Tundu Lissu anasema Tanzania itarudi na kombe la AFCON 2024. Tuungane kwenye mambo ya kitaifa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Mhe. Tundu Lisu anapasha misuli michuano ya Afrika huko Ivory Cost. Kauli mbiu yake ni moja tu TUTARUDI NA KOMBE.

Nimefurahi sana kumwona yeye na familia yake wameungana na vijana wetu. Amefanya nijifunze kwamba kwamba mambo ya kitaifa mzalendo namba moja ni huyu Bwana.

Anapigania rasilimali zetu, anapigania katiba yetu, amepigania wakati wote sheria za nchi na sasa amesimama kutetea bendera yetu kwenye michezo.

Katika yote haya hakuna siku amewahi kumwibia Mtanzania wala kumdhulumu, ni Mtanzania anayezeeka bila kula rushwa wala kupokea rushwa. Kila la heri Taifa stars cheers
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom