Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Interesting...
Mzee alikuwa jasiri sana.
Pumzika kwa amani.
Sana mtu kuwekwa kizuizini kwa sababu tu ya kuwa na mawazo tofauti kuhusu Muungano hapa Mwalimu alichemka. Mzee amefariki na sononeko la nafsi .Wacha apumzike.
 
Duh Mzee wa watu kajifia na kinyongo kikubwa lakini laana ya kuwauza wazanzibar iliendelea kumtafuna hadi mauti yalipomkuta.

Mzee A Jumbe alikubali kuziunganisha TANU na ASP kwasababu aliamini Mwl Nyerere angempachika uRais wa JMT.Katika uhai wa muungano hakuna Rais wa Zanzibar aliyefanya ziara nyingi katika mikoa ya Tanganyika kama Mzee Jumbe hakuna na wala hatakuja kutokea hata siku moja.Inaelekea Mwl Nyerere alimwandaa lakini kuibuka kwa Marehemu Sokoine Waziri Mkuu wa wakati wake kulififisha ndoto za Jumbe kuchukua mikoba ya Mwl Nyerere ambaye tayari alishajiandaa kuondoka ikulu ya magogoni kilichochelewesha ni vita ya Kagera ilibidi Mwl aongeze muda kidogo.

Baada ya Jumbe kuona nyota ya Sokoine inazidi kuwaka akaanzisha madai ya kumezwa kama si Sokoine ambaye tayari alionekana wazi angechukua mikoba Jumbe asinge piga kelele wala kuleta madai ya kumezwa.Wakati TANU & ASP zinaunganishwa alijua wazi Zanzibar ingemezwa lakini tamaa ya madaraka ya wakati huo ilimnyamazisha.

Wale wote wanaomshabikia Jumbe wajiulize ni kwanini alikubali kuunganisha TANU & ASP halafu akaja kuikana baadae.Nini ilikuwa sababu ?????.
Mkuu
Ngogo infact umetoa uchambuzu mzuri usio biased wala uongo bali unatoa mwanya wa watu wenye akili timamu wafikirie na kuhoji vitu vya msingi .hongera mkuu

Mi nadhani jumbe asilaumiwe kwa matokeo ambayo ni kuiunganisha asp na tanu..alifanya hivo huwenda alikuwa influence..why nasema hivi?
Tujiulize nani aliempigia chapuo kama si kumuweka kwenye hiko kiti iko wazi ni nyerere..alichofanya jumbe ni kujaribu kufight within system kitu ambacho kwa namna fulani alifanikiwa lakini kwa sehemu kubwa alishindwa ..kulikuwa na wapiganaji wakubwa sana kuikomboa zanzbar kutoka kwa mkoloni nyerere wengi wao wakiuawa eidha kwa kufitinishwa au kutafutwa na majasusi...mimi nitamkosoa sana marehemu nyerere juu ya zanzbar...
 
Hivi kwani kama muungano ni hiari kwanini Tanzania unalazimishwa na dola au kuna umuhimu ambao amabao hatupo kwenye system hatuuoni?
Mkuu
Sababu utashangaa..kwa mfano ulimsikia lukuvi kwenye video moja akiongea kanisani yaan ile ndo uchonganishi wa kidini..anasema zanzbar wakaz wake 98%..ni waislamu kwa ivo ukiwaachilia uhuru watatangaza kuwa ni taifa la kiislam kwa ivo magaidi wataweka kambi zanzbar ambayo ni tishio kwa tanganyika

Hiyo ndo kauli ya waziri mwenye dhamana kabisa...kwa hiyo wazanzbar wanatawalia na mkoloni ccm kwq sababu ya uislam wao..
 
Sana mtu kuwekwa kizuizini kwa sababu tu ya kuwa na mawazo tofauti kuhusu Muungano hapa Mwalimu alichemka. Mzee amefariki na sononeko la nafsi .Wacha apumzike.

Jumbe kilichomponza inaonekana ni kutunishiana mzuli na Mwl Nyerere. Utaona Jumbe aliongoza kama raisi Zanzibar kuanzia mwaka 1972 mpaka 1984 ni miaka takribani 12. Miaka 12 kwa watawala wengi wa kiafrika wanakuwa na kiburi cha madaraka pengine japo hatuna uhakika ndicho kilichomkuta mwanamapinduzi huyu nguli pia. Kitendo cha yeye kuajiri mwanasheria mkuu wa Serikali raia wa kigeni bila kumshirikisha mkuu wake wa kazi ambaye kwa wakati huo alikuwa raisi wa muungano Mwl Nyerere ni kosa kubwa ambalo Jumbe amefanya hilo pekee lilitosha kumvua nyazifa zote alizokuwa nazo. Kama hiyo haitoshi labda na hizo document za maandiko yaliyokuwa na dalili kwamba alikuwa anajipanga ku sabotage muundo wa serikali ambayo yeye anatumikia -- labda wataalamu wa mambo ya usalama au ulinzi watatuambia hiyo imekaa vipi? Kama kufanya hivyo ilikuwa ni threat kwa ulinzi na usalama wa nchi kwa nyakati hizo it was obvious kwamba ilikuwa lazima iwepo mechanism ya kumdhibiti ikiwemo hiyo ya kumuweka kizuizini. Kuna mengi hatuyajui maana nakumbuka historia tuliyokuwa tunasomeshwa mashuleni ilimtaja Jumbe alikuwa raisi wa Zanzibar na baadae akajiuzulu basi -- haisemi zaidi kwann alijiuzulu nk. nadhani mambo mengi wakati huo yalikuwa ni siri na yalikuwa yakifichwa. Sababu hata CIA huwa baada ya muda wakishaona jambo lililokuwa siri halina tena madhara hata likitolewa hazadhani huwa wa expose nadhani na hili lilishapita kwa hiyo wajuzi wa mambo kama hakuna madhara kutujuza tujuzeni jamani.
 
Back
Top Bottom