Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

.

Nimeipenda sana comment yako hii...hapo ndipo unafiki wa wanasiasa unavyojionyesha wazi...Tundu Lissu hajasema chochote cha maana katika andiko lake...ameruka makusudi kuwataja wanasiasa waliomtumbukiza Jumbe mtegoni...Ndiyo maana mimi siasa sipendi kabisa....Lissu angefanya cha maana kama angewataja wote waliomhadaa Jumbe lakini kwenye kikao cha NEC wakaingia 'mitini'...Tundu Lissu asituambie chochote kuhusu suala hili baadhi yetu tunajua sana kilichotokea na hatuwezi kuweka hapa mambo hayo....Watu wanafiki sana, tena sana...naishia hapo...inaudhi sana
Wewe unasema unajua sana kilichotokea na hauwezi kuweka wazi, kwanini sasa unamshikia bango Lissu aweke wazi, anza wewe kama huwezi piga kimya!
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Ieleze tuielewe basi, sisi tusioijua
 
Ieleweke hapa kuwa alichokiandika Lissu siyo makala ya kiuchambuzi kuhusu maisha ya Aboud Jumbe bali ni maelezo mafupi kuhusu wasifu wa marehemu (eulogy). Pia, shutuma kuwa Maalim Seif kumsaliti Jumbe ni uzushi ambao haujawahi kuthibitishwa popote; hivyo mwandishi yeyote makini hawezi kuingiza uzushi katika andiko lake.
 
Lissu amesema ukweli mtupu, Jumbe alikuwa jasiri sana, sio viongozi wa sasa wa zanzibar ambao wamewasaliti wazanzibar
Kwenye 'Vijana wa Usalama' ame edit for his own good. Ilibidi aandike "Maalim Seif aliiba ile Hati ya Mashtaka mezani kwa Mzee Aboud Jumbe na kumpelekea Mwl. Nyerere. Alifanya hivyo akijua kuwa Mwalimu atakasirika na atamwondoa madarakani. Akiishamuondoa, atamuweka yeye Maalim Seif". Tundu Lissu hata sisi tunaijua sana Historia.
 
Tundu mnafiki sana, mbona hajamtaja maalim sefu katika hili? Na Leo Lowasa kampongeza sana Jumbe kwa kuulinda na kuuimarisha muungano ambao Lissu anauponda! Sasa Kwanza Lissu hela kama za Lowasa hana! Mwisho wa siku anapozidi kupingana na mmiliki wa machadema ajue atafukuzwa fasta kama wenzake.
 
naona haujasoma vizuri mkuu..Lisu amendika hapo kuwa siri zitolewana wanausalama...unajuaje kati ya wanausalama hao hakuwa maalim....sio lazima atajwe mtu jina...
Kama si lazima atajwe mtu jina kwa nini kataja jina la Jumbe?
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Thread ya Jumbe, maalim seifu wa nini humu haya andika historia yako kuhusu seifu basi
 
Lissu anasema 'watu wa usalama wa Mwalimu' ndio waliiba nyaraka zilizotumika kumsulubu Jumbe. Hebu Lissu awe muwazi na aseme nani aliiba nyaraka?
Watu wa usalama huwa wanatajwa kwa majina? Au mumesahau kilichoiponza mwanahalisi
 
Inawezekana Nyerere kampandikiza Seif CUF na kumwambia wewe kaa huko watakupigia kura, sisi tutaiba ili tubaki CCM. Jifanye unakasirika, lakini watulize wasilete machafuko.

Who is to say that that is not the case na Seif anawafanyia kazi CCM mpaka leo?
Afadhali leo umeikiri kwamba CCM huwa wanaiba kura!!
 
Afadhali leo umeikiri kwamba CCM huwa wanaiba kura!!
Sio leo nimekiri.

Neno kukiri linaashiria kukubali ovu ulilofanya.

Mimi si CCM hivyo siwezi kukiri ovu la CCM.

Ninapoandika "sisi" hapo nibsauti ya Nyerwre akiongea na Hamad. Si sauti yangu. Comprehension please.

Pia, sijaanza kuandika haya leo. Labda wewe ndiye unayaona leo.
 
Kwa maelezo yako inaonesha umeunga mkono "maneno" ya Nyerere kwamba CCM wanamtumia Maalim kutuliza jazba za Wazanzibar CCM wanapoiba kura. Huko kuamini "kilichosemwa" na Mwalimu ndiko kukiri kwenyewe!!
 
Unafahamu maana ya neno kukiri? Unajua tofauti ya kukiri na kuripoti?

Umesema nimekiri, nimekiri nini?
 
Unafahamu maana ya neno kukiri? Unajua tofauti ya kukiri na kuripoti?

Umesema nimekiri, nimekiri nini?
Kukiri ni kukubali kuwa jambo fulani ndivyo lilivyo! Na wewe kwa maneno yako unakiri kwamba CCM wamempandikiza Seif Sharrif Hamad ili wao CCM wakiiba kura yeye awe anawatuliza wafuasi wa CUF hazira zao!!
 
Nanukuu

Kamusi Kuu ya Kiswahili.

Baraza la Kiswahili la Taifa.

Chapisho la 2015 la Longhorn.

Ukurasa wa 463.

Kiri.

Kubali kuwa umetenda jambo fulani.

Mathalani "Alikiri kuhusika katika ujambazi"

Ungama, wafiki, itika.

Mwisho wa kunukuu.

Kukiri ni kukubali jambo ulilotenda au kuhusika.

Mimi si CCM. Sijawahi kiwa CCM. CCM walivyomoandikiza Hamad sijahusika.

Nitakiri vipi jambo ambalo sijahusika?

Unaelewa maana ya kukiri?

Au unachanganya mtu anayeripoti kitu unafanya ripoti hiyo kuwa ni kukiri?

Jifunze kutumia maneno ya Kiswahiki kwa ufasaha ili usiharibu maana.
 
, wafiki, itika.
Jifunze kutumia maneno ya Kiswahili kwa ufasaha ili usiharibu maana.
Kwa nukuu uliyoifanya ina maana wewe umeafiki kwamba Hamad anatumika na CCM kuwatuliza wafuasi wa CUF CCM wanapoiba kura!!
 
Jifunze kutumia maneno ya Kiswahili kwa ufasaha ili usiharibu maana.
Kwa nukuu uliyoifanya ina maana wewe umeafiki kwamba Hamad anatumika na CCM kuwatuliza wafuasi wa CUF CCM wanapoiba kura!!
Nikiafiki wakati sijahusika nimekiri nini?

Unafahamu synonym ni nini?

Nikiafiki kwamba Lowassa ni mwizi nimekiri kwamba Lowassa ni mwizi?

Nitakiri vipi Lowassa ni mwizi wakati si mimi niliyehusika katika wizi huo?

Again. Unaelewa maana ya kukiri?

Au unachanganya synonym ya kukiri, kuafiki, kama kukiri?
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Hebu tutajie wewe boss
 
Back
Top Bottom