Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
sasa wewe si uyaandike hayo ya seif au mpaka uandikiwe?
 
.

Nimeipenda sana comment yako hii...hapo ndipo unafiki wa wanasiasa unavyojionyesha wazi...Tundu Lissu hajasema chochote cha maana katika andiko lake...ameruka makusudi kuwataja wanasiasa waliomtumbukiza Jumbe mtegoni...Ndiyo maana mimi siasa sipendi kabisa....Lissu angefanya cha maana kama angewataja wote waliomhadaa Jumbe lakini kwenye kikao cha NEC wakaingia 'mitini'...Tundu Lissu asituambie chochote kuhusu suala hili baadhi yetu tunajua sana kilichotokea na hatuwezi kuweka hapa mambo hayo....Watu wanafiki sana, tena sana...naishia hapo...inaudhi sana
sasa na wewe si ukamilishe au ndio
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Hii ni eulogy kwa ajili ya hayati Mzee wetu Aboud Jumbe. Kwa nini unataka Maalim Seif atajwe/azungumziwe?
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Kwani na Maalim Seif Shariff Hamad amefariki?
 
HII NDIO TUNU KATIKA TANZIA YA ABOUD MWINYI JUMBE

IMESAMBAZWA KWENYE MEDIA NA Comred Mbwana Allyamtu

Imeandikwa Na Mhe Tundu Lissu

Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia. Akiwa na miaka 96, Jumbe aliishi muda mrefu sana kwa kigezo chochote kile. Alikuwa mwasisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya January 1964.

Alikuwa pia mwasisi wa Muungano ulioizaa Tanzania miezi michache baadae. Baada ya Sheikh Abedi Amani Karume kuuawa mwezi April 1972, Jumbe aliteuliwa kuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, na alishikilia madaraka hayo hadi January 1984. Wasomi wa Muungano wameandika kwamba wakati Karume anauawa mahusiano yake na Mwalimu Nyerere yalikuwa yameharibika kiasi kwamba Jumbe (kwa upande wa Zanzibar) na Bhoke Munanka (kwa upande wa Tanganyika) ndio walikuwa kiunganishi cha mawasiliano kati ya Mwalimu na Karume. Hii pengine ndio sababu Mwalimu alitumia ushawishi wake kuhakikisha Jumbe anateuliwa kumrithi Karume.

Hata hivyo, Jumbe atakumbukwa zaidi na historia kwa upinzani wake kwa mfumo wa sasa wa Muungano kuliko, pengine, kwa jambo jingine lolote. Jumbe alikuwa mwanasiasa wa kwanza, baada ya era ya Karume, kutambua kwamba muundo wa serikali mbili ulikuwa umeipokonya Zanzibar mamlaka yake na kuyahamishia Tanganyika. Alikuwa wa kwanza kutambua kwamba kuzaliwa kwa CCM, katika context ya Muungano, kulimaanisha mwisho wa mamlaka yaliyokuwa reserved kwa Zanzibar chini ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

Sio tu alitambua bali pia Jumbe alichukua hatua kupinga Zanzibar kupokonywa mamlaka yake hayo. Ili kufanikisha azma yake, Jumbe alilazimika kumwachisha kazi Mwanasheria Mkuu wake aliyempewa na Mwalimu Nyerere, Damian Lubuva, na kumwajiri Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, raia wa Ghana, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Kwaw Swanzy ndiye aliyeandaa 'hati ya mashtaka' dhidi ya Muungano iliyokamatwa na watu wa usalama wa Mwalimu na baadae kutumika kumsulubu Jumbe kwenye kikao cha NEC ya CCM Dodoma January 1984.

Kwa sababu ya upinzani huo, Jumbe aling'olewa madarakani pamoja na Waziri Kiongozi wake Ramadhani Haji Faki na Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy alitangazwa persona non grata na kufukuzwa nchini. Mwalimu akatangaza 'kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa' Zanzibar na waZanzibari wengi wapinzani wa Muungano, kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza Wolfgang Dourado, kuwekwa kizuizini. Miaka kumi baada ya kuondolewa madarakani, Alhaj Aboud Jumbe alichapisha kitabu chake juu ya Muungano, 'Miaka Thelathini ya Dhoruba', ambako aliweka bayana ugomvi wake na Mwalimu juu ya Muungano.

Jumbe ni kiongozi pekee wa juu wa rika la wapigania uhuru wa Tanzania kuandika memoirs zake juu ya Tanzania na matatizo ya Muungano wake. Hata Mwalimu hakufanya hivyo na alikufa na siri zake juu ya mambo mengi makubwa yalitokea wakati wa utawala wake. Kwangu mimi, hii ndio merit kubwa na mchango mkubwa wa Alhaj Aboud Jumbe kwa kizazi cha sasa na vijavyo vya waTanzania. Alikuwa na ujasiri wa kusema na kuandika juu ya 'The Forbidden Subject', tena katika kipindi cha Mwalimu Nyerere ambapo ujasiri wa aina hiyo ulikuwa ni jambo la hatari kubwa. Kwa sababu hiyo hiyo, Jumbe alilazimika kuishi theluthi ya mwisho ya maisha yake 'kifungoni' Mji Mwema, Kigamboni, ambako alipelekwa mara baada ya kung'olewa madarakani mwaka '84.

Sikuwahi kubahatika kuonana na Alhaj Aboud Jumbe wakati wa uhai wake. Hata hivyo, nimejifunza mengi sana kutoka kwake, hasa ujasiri wa kuuhoji Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Jumbe amekuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye mjadala wa Muungano kwa zaidi ya miongo mitatu sasa. Ninadiriki kusema kwamba hoja ya Serikali Tatu ilianzia kwa Jumbe. Roho, spirit, yake ilikuwa kila mahali wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kati ya 2011 na 2014.

1471258418776.jpg

Kivuli chake kilikuwa kila mahali wakati wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014. Pengine kuliko hata Mwalimu Nyerere, Jumbe ndiye aliyetufundisha kuufahamu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Atakumbukwa kama mmoja wa waTanzania maarufu na wapigania uhuru wakubwa wa Zanzibar ya baada ya Muungano.

Adieu Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.
Adieu mTanzania jasiri.
Adieu shujaa wa uhuru wa Zanzibar.

Hili ni andiko la Tundu Lissu

[emoji767] copy rights reseved
[emoji768]revesed by Comred Mbwana Allyamtu

Napatika kwa mawasliano

Comred Mbwana Allyamtu.
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com
 
M/mungu akupe rehema..ulikua mtetezi wa kweli ndo maana ukawekwa kizuizini mpaka unakufa..sio hawa waleo leo anakamatwa kesho anatolewa wanaendelea kushirikiana kutuhujumu mpaka tunajiuliza nani bora kati ya watawala na wapinzani alimradi ghasia tu.
 
Lissu anasema 'watu wa usalama wa Mwalimu' ndio waliiba nyaraka zilizotumika kumsulubu Jumbe. Hebu Lissu awe muwazi na aseme nani aliiba nyaraka?

Swali hilo litakuwa gumu kwa Mh Lissu,kwanza alikuwa bado kijana mdogo.Pili Jumbe alifukuzwa na NEC ni nadra wajumbe wa NEC siku hizo kutoa nje siri za kikao.
Kupitia Radio Tanzania taarifa ya saa mbili jioni ilitangaza kuwa Jumbe amejiuzuru nyazifa zote za chama na serikali.
Watu wa kada mbalimbali hata bila kupitia mafunzo maalumu ya ukachero waliitwa watu walio kwenye system kwa maana wangeweza wakawakilisha tuhuma mmoja kwa mmoja kwenye ngazi za juu za utawala.Yawezekana hata typist akijiamini tu angeweza kuripoti nje ya utaratibu wa ofisi,na hiyo ndio ilivyokuwa miaka ile.
 
Interesting...
Mzee alikuwa jasiri sana.
Pumzika kwa amani.
 
Dah kweli tumetoka mbali!Yaani Jumbe anavuliwa nyadhifa zote asubuhi lakini wananchi wanapata taarifa saa mbili usiku,tofauti na sasa unavuliwa nyadhifa zote huku watu wapo jf wanajua majanga yanayokukuta kwenye mkutano muda huo huo
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?

hilo hajui
 
.

Nimeipenda sana comment yako hii...hapo ndipo unafiki wa wanasiasa unavyojionyesha wazi...Tundu Lissu hajasema chochote cha maana katika andiko lake...ameruka makusudi kuwataja wanasiasa waliomtumbukiza Jumbe mtegoni...Ndiyo maana mimi siasa sipendi kabisa....Lissu angefanya cha maana kama angewataja wote waliomhadaa Jumbe lakini kwenye kikao cha NEC wakaingia 'mitini'...Tundu Lissu asituambie chochote kuhusu suala hili baadhi yetu tunajua sana kilichotokea na hatuwezi kuweka hapa mambo hayo....Watu wanafiki sana, tena sana...naishia hapo...inaudhi sana
Watu kama nyinyi sijui ni
watu wa aina gani. Tunashindwa kabisa kuwaelewa.
Unamlaumu Lissu kwa madai kwamba ameshindwa kuwataja wote waliomhadaa Jumbe
Wakati huohuo wewe unadai unajua sana ila huwezi kuweka hapa hayo mambo
Sasa twambie wewe una uhakika gani kwamba Lissu anajua yote kama unavyojua wewe? Na kwanini unaogopa kuweka huo ukweli unaoujua wewe na wakati huohuo ukilaumu kuwa Lissu ameficha ukweli?
Je kwa watu ambao hawaelewi chochote nani hapo ataoneka ni wa maana kati ya wewe unayedai unajua mengi lakini huwezi kuweka hapa ama Lissu aliyethubutu kueleza japo hayo machache
 
Hiyo inaitwa "selective amnesia".

Maalim Seif alikula njama ma secretary wa Jumbe kuiba nyaraka za siri za Jumbe alizokuwa anatayarusha kuhusu muungano. Seif akampelekea Nyerere.

Ndiyo maaana miaka yote Seif na Nyerere walikuwa wanakutana kwa siri na hawasemi wameongea nini.

Na mpaka leo Seif hajasema vile vikao na Nyerere wameongea nini.

Inawezekana Nyerere kampandikiza Seif CUF na kumwambia wewe kaa huko watakupigia kura, sisi tutaiba ili tubaki CCM. Jifanye unakasirika, lakini watulize wasilete machafuko.

Who is to say that that is not the case na Seif anawafanyia kazi CCM mpaka leo?

Mmh!

mfupa huu

umenena mazito, magumu....
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Andika yako kuhusu Marehemu Aboud Jumbe; kama unataka kuandikanya Maalim Sefu subiri atakapokuwa marehemu kama CCM inavyohangaikia.
 
Hapa nakuunga mkono kiongozi! Ukweli lazima usemwe bila kujari unamgusa nani vibaya.
Haya yanatakiwa kujadiliwa vyumbani nadhani si yote mazuri kwa walaji
Issue za kijasusi zijadiliwe na wenyewe
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom