Familia ya Tundu Lissu yamrushia lawama rais Magufuli kuhusu upelelezi na Matibabu ya ndugu yao

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884

Heshima kwenu wakuu,

Msemaji wa familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, mnadhimu wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni na aliyekuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika Mheshimiwa Tundu Lissu, wakili Alute Mughwai, amelalamikia Serikali ya rais Magufuli kutoonesha dhamira ya kumtibu ndugu yao. Ameyasema hayo wakati akitoa mrejesho wa maendeleo ya afya yaTundu Lissu kwa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS).

"Serikali haina dhamira ya kupeleleza watu waliompiga risasi Lissu". Amesikika Alute akisema.

Msemaji huyo wa Familia amesema, familia imeshaonana na kuongea na Waziri mkuu kwa masaa mawili, Familia ilikaa na kufanya mazungumzo na Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa masaa mawili, Familia ilikaa na kufanya mazungumzo na Spika wa bunge kwa masaa manne lakini wote hawatoi jibu linaloeleweka. Spika alisema kwamba hahudumiwi sababu hakufuata taratibu za kwenda kutibiwa Kenya.

Familia inaitaka Serikali iruhusu Wapeleleze na wachunguzi kutoka nje ya nchi ambao walikubali kufanya uchunguzi tena bure, waje wafanye uchunguzi wa watu walimpiga risasi ndugu yao ukweli ujulikane.

Ombi lao la pili wanataka bunge litoe posho na matibabu kwa ndugu yao kwani hilo swala lipo kisheria. Wabunge wengine wakiwa wanaumwa wanahudumiwa na bunge mgonjwa na msaidizi wake. Ikiwemo sitahiki zake kama mshahara na marupurupu mengine, lakini bunge lilikataa wala halitaki kujua mgonjwa ambaye ni mbunge mwenao anaendeleaje.

Amesema Lissu anaendelea Vizuri na akifika atataka haki yake na familia tutamuunga mkono.

Kasema sasa Lissu anaendelea vizuri na anatia moyo, ila kuhusu swala la kurudi haijulikani atarudi lini.

Amesema kwa sasa wanaongea na Washauri wa familia nini cha kufanya, lakini chaguo lao la kwanza ni kudai haki yao mahakamani. Hakuna sheria ilipoandikwa kwamba mtu akiumwa aombe ruhusa kwa rais ya kutibiwa bali sheria inasema mbunge akiumwa atahusumiwa na bunge yeye na msaidizi wake.

Baadhi ya Mawakili wamesema hiyo ipo wazi. Mtu aliyekataza na kutoa amri Tundu Lissu na Maalim Seif wasitibiwe watakapoumwa anafahamika.

Wakili ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisema hili swala TLS watahakikisha wanapata haki ya Wakili mwenzao. Amesema Wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hawajawahi kuogopa na hawataogopa vitisho.

Familia imewaomba Mawakili wote wa TLS wawaunge mkono pindi watakapoenda Mahakamani.

Hivi karibuni Serikali iliilaumu CHADEMA kwamba ndio inayochelewesha uchunguzi.

Ilisema mara nyingi wamekuwa wakitaka ushirikiano kutoka CHADEMA bila mafanikio

Yadaiwa CHADEMA wamekuwa wakimficha dereva wa Lissu

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Massauni aliyasema hayo Bungeni wakati akijibu swali la Saed Kubenea(Mb) aliyehoji ni lini Serikali itakamilisha uchunguzi wa matukio ya uhalifu yanayofanana na ugaidi likiwemo la Tundu Lissu
 
Kwa mujibu wa taarifa yake mwenyewe Jiwe, amesema hadharani kuwa yeye ni kichaa na anateua vichaa wenzie katika teuzi zake!

Kwa hiyo unategemea nini hapo??

Hivi Waziri mwenye akili zake timamu anaweza kweli kufanya kitendo kama alichokifanya yule Waziri aliyetajwa na Jiwe kuwa kamteua kutokana na ukichaa wake, kwenda na rula Bungeni na kuanza kuwapima samaki ambao tayari wamekaangwa??

Kwa hiyo hatushangai hata maamuzi yao nayo yanakuwa ya ukichaa kichaa!
 
Key Word

Baadhi ya Mawakili wamesema hiyo ipo wazi. Mtu aliyekataza na kutoa amri Tundu Lissu na Maalim Seif wasitibiwe watakapoumwa anafahamika

Mungu mbariki Tundu Lissu....
 
Inasikitisha sana. Kwa hili, Mungu hatakuwa Athumani. Ni suala la muda tu. Hakuna mwenye fedha. Fedha zote ni mali ya serikali ambao ni wananchi wenyewe. Cheo ni dhamana na uhai ni wa Mungu pekee.
 
Kwa nini hawakufata yanayotakiwa mwanzo..

Lilivyo gazeti wameomba msamaha kwa kumsingizia kutaka kumuua huyo ndugu yao.. na kufurahia chama chake kubwabwaja mambo ya ajabu juu ya huu utawala?

Wajitafakali sio kwamba wameona wamekimbiwa na wanaochochea maovu nchini na kuanza kulia lia.

Waombe msamaha kwa mchi nzima tena Lissu mwenyewe and co
 
..waziri mkuu mazungumzo ya masaa 2.

..Spika mazungumzo ya masaa 4.

..Mwanasheria Mkuu mazungumzo ya masaa 4.

..wote hao wameshindwa kumsaidia mbunge mwenzao?

..Tumefikia hatua mbaya sana ya UKATILI.
Inashangaza ati na wao hawakuweza kutoka majibu na kutatua suala hilo! Kama hata PM, Spika nao wameshindwa basi kiti cha enzi pale Jumba Jeupe ndio kikwazo.

Vv
 
Kwa nini hawakufata yanayotakiwa mwanzo..

Lilivyo gazeti wameomba msamaha kwa kumsingizia kutaka kumuua huyo ndugu yao.. na kufurahia chama chake kubwabwaja mambo ya ajabu juu ya huu utawala?

Wajitafakali sio kwamba wameona wamekimbiwa na wanaochochea maovu nchini na kuanza kulia lia.

Waombe msamaha kwa mchi nzima tena Lissu mwenyewe and co
Fungua akili dada, akina nani hao ambao hawakufuata yanayotakiwa? Mhanga na majeruhi anahusishwa namna gani kwenye hilo sakata la kufanya wanayotakiwa?

Vv
 
Kwa nini hawakufata yanayotakiwa mwanzo..

Lilivyo gazeti wameomba msamaha kwa kumsingizia kutaka kumuua huyo ndugu yao.. na kufurahia chama chake kubwabwaja mambo ya ajabu juu ya huu utawala?

Wajitafakali sio kwamba wameona wamekimbiwa na wanaochochea maovu nchini na kuanza kulia lia.

Waombe msamaha kwa mchi nzima tena Lissu mwenyewe and co
Watanyoosha tu maelezo, ujuaji juaji huku mnamgonjwa wapi na wapi? Mara matusi , mara kutishia viongozi , yote yatawatoka mpaka mjue kunyenyekea ni sehemu ya ustaarabu.
 
Back
Top Bottom