Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
HABARI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani
Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amemhoji Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani sababu za kutoshtakiwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, Rais Ali Mohamed Shein na Hassan Nassor Moyo waliotajwa kwenye makala inayodaiwa ya uchochezi.
Lissu alimuuliza swali hilo Kamanda Hamdani aliyekuwa akitoa ushahidi jana kwenye kesi ya tuhuma za uchochezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika Mahakama ya Kisutu.
Kamanda Hamdani aliyekuwa akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi alikumbana na swali hilo ulipofika wakati wa maswali ya kuhoji kutoka upande wa utetezi.
Lissu alitilia mkazo swali hilo kwa maelezo kwamba Kamanda Hamdani ndiye mlalamikaji na kiini cha kesi hiyo. Washtakiwa wengine ni, Jabir Idrissa na Simon Mkina ambao kwa pamoja wanadaiwa kuandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Akijibu swali hilo la Lissu, Kamanda Hamdani alisema Rais Shein, Maalim Seif na Moyo hawajashtakiwa katika shauri hilo na kwamba yeye hana jukumu la kuwafungulia mashtaka.
Lissu aliendelea kumuuliza shahidi huyo wa upande wa mashtaka kwamba katika maelezo yake (Kamanda Hamdani) ya polisi aliwataja Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Rais Dk Ali Mohamed Shein na Mwanasiasa Mkongwe, Hassan Nassor Moyo na kusema maneno yao hayakuwa ya uchochezi.
Hata hivyo, Kamanda Hamdani alijibu swali hilo kwa kusema kuwa hakuwataja.
Lissu alimuonyesha shahidi huyo gazeti la Mawio la Januari 14, 2016 na kumtaka amweleze Hakimu Simba idadi ya aya za makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa na kichwa cha habari cha ‘Machafuko yaja Zanzibar’.
Baada ya kuulizwa swali hilo, Kamanda Hamdani alimueleza Lissu kuwa hawezi kuzihesabu, lakini mahakama ilitoa maelekezo azihesabu, akaomba muda akapewa, akazihesabu kuwa zipo nane.
Lissu alidai kuwa yeye amezisoma zipo 55 na kwamba aya 37 ni za maneno ya Maalim Seif, aya nane ni za maneno ya Tundu Lissu, aya nne ni za maneno ya Moyo na kwamba kwenye aya tatu, ametajwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Kamanda Hamdani alidai kuwa ni sawa.
Aliendelea kumhoji shahidi huyo wa upande wa mashtaka kwamba:
Lissu: Kwa uelewa wa akili yako anayetajwa mara nyingi kwenye makala hiyo inayodaiwa kuwa ni ya uchochezi ni nani?
Kamanda Hamdani: Maalim Seif.
Lissu: Wakati unaisoma makala hiyo ulibaini kuwapo kwa matamshi ya chuki na uchochezi dhidi ya Serikali ni kweli ama si kweli?
Kamanda Hamdani: Ni kweli.
Lissu: Kwa uelewa wako mtu anayetoa matamshi yenye kuibua hamasa au chuki dhidi ya Serikali ni lazima uwe uchochezi?
Kamanda Hamdani: Kwa uelewa wangu ni lazima uwe uchochezi.
Lissu: Alimuonesha shahidi huyo hati ya mashtaka na ya maelezo ya awali (PH) na kuuliza ni sawa nikisema makala nzima ya ‘Machafuko yaja Zanzibar’ ilikuwa ni makala ya uchochezi?
Kamanda Hamdani: Ni kweli.
Lissu kama makala yote ni ya kichochezi wote walioshiriki ni wachochezi?
Kamanda Hamdani: Ni sahihi.
Lissu: Ni kwa nini Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Rais Dk Ali Mohamed Shein na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo hawajashtakiwa, kwa nini Tundu Lissu pekee ameshtakiwa?
Kamanda Hamdani: Jukumu hilo siyo la kwangu, mimi ni mlalamikaji.
Lissu: Kwenye lengo lako mbaya wako alikuwa ni Tundu Lissu?
Kamanda Hamdani: Hapana sina ubaya na Lissu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 3, itakapoendelea kusikilizwa.
Chanzo: Mwananchi

- Lissu alimuuliza swali hilo Kamanda Hamdani aliyekuwa akitoa ushahidi jana kwenye kesi ya tuhuma za uchochezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika Mahakama ya Kisutu.