Uchaguzi 2020 Tundu Lissu amjibu Magufuli: Kama kweli anampenda aseme wakina nani walimpiga risasi, na kwanini alimnyima pesa ya matibabu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,571
2,000
“Kwakuwa amesema ananipenda kama alivyodai akiwa Ikungi, Singida aseme ni akina nani walionipiga risasi 16,

Kwakuwa ananipenda aseme ni kwanini alininyima pesa za matibabu baada ya kupigwa risasi.." Mhe. Tundu A Lissu.

"Kwakuwa amesema ananipenda aseme ni nani aliyemkusudia auawe katika hotuba yake aliyoitoa wakati akipokea ripoti ya madini na kusema kuwa anamsumbua sumbua katika agenda yake ya madini na kwamba bora msaliti auwawe"-; Mhe Lissu

 

Southern Highland

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
8,381
2,000
Imagine wanakutana kwenye mjadala hawa
JamiiForums163011646.jpg
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,120
2,000
Magu ameshapaniki na Sasa dalili zinaonyesha ataviamrisha vyombo vya usalama kuchezea uchaguzi.

Na hapo ndio mtego wa Lissu ulipo

Yaani mwaka huu uchaguzi uwe huru Lissu mapema anachukua uchaguzi uchezewe watu waingie barabarani Jiwe akimbie Ikulu

Patamu Sana mwaka huu.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,609
2,000
Tatizo la mgombea wa CCM hana sera wala hoja nzito za kuweza kuwavutia wananchi, siku zote yeye huongea mambo rahisi rahisi tu ambayo yanaonekana ni yenye tija kwa watu wenye akili duni na upofu wa kufikiria. Viongozi makini duniani huwa hazungumzii vitu vyepesi ktk nyakati za kampeni za uraisi, bali hushusha nondo zilizojaa madini tupu.

Haya ndiyo mapungufu ya kiongozi wa nchi kukwepa kuongea ama kushauriana na viongozi wengine mashuhuri hapa duniani kwa kificho cha kubana matumizi. Kwa kuwa anajikuta hawezi kuongelea mambo muhimu yenye kugusa maslahi mapana ya Watanzania wenye fikra pana.
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,524
2,000
Hilo swali la Lissu ni gumu sana, haliwezi kujibiwa kamwe, ndio maana siku hizi jamaa yetu anaonekana mpole sana, anajua wakati huu wa kampeni mengi sana yatasemwa, hasa yale asiyopenda kuyasikia, namshauri awe mvumilivu sana.
Kama angeacha wapinzani waongee na magazeti na TV ziwe huru, wapinzani wasingekuwa na ya kuongea sasa hivi. Kinyume chake sasa hivi Magu hana jipya, watu wamewamiss wapinzani
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Tbc simuliwafukuza wenyewe, na utube nao wameminywa? Nyie vipi?

Unajitoa ufahamu? Inaitwa unajifanya hamnazo? Wewe hujui kwa nini TBC alifukuzwa? Hujui alikuwa anatekeleza maagizo tokea mbinguni?

Subiri kidogo sindano iwaingie.

Tafuta za namna nyingine maana huenda hata zile risasi 16 utakuwa unadhani kuwa jiwe anasingiziwa tu.

Bila shaka yalikuwa ni mawe ya manati.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
5,077
2,000
Magu ameshapaniki na Sasa dalili zinaonyesha ataviamrisha vyombo vya usalama kuchezea uchaguzi.

Na hapo ndio mtego wa Lissu ulipo


Yaani mwaka huu uchaguzi uwe huru Lissu mapema anachukua uchaguzi uchezewe watu waingie barabarani Jiwe akimbie Ikulu

Patamu Sana mwaka huu.
😂😂, Watu waingie barabarani, jiwe akimbie wapi😲? Hata sisi tunauwezo wa kuingia road kumpambania,msitutishe na slogan zenu mitamdaoni ambazo hamuwezi kizitekeleza.Tutadeal na kila kima, atakaejaribu kuleta upumbavu.🚶🚶🚶🚶
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,150
2,000
Unajitoa ufahamu? Inaitwa unajifanya hamnazo? Wewe hujui kwa nini TBC alifukuzwa? Hujui alikuwa anatekeleza maagizo tokea mbinguni?

Subiri kidogo sindano iwaingie.

Tafuta za namna gani? Hata zile risasi 16 utakuwa unadhani kuwa jiwe anasingiziwa tu.

Bila shaka yalikuwa ni mawe ya manati.
Joni kwanza, muliwafukuza? Na youtube je? Chadema media Nani kaifungia?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom