Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Tundu Lissu anavyomuelezea Marehemu Jumbe

Dah kweli tumetoka mbali!Yaani Jumbe anavuliwa nyadhifa zote asubuhi lakini wananchi wanapata taarifa saa mbili usiku,tofauti na sasa unavuliwa nyadhifa zote huku watu wapo jf wanajua majanga yanayokukuta kwenye mkutano muda huo huo
Wee acha mkuu,enzi hizo ilibidi taarifa ya saa mbili usiku isikupite.Ukisikia ngoma za mzee Morris jiandae kusikiza taarifa,sio kama sasa kuna njia nyingi za kisasa.Habari ya kwanza ni Raisi Nyerere kasema...... Habari ya pili Raisi Nyerere kasema.....na tatu hivyo hivyo.Ilibidi tusikilize taarifa kwa makini ili usije ukajitumbukiza matatani bila kujua
 
Na wewe andika au anzisha uzi ukimzungumzia yule Hamad Rashid Mohammed juu ya upekepeke kwa namna alivyo fanya kwa Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.

Kidogo na yule Amani Abeid Karume naye pia ndiye aliyeasisi Serikali ya umoja wa kitaifa.

Ukimfuatlia utagundua aligundua madhambi mengi sana na sio makosa tuu na sasa kama yuko against na baadhi ya mambo ya Serikali/CCM.

Ni mpuuzi pekee anayeweza kuamini tuna muungano wakati ukweli zaidi unaonekana Tanganyika kuikalia Zanzibar kimabavu!!

Lissu amesema ukweli mtupu, Jumbe alikuwa jasiri sana, sio viongozi wa sasa wa zanzibar ambao wamewasaliti wazanzibar

Maneno yako sahihi na hapo ni introduction tuu, kjna mengi sana ambayo waTanzania tukiyajua kuhusu huu Muungano tutakuwa vichaa kama sio wendawazimj au wehu.

Mwenyezi Mungu amlipe mema kwa NIA yake njema kwa wa Zanzibar na waTanganyika.

Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?

Hivi inawezekana kabisa Tundu Lisu angeweza kuandika andiko tofauti na hili?

Hivi haoni kuwa Aboud Jumbe pamoja na umuhimu wake na wasifi wake kama kiongozi alikosea mwenyewe timing? Inakuwaje a revolutionary leader aanze kupinga misingi yake aliyoianzisha mwenyewe?

Wakati huo Alijiongopea mwenyewe mwenyewe (tukiwa wadogo enzi hizo tulikaririshwa na kuimba

"Nyerere na Jumbe ni ndugu Moja, ndugu moja",

ki ukweli Mzee Jumbe namuona ni mwanasiasa maslahi na hana tofauti na Maalimu Seif, Lowasa, Mgeja, Msindai, Hamad Rashid, Lawrence Masha, Mpenda zoe, Mungai, etc.
Pumzika kwa amani Babu yangu, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, ulitimiza wajibu wako, tutajifunza mwengi kutoka kwako.
 
Kwa hapa Tanzania, ni Tundu Lissu pekee ndiye mwanasheria na mwanasiasa aliyejaaliwa ubongo mkubwa. Hii ni tunu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

..nashangaa.

..wakubwa wote waliofanya kazi na Mzee Jumbe wameshindwa kuandika tanzia?

..badala yake TUNDU LISSU ndiyo anaandika ya Aboud Jumbe Mwinyi?

..Ali Hassan Mwinyi, Salim Ahmed Salim, Jakaya Kikwete, Augustino Ramadhani, Maalim Seif, P
Pius Msekwa, ni baadhi ya vigogo ambao walifanya kazi na Mzee Jumbe.

.. tume za Nyalali, Kisanga, na Warioba zote zimependekeza serikali 3 maana yake ni kwamba Aboud Jumbe alionewa.

Cc Mohamed Said
 
Haya yanatakiwa kujadiliwa vyumbani nadhani si yote mazuri kwa walaji
Issue za kijasusi zijadiliwe na wenyewe
Nawasilisha
Mwenye ukweli na aseme sasa au anyamaze milele!
 
RIP Hero Jumbe, ila laana yako itawatafuna wengi kizazi na kizazi na hesabu wataitoa tu.
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?

Kwa hiyo akimtaja Maalim roho yako nyeupe kabisa ccm ni janga kubwa sana
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Kha! Yeye kaamua kumuongelea Jumbe, hayo ya Seif ni yako wewe.
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Andika yako na umtaje, mbali na hapo pessimism itaku ua!
 
Hotuba za namna hii ndio Mzee Jumbe alizikataa baada ya kufa kwake, unafiki na sifa alijua mapema!
 
lisu ameandika aliyoyaona anayepinga atuwekee ya kwakwe, mbona hata hstoria kwamba aliyekomboa zanzibar ni Okelo lakini hawakumwandika popote
 
Hapa fisi na nyumbu utawajua wanabase kwenye mahaba ya vyama vyao.
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Lisu ametoa maelezo ya Jumbe, sio ya Seif.
 
Hiyo inaitwa "selective amnesia".

Maalim Seif alikula njama ma secretary wa Jumbe kuiba nyaraka za siri za Jumbe alizokuwa anatayarusha kuhusu muungano. Seif akampelekea Nyerere.

Ndiyo maaana miaka yote Seif na Nyerere walikuwa wanakutana kwa siri na hawasemi wameongea nini.

Na mpaka leo Seif hajasema vile vikao na Nyerere wameongea nini.

Inawezekana Nyerere kampandikiza Seif CUF na kumwambia wewe kaa huko watakupigia kura, sisi tutaiba ili tubaki CCM. Jifanye unakasirika, lakini watulize wasilete machafuko.

Who is to say that that is not the case na Seif anawafanyia kazi CCM mpaka leo?
Maneno mazito haya, kwamba Maalim Seif alikuwa na vikao vingi vya siri na Mwl. Nyerere!!? Haki ya nani huu msiba unafumua mengi.
 
Hiyo inaitwa "selective amnesia".

Maalim Seif alikula njama ma secretary wa Jumbe kuiba nyaraka za siri za Jumbe alizokuwa anatayarusha kuhusu muungano. Seif akampelekea Nyerere.

Ndiyo maaana miaka yote Seif na Nyerere walikuwa wanakutana kwa siri na hawasemi wameongea nini.

Na mpaka leo Seif hajasema vile vikao na Nyerere wameongea nini.

Inawezekana Nyerere kampandikiza Seif CUF na kumwambia wewe kaa huko watakupigia kura, sisi tutaiba ili tubaki CCM. Jifanye unakasirika, lakini watulize wasilete machafuko.

Who is to say that that is not the case na Seif anawafanyia kazi CCM mpaka leo?

naona haujasoma vizuri mkuu..Lisu amendika hapo kuwa siri zitolewana wanausalama...unajuaje kati ya wanausalama hao hakuwa maalim....sio lazima atajwe mtu jina...
 
Tundu Lisu mnafiki mbona hajaweka mchango wa Maalim Seif sahariff hamad kwenye kung`olewa kwa Jumbe?.Naona anaruka ruka tu hakuna mahali anamtaja seif shariff hamad kwa kuwa anaye UKAWA anafikiri watu hawajui historia?
Ni mpaka ujue andiko hilo ni mahsusi kwa ajili ya kitu gani. Usifikiri kuandika ni kuandika tu kama ambavyo watu wanaandika facebook na siku hizi hapa JF!
 
Back
Top Bottom