Tundu Lissu ana A++ ya bunge

Wanajf naona mbunge wetu lisu anaendelea kuwaburuza wabunge wote wa bunge la tanzania.
Nimesukumwa na hoja ya kwamba ana uwezo wa kusimamia anachokisema(hateteleki),jana amenifurahisha sana pale alipokuwa ananukuu baba wa taifa kuwamaliza mafisadi jairo na wenzake.
Hivyo naaaamua kumpa A++ ya kazi nzuri
JE KUNA ANAYEBISHA???????KAMA WABISHA TOA SABABU

naunga mkono hoja mkuu,kinachompambanua lissu na wabunge wa magamba ni kwenye kujenga hoja na kuitetea.wote wanaojaribu kujibu hoja wanaishindwa kufanyahivyo zaidi wanaishia kuanzisha story na mipasho ambayo haijibu hoja.
Mfano. Katika hoja zake za msingi kuhusu uwakilishi wa wazanzibar katika mchakato wa katiba hakuna mbunge aliyejibu hoja hiyo kwa ufasaha.hata leo kwenye mdahao alitoa ufafanuzi jinsi gani katiba ya zanzibar inavyokinzana na ya jamhuri ya muungano na mnyaa ameshindwa kukanusha hilo zaidi kuanzisha story nyingine katika kukwepa hoja.
 
lakini muangalie msimamo wake unagusa zaidi maslahi na ustawi wa taifa au unajenga chama chake2,, maana hata anasahau kuwa wanaopiga kura cyo wote wanachadema,, na akumbuke cku watakapopata ridhaa ya kushika doka watakuwa na misimamo yao hiyo? hapana anaoneka ni mzuri2 kwa kuwa yupo nje lakini atakapokuwa ndani ya sistime hatotetea haya. Jinsi anavyojibu ni kuonesha tuu ufundi wa sheria lakini dhana nzima na nia vinamsuta.
 
Lissu ni jembe. Mkwe.re mwenyewe alisema singida bora wamnyime yeye kura za urais lakini wasimpe ubunge Lissu. Ni wazi Lissu wanamtambua!
 
JF imevamiwa! Hivi wewe ni da au ka?
Mboni waendhelea n'dhungusha shida yangu yakhe? wee ndo uliyenteua sasa yakuaje wataka n'geudhia paja badala ya n'gongo? waogopa kirungu weye dhio? ntafanya polepole badhi!
 
Ni muda mrefu sijachangia humu jamvini, ila hii
Thread ya Tundu lissu imebidi nijitokeze.
Jana nilimsikiliza Tundu Lissu akichangia hoja ya
Kamati teule, and to be honest he drove me to tears.
Niliguswa sana but in short inatupa picha madudu hayo yanafanyika ktk
Wizara zote.
Kitu kimoja nataka kuiasa serikali wao ndio wachokonozi wakubwa
Wa amani tuliyonayo.
Ebu mtu aniambie unakuwa na amani gani ambapo
Kila kukicha madudu yanafichuliwa jinsi hela$
Zetu zinavyotafunwa. Tunalipa kodi, cha maana out of that hatukioni.
Wajue wananxchi wamechoka na ni time bomb! Yakiharibika wasimtafute mchawi.
Wakujilaumu ni wenyewe.
Kuepukana na haya tendebi haki, wapeni wanachi haki jinsi
Ongozeni nchi kwa uzalendo na kwa kufuata miiko ya uongozi.
Punguzeni usanii- wananchi wamechoka.
Na ushauari wa bur watanzania Tuacheni UNAFIKI, unaturudisha nyuma badala ya kusonga mbele.
Kama mtu hachapi mzigo aambiwe, tusivikane vilemba vya ukoka.
Jamani tufkirie vizazi vijavyo na tuache tamaa za mbwa.
Ila naamini Mungu anatusimamia, na iko siku atatufunulia yote.
 
Rejeo sinto kushangaa unapokubali yaishe kimya kimya kama mzee wako kingunge aliyeshindwa kuiabudu hotuba ya jk alipokuwa na wazee wa dar...taratibu utakuja tuu it's the matter of time
Siwezi kukoment kwenye issue ambayo haina msingi.
 
Back
Top Bottom