Pindi Chana, alisema hawezi kulizungumzia hadi kwanza apate sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo.

  "Mimi muda huu siwezi kuzungumza chochote mpaka niwe na ushahidi wa kile kilichomfanya atoke ndani ya ukumbi wa mikutano,"alisema Chana.


  Katika mjadala huo wadau mbalimbali waliochangia walipinga baadhi ya vipengele vya muswada kwa maelezo kuwa vinavunja katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 2. koo

  koo JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo na makamba anajidanganya kwamba anaweza kupambana na chadema kamuagiza mwenyekiti wa uvccm kuandaa mpango wa kupambana na chadema kila kona na eti wameomba usalama wa taifa kuhakikisha wanawajulisha mbinu zote za chadema kabla hazijatekelezwa. Jamani tuwe tayari kwa mapambano wabunge wetu tuko tayari tunawasubiri.
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Mbona wa CCM na UDP walizomewa Chuo Kikuu, hakuna aliyesusa? Hawa Chadema wamezowewa kidogo tu wanajidai kususa. Wazomee wao tu, wakizomewa wanasusa. wakishindwa kura wanasusa, wakoje hawa?
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Hao watoto walibana nafasi watu wenye mawazo pevu wasiingie kujadili katiba.
   
 5. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  huu utani sasa, kuweka watoto karimjee, kwa nini wasingewafuata huko mashuleni, Mi nadhani tungepunguza utani kwenye mambo ya msingi kama hili la Katiba.
   
 6. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Jana Mboe Mwnyekiti wake kasema kama kushangilia sio kosa iweje kuzomea iwe kosa? au Tindu hajamsikia Bosi wake? ishu ya watoto haipo as wote inaonekana ni above 18 years, mbona kwenye maandamano wanakusanywa? kama issue ni kulala wameiga viongozi wao pale bungeni kila siku wanauchapa, hata Ngeleja keshauchapa mkutanoni mbele ya JK kule paris.
   
 7. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  napenda zomea zomea iendelee kwa wote maana inaonesha ni namna gani watanzania tunaweza kujadili!!! Inaonesha namna gani tunaweza na kumudu majadiliano!!! Inaonesha ni upeo kiasi gani tulio nao, hakuna haja ya kukemea zomeazomea!! Nadhani ni aina ya watanzania kujadili mambo!!! Zomeazomea ni burudani tosha na ni funzo pia kwa wanaopenda zomeazomea!!

  Zomeaneni siku zipite tupate katiba mpya itakayokuwa 'nzuri' kwa sababu zomeazomea itakuwemo!

  Wanasiasa wa nchi hii si makini, na ndilo linapelekea na wananchi kuwa kama wao. Hapo usisahau na serikali yenyewe!!!
  Woote ni kama pipa na mfuniko wake!!
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haa haaaaa! Uliwauliza juu ya umri wao ndugu? Ukitaka kujua kama Serikali iko serious na utoaji maoni ulio huru katika Muswada huu soma kifungu cha 28 (2) na (3) cha Muswada: "28 (2) For the purposes of subsection (c) paragraph (1) the referendum campaign shall be conducted by the Commission and no political party or affiliate organization to a political party shall participate in a referendum campaign.
  (3) A person who contravenes the provisions of subsection (2) commits an offence and on conviction be liable to imprisonment, without fine, to a term not exceeding two years."


  Kifungu hiki kina jambo la ajabu sana: Kwamba eti Tume iliyokusanya maoni ndio ifanye Kampeni yenyewe, sasa hapo unategemea nini? Si watafanya kampeni kuvutia kile wanachoamini? Na endapo mtu mwingine anafanya kampeni eti linakuwa kosa la jinai! Sasa hapa ukiambiwa kuwa CCM/Serikali imepeleka watoto ili kukaba nafasi za watu wenye uchungu na uelewa wa mambo ya nchi yao utashangaa?
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Hii katiba inawahusu zaidi hao watoto, na ni uongo waliosema wamekodishwa hao walipelekwa masomo kwa vitendo, ni kawaida kabisa, hata bungeni huwa tunaona wakipelekwa! Msitafute sababu zisizo na maana.

  Jee, mnataka kusema kuwa watoto hawana haki nchi hii?
   
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hawa watoto waliokodishwa kwenda kula usingizi kwenye ukumbi wa Karimjee au unazungumzia watoto wepi ndugu?
   
 11. g

  gepema Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Majimshindo wewe ni mpumbavu wa mwisho hivi unaweza kutetea upuuzi huu,hawa wahuni(watoto) unaweza kweli kusema kwamba ni wanafunzi ambao wapo kwenye masomo ya vitendo? Wachafu,wamevaa shabeshabe halafu unataka kusema nini?!!
  Jaribuni(CCM) kutumumia ubongo kufikiri badala ya unyayo
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Watoto wanahaki sawa kama babu, kwanza wanasoma civics kwa vitendo kama ni swala la kukodisha ccm walimkodi Tambwe , chadema nao walikodi Slaa kuwakilisha mawazo ya chama.

  Tatizo linakuwa palepale, wenye makosa ni wale walioanzisha kuzomea wenzao, binadamu inabidi kuheshimu mawazo ya mwezako hata kama wewe unayona ni ya kipuuzi. Na unapoona hivyo na mwezako pia anayoana mawazo yako ni ya kipuuzi. kwa hiyo mkubaliane kuzomeana. Haiwezekani wewe uzomee tuuuu harafu kinyume chake kisiwe sahihi.

  Mimi nawashangaa hawa viongozi, wanashindwa kuelewa tu ya kwamba mnapotofautiana kimawazo kila upande kwa mawazo yao huona wako sahihi kwa asilimia 100% na kila upande huona upande mwingine ni wenye mawazo ya kipuuzi. Hivyo basi, muungwana hunyamaza na kuondoka, lakini uki opt kuzomea eti kwa sababu mawazo yake umeyaona ni ya kipuuzi ndivyo hivyo naye atazomea maana atakua anaamini kabisa nawe ni u mpuuzi.
   
 13. M

  Mwanaume Senior Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  why masomo kwa vitendo, then wanakaba nafasi za sensitive contributors? Kama ndivyo, si wangepewa viti vyao tofauti na hivyo ili wakae kama listeners wakiwa pembeni?
   
 14. k

  kamalaika Senior Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  chadema ni chama makini. Mtu yeyote ambae hafikiri kwa maslahi binafsi atakubaliana na mimi. Chadema hakiwezi kuzomea kwenye mikutano it is way above that
   
 15. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kilichofanyika jana ni upumbavu na aibu kubwa kwa taifa, ni ujinga tu.
   
 16. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mbona Lissu hakutoka nje wakati Tabwe anazomewa mpaka wakahairisha mkutano, tuwe wauungwana kwa kuheshimiana kwanza.
   
 17. k

  kamalaika Senior Member

  #17
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  CCM mnapesa za kuchezea mngewekeza kwenye elimu, afya, michezo tungekuwa mbali sana.

  Ukiwauliza hao watoto mjadala ulikuwaje nn kilizungumzwa hawatakuambia kitu maana wamepiga mbonji wengi wanadai waliamshwa saa 11 usiku kuwahi kubana nafasi ukumbini.
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 12,009
  Trophy Points: 280
  Hata kama watoto wana haki sawa lakini kuna maamuzi mengine lazima yafanywe na watu wazima au wazazi wao kwa manufaa yao. Lissu was right to walk out huwezi kujadili mambo ya msingi na watoto tena waliolala kwa kisingizio cha haki sawa.

  Hizi mbinu wanazofanya CCM zilifanywa na nchi mbalimbali lakini hazikufanikiwa matokeo yake waliokuwa wanazuia waliishia jela(Kenya).

  [​IMG]
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wewe ni mtu wa ajabu sana...kukaa kimya pia ni hekima............jana palikuwa na watot wa kuanzia miaka 11 hadi 17........kama huna uwezo wa kuweka hoja zenye mashiko au unachangia kwa ushabiki basi wewe hufai na hujui nini unakizungumza
   
Loading...