Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Kuanzia sisi tuliojaariwa uhai na mwenyezi Mungu sasa hadi vizazi vyote vinavyokuja vya Tanzania na hasa Tanganyika historia ya Nchi yetu hatutaisimulia kwa kuwaeleza kina Mkwawa au Nyerere kama mashujaa wa hili Taifa.
Kuanzia sasa historia ya nchi yetu hasa kwenye mapambano ya haki sawa kwa wote, utawala bora na matumizi sahihi ya rasilimali za Taifa kwa faida ya Watanzania wote jina TUNDU ANTIPASS LISSU litasomwa katika historia yote ya Tanzania na Tanganyika hadi mwisho wa hii Dunia.
Kuanzia sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kitasomwa na kutajwa na Watanzania kama alama kuu ya mapambano ya kweli ya Haki, Utawala Bora na Kuwatetea kweli Wananchi dhidi ya Udhalimu.
Namshukuru Mungu kuweza kuishi nyakati hizi. Mungu anipe Uhai ipo siku vitukuu vyangu vitaniuliza kuhusu huyu Lissu na hawa Chadema na Insha Allah nitakuwa sehemu ya kuwaelezea namna hawa watu walivyoandika upya Historia la Taifa letu.
Mungu mbariki Tundu Antipass Lissu
Mungu wabariki Chadema✊️✌️